Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Mbu

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani ni kuwa shimo lilikuwa limechimbwa kabla ya siku ya tukio na ndio maana akatajwa kuwa alikuwa na dhamira ya kumuuwa

Kwa mujibu wa maelezo ya huyo Bi Asha pia ni kuwa alimchukua chooni na kumfunga na shuka alilolimwagia mafuta ya taa na kumchoma [kidogo] ili damu isite kutoka

Pia kwa mujibu wa maelezo hayo hayo, ni kuwa baada ya hapo alimzonga na mkeka/jamvi na kwenda kumfukia bustanini

Hakuna maeleo yanayosema kuwa alimkata kata viungo
 
Mbu;

Mkubwa, while sipingani na wewe - querry yangu kubwa ni kuwa kuna maswali mengi zaidi ya majibu - mfano umezungumzia swala la kumchoma moto ni kitu ambacho kisingewezekana kwa sababu mtaani wote mngejua (i totally agree with you.
lakini kwenye hukumu pia wameongelea kuwa alimchoma moto na wakaikubali hiyo - sasa huoni kuwa inawezekana mahakama inaweka many "reasonable doubt" kwa mazingira haya?
 
Mtambuzi;

Tuletee na ile kesi ya yule mama ALIETAKA KUIFILISI TANZANIA, simba ...... yaani bora yule angesepa na ile chenji bwana kuliko sasa hivi...
 
gambachovu;

Yule mama alikuwa kule gerezani Morogoro sidhani kama alinyongwa huyu mama mwenye data atupe tafadhali
 
Tsidekenu;

Ingekuwa ni vyema wanasheria wetu kama wangekuja kututegulia hiki kitendawili.
 
Gaijin

Ni kweli kabisa, huku mitaani wengi wanadai alimkatakata viungo na kumuweka kwenye gunia kisha akamzika..........Lakini kama ilivyoelezwa pale mahakamani wakati kesi ikiunguruma, hakuna mahali ilisemwa au ilitamkwa kwamba alimkatakata na kumuweka kwenye gunia na kisha kumzika..............Labda kama atajitokeza mmoja wa mashuhuda atuelezee kilichojiri, vinginevyo basi huo ulikuwa ni uzushi tu wa watu wa Dar...............
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umesema vyema. Manake kuna mwanamke huyo mmoja wa makamo, kumchoma moto mtu, kumzonga na mkeka, kumburuza hadi bustanini, kumzika, bila ya majirani kuona kweli asubuhi hiyo ya saa tano?

Kwa nyumba za upanga ianwezekana sana na tukumbuke kipindi hicho hata watu walikuwa hawakatizi sana upanga.
Unaweza ukakatiza mtaa peke yako mwanzo mwisho
 
Asprin;

Imani yake inamwambia kuwa MUUAJI NA YEYE LAZIMA ANYONGWE HADI KUFA, BAADA YA KUPATIKANA USHAHIDI WA KUTOSHA, kwa hiyo naona ni sawa tu, aliua kwa kukusudia na yeye LAZIMA auawe !
 
Gustavo u made my friday!
Kwakweli nakumbuka nikiishi mitaa ya upanga nikiwa bado kidogo
Hili tukio lilinijengea woga sana

Kumbe hawa mapolisi wameanza long kupuuzia mambo
Labda wangemfungulia mashitaka huyu mwenye vitisho na kumpa karipio kali labda ingeepusha kifo cha huyu dada

Eh mungu katuhukumu sawasawa na maovu yetu
 
Mkuu Mtambuzi
Asante sana kwa kuandika habari/hadithi nzuri kwa mpango mzuri na lugha fasaha
Ahsante mkuu, najitahidi kuienzi lugha yetu ya KISWAHILI, ili wale tusiosoma academia tupate kujifunza.................
 
Gaijin;

...naam, naam....ndio maana tangu awali nilisema tufuate ushahidi wa mahakamani...
Maana hearsays pia zilikuwapo...
Kuna waliosema siku hiyo walikutana A'port walipokwenda msindikiza profesa...

Mama Haule akamshawishi bi Happy waende 'home' wakayaongee....
Anyway, asante kwa kumbukumbu hii..
 
Mbu
Mimi nilisikia, eti Asha alimwalika Happy nyumbani kwake akamsuke nywele, na wakati kakaa kitako akisubiri kusukwa akatwangwa na lichuma lizito kichwani na Asha akafariki.................Kwa kweli yalisemwa mengi sana...............
 
Inasikitisha sana
napenda kujua kwa hiyo asha alishanyongwa au anatumikia kifungo cha maisha??
Sijawahi kuisikia hii story

Inasikitisha kwa kweli. Sheria nayo haiko fair,kwa nini chanzo cha yote hayo(wanaume) hawaguswi?
 
....hizi kesi miaka ile ya RTD na Ben Kiko, magazetI ya Uhuru, Daily news na Mzalendo ndio maana
habari ilishika kasi ya ajabu...

Miaka hii ya dot com yanatokea haya watu mnajionea kawaida tu...majuzi kati hapa kuna mwanamama mke wa "kigogo"
Wa Ikulu (inavyosemekana) ...,nusura nusura naye na binti Sepetu...hata kwenye magazti ya Shigongo walitoa picha za magari yao yalogongana

....na kuna mengineyo mengi tu watu hawashtuki tena...
 
Back
Top Bottom