Anayejua namna ya kutengeneza bagia za kunde

Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
852
Kwa anayeweza kunipatia hiyo recipe ya kuandaa bhajia za kunde anisaidie,
Thenx in advance.
 
Mimi pia ni mpenzi wa hizo bagia ila kwa kuzitengeneza mwenyewe si kwa kuzinunua mtaani au kula hotel coz maandaliz yake sijui wanafanyaje zinakuwaga na mchanga sana.Karibu!!!!
Bajia Za Kunde

Bajia%20Za%20Kunde.jpg

VIPIMO

Kunde za kupaaza 1 ½ Vikombe (hizi kunde kwetu tunaziita (njoombo)

Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa ½ Kikombe

Baking soda ¼ Kijiko cha chai

*Bizari mchanganyiko 1 Kijiko cha chai

Maziwa 2 Vijiko vya supu

Chumvi 1 ¼ Vijiko vya chai

Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu

Mafuta ya kukaangia

* Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
  2. Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.
  3. Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
  4. Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
  5. Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
  6. Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
  7. Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.
Kwa hapo unaweza kuserve kwa chai, maziwa,juice au chochote unachopenda wewe!!
 
theenx ameline. . .nazipenda kweli, zinakua na mchanga coz wengi kunde wanazisaga na mawe instead ya kwenye mashine.
One more thing. . .ni pm nikuulize kitu.
 
Last edited by a moderator:
Amelina nisaidie jinsi ya kutoa yale maganda kwa urahisi maana siku moja niilijaribu kupika niliziloweka usiku wote halafu asubuhi nikawa natoa maganda kwa mkono nilipochoka nikazisaga hivyohivyo. hazikunipendeza hata kidogo kwa ajili ya ule muonekano wa magandamaganda na bahati mbaya nilikula zikanivuruga tumbo. ila nazipenda sana.
 
pole sana mwaya, kuna kunde za aina mbili, kuna zile nyembabaa ambazo kweli zinasumbua sana maana ni ngumu kwelikweli zinakua kama choroko hivi, halafu kuna zile kubwa kias ila hazifikii ukubwa wa mbaazi, zile ni laini na ukiziloeka weka chumvi kidogo na asubuhi ukizifikicha zinatoka kwa urahis kabisa. zile nyembaba zinasumbua. ukisaga na maganda zinapoteza ladha kias fulani..best of luck
 
du kweli asante umenifungua macho na kuongeza ufahamu kwenye ubongo lazima hili pishi niliwin.
 
rubi,huwa mimi nachambua kunde zangu kwa kuzitoa mawe na uchafu,halafu nazitoa maganda kwa kuzisaga kidogo kwenye blander(ya kusaga vitu vigumu),halafu nazitia kwenye ungo napeta maganda yote,halafu ndo naloweka kwenye maji(hapa waweza roweka asubuhi mpaka jioni),halafu nachuja maji(ikiwa maji ni mengi) kisha naweka kwenye blander pamoja na viungo(angalia list ya viungo alivotaja amelina),kisha nachoma kwenye mafuta
rubi nadhani nimekusaidia jinsi ya kutoa magada
 
Jamani nimeloweka kunde tokea asubuhi ili niandae bagia...naona uvivu kuzisaga nitengeneze bagia sasa...vipi nikiendelea kuziloweza hadi kesho asubuhi nitakuwa nimeharibu?

cc farkhina...mwari wako mvivuuuuu!
 
Last edited by a moderator:
Jamani nimeloweka kunde tokea asubuhi ili niandae bagia...naona uvivu kuzisaga nitengeneze bagia sasa...vipi nikiendelea kuziloweza hadi kesho asubuhi nitakuwa nimeharibu?

cc farkhina...mwari wako mvivuuuuu!

Ahhahahahaha mwari kila siku huishi kuntia aibu weye
 
Last edited by a moderator:
Jamani nimeloweka kunde tokea asubuhi ili niandae bagia...naona uvivu kuzisaga nitengeneze bagia sasa...vipi nikiendelea kuziloweza hadi kesho asubuhi nitakuwa nimeharibu?

cc farkhina...mwari wako mvivuuuuu!

Hua hazina neno ila uwe unazibadili maji.....
 
Last edited by a moderator:
Thanx...ila asubuhi nlikuta zimeanza kuota ...lol...nikazitia pilau masala kupunguza ladha ya uchachuu....zilikuwa tamu.

Itakua tangu ulipoziroweka jana yake hukubadil maji. Mie huzibadili maji kila masaa mawili au matatu na ukiamua kuzilaza ziweke kwenye fridge na maji yake
 
Jamani hivi hizi kunde tunazoongelea hapa ndio zile kunde ambazo tunakula majani yake(majani ya kunde)
Mi natamani kujaribu Ila sijaelewa vizuri.
 
Amelina nisaidie jinsi ya kutoa yale maganda kwa urahisi maana siku moja niilijaribu kupika niliziloweka usiku wote halafu asubuhi nikawa natoa maganda kwa mkono nilipochoka nikazisaga hivyohivyo. hazikunipendeza hata kidogo kwa ajili ya ule muonekano wa magandamaganda na bahati mbaya nilikula zikanivuruga tumbo. ila nazipenda sana.
Kuna ambazo huuzwa sokoni zikiwa zimeshatolewa maganda ingawa huwa bei juu kidogo uwe unatafuta hizo kama huitaji usumbufu
 
Mahitaji
Kunde zisizo na maganda nusu kilo
Vitunguu maji 3
Vitunguu saumu 2
Chumvi
Mafuta
Pilipili 1

Maelekezo
Weka maji kwenye sufuria, beseni au chombo chochote.
Weka kunde kwenye hayo maji uziloweke, mimi huwa napendelea kuziloweka usiku mzima ili zilainike vizuri.
Andaa viungo, kata vitunguu maji vipande vidogo sana, vitunguu saumu menya weka kwenye chombo na pilipili ikatekate.
Chukua blenda, toa kunde kwenye maji, ziweke kwenye blenda.
Weka vitunguu maji, vitunguu saumu, pilipili na chumvi humo ulipoweka kunde
Ongeza maji kidogo sana,upate urahisi wa kusaga. Hakikisha unaposaga kunde zimelainika na viungo ulivyoweka vimesagika vizuri.
Hakikisha pia mchanganyiko hauwi mwepesi, bandika sufuri jikoni, weka mafuta yakipata moto, chukua kijiko chota ule mchanganyiko, weka kwenye mafuta.
Usigeuze mpaka uone chini imeiva vizuri geuza upande wa pilipili, ukiona imeiva epua, chuja mafuta hapo ni tayari kuliwa.
 
Inaonekana tamu, sasa kutoa maganda kunde si itabidi niziloweke kwanza?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom