AN OPEN LETTER to BAE Systems: Do not return radar money to Tz Government

nimesoma maelezo kuhusu hii charge ya rada kurudi kwenye website ya BAE
kumbe kulikuwa hakuna haja ya kutuma wabunge kwenda uk
walikuwa na uwezo wa kutengeza agreement hapa hapa nyumbani maana
board iliyoundwa inamsikiliza kila mtu.

ni nini kilichowapeleka hawa wabunge wetu huko uk
----serikali haitaka kutumia njia za maandishi kama e-mail/kukwepa kukwepa report!!!!
----- wabunge waliotumwa yawezekana wamekwenda kupiga magoti kwa BAE bila hoja ya msingi
----matumizi mabaya ya pesa ya serikali na porojo
---- kuna kitu wanajaribu kutuficha wananchi wa tanzania kwenda kuyafanyia uingereza hali wana ubalozi hapa

misingi yote nimeitoa kwenye hii barua kwa sasa ni na hakika hiyo pesa ni ya kuliwa

[h=1]BAE Systems forms advisory board on Tanzania[/h]17 Jun 2011 | Ref. 110
BAE Systems today announces the formation of an advisory board on Tanzania.
The Board will be chaired by Lord Cairns. Philippa Foster Back, OBE will serve as Deputy Chair. Additional independent members will be appointed to the Board in due course with the agreement of the Chair and Deputy Chair.

The Company will be represented on the Board by four senior executives; Philip Bramwell (Group General Counsel), Linda Hudson (President & CEO of BAE Systems, Inc), Charlotte Lambkin (Group Communications Director) and Lawrence Prior (Executive Vice President of Service Sectors for BAE Systems, Inc) who will act as the Executive Liaison members.
BAE Systems has made sustained efforts to become recognised as a leader in responsible business conduct. The formation of this Board forms part of this process and is in line with the settlement agreement with the Serious Fraud Office (SFO), approved by the Court in December 2010. As part of the settlement BAE Systems agreed to pay the sum of £29.5 million for the benefit of the people of Tanzania. The Company is now holding the sum as a fund in a treasury account and will confirm with the SFO the payments made from this account are consistent with the settlement agreement.
The independent members of the Advisory Board will guide the Company as to the optimum means of applying the £29.5 million for the benefit of the people of Tanzania in accordance with all applicable company polices. In addition to disbursements from the fund, the Company is willing to explore opportunities to enhance its overall contribution by utilising its advanced technological capabilities to maximise the effectiveness of projects supported by the fund.
Lord Cairns said: "I welcome the opportunity to Chair this Advisory Board. It provides us with a great opportunity to deploy this substantial fund in a way that will provide sustained benefit as Tanzania advances down the path to full development. I look forward to working with my fellow Board members, the company and others with relevant knowledge to deliver this important piece of work."

Notes to editors
[h=4]Advisory Board on Tanzania - biographies of Independent Members[/h]Lord Cairns
An investment banker by profession, Lord Cairns has had a long and distinguished career in both the business and the voluntary sectors. He served as both CEO and Deputy Chairman of S G Warburg plc, Chairman of BAT Industries plc and Chairman of Allied Zurich.

He has also served as Chairman of the Charities Aid Foundation, Chairman of Voluntary Service Overseas, Chairman of the Overseas Development Institute and Chairman of the Commonwealth Business Council. He was a trustee of the Princess of Wales Memorial Fund.

Lord Cairns has extensive experience of Africa through many of the above. He was also for 10 years Chair of the Commonwealth Development Corporation which made substantial investments both in Tanzania and across other African countries. He was Chairman of the African mobile communications company Celtel International (which became Zain Africa BV). He is currently a board member of the Mo Ibrahim Foundation.

Philippa Foster Back, OBE
Philippa has 30 years of business experience, having begun her career at Citibank. Following nine years at Bowater, leaving as group treasurer, she became group finance director at DG Gardner Group, a training organisation. She joined Thorn EMI in 1993 as group treasurer until 2000. She was appointed Director of the Institute of Business Ethics (IBE) in 2001.
In connection with her IBE role she served on the Woolf Committee 2007/8 looking at ethical business practice in BAE Systems plc; and has been appointed to the Advisory Board of the Centre for Corporate Reputation at the Said Business School at Oxford University and consequently as a Visiting Fellow of the University.
She sits on the Boards of the Institute of Directors and of the Norfolk and Norwich University Foundation Trust Hospital, where she chairs the Audit Committee. She is also Chairman of the UK Antarctic Heritage Trust.
Philippa was awarded an OBE in the New Year Honours 2006 for services to the Ministry of Defence where she was a NED and chaired the Defence Audit Committee from 2002-2007. In July 2008 she was awarded the Marks & Spencer Sieff Award.

[h=4]For more information, please contact:[/h]Lindsay Walls, BAE Systems
Tel: +44 (0)1252 383074 Mob: +44 (0)7793427582
Lindsay.walls@baesystems.com
Leonie Foster, BAE Systems
Tel: +44 (0)1252 383777 Mob: +44 (0)7540 630168
[h=4]Issued by:[/h]BAE Systems, Farnborough, Hampshire GU14 6YU, UK
Tel: +44 (0) 1252 384719 Fax: +44 (0) 1252 383947
www.baesystems.com

Natumaini tumeona jinsi wahisani wanavyo kamilisha miradi wakiisimamia wao wenyewe,mfano mzuri shule zinazojengwa na JICA.Kwa hiyo naona chenji ya rada isimamiwe na NGOs makini kwa maendeleo ya Watanzania lasivyo fedha hiyo isubiri serikali makini yaani CDM 2015.
 
Wewe Naibu Spika Ngugai unasema..................eti kwenye mauzo.........BAE walikosea kuandika invoice...............huna akili wewe!!............
 
..And you call ya self a great thinker! how can a great thinker write such a rot? you are ruining the imge of the JF!! kama kuna ki-ngo umeanzisha ukidhani zitapitishiwa kwako, ulie tu. andika kwa kila umdhaniaye hela itakuja serikalini tu. Ningekuona una akili japo kidogo kama unge toa proposal hiyo pesa itumikeje ikija lakini kusema isirudishwe halafu useme una uchungu na nchi si kweli! ww ni sawa na mla rushwa yeyote yule aliyepo TZ. Shame on you and the likes of you!

BAE wants to pay to the Education cause directly, Tanzanian governments wants the money in their hands first. But when you think about BAE should stop discussing how Tanzania will use this money and just give it back. If it were any other country that would be the noble thing to do.
But corruption cases in Tanzania are so serious that even BAE is scared to give back the money 'they stole' in fear that they will lose it to people people who will re-steal it. Get it?
 
WAWAKILISHI WA BUNGE TZ WAKIONGEA KUHUSU BAE RADAR

Last edited by a moderator:
Ahsante sana kwa clip.
Nimekuwa disappointed si kwa ujumbe wa Ndugai na majibu, bali kwa hao wanaoitwa waandishi wa habari na wote walioaanda mazunguzo haya.
Naomba kama kuna uwezekano yawepo mahojiano na KHL (mwanakijiji).
Nasema hivi kwasababu ni wazi kabisa hao waliouliza maswali hawajui undani wa suala lenyewe au wamekirimiwa. Insikitisha sana.
Niliangalia mahojiano ya Ndugai na BBC (Zuhura Yunus) yalivyokuwa bora kuliko haya.

Ndugai ameeleza kuanzia hukumu iliyotolewa kama anavyotuimbisha waziri Membe. Wasichosema ni chanzo cha wizi, yaani wanataka tuangalie tulipoangukia na si kujikwaa

Kwanza walitakiwa waulize hiyo kamati maalumu imeundwaje na kwa utaratibu gani tukizingatia Membe alifikisha jambo hili bungeni kwanza.
2.Wlitakiwa waulize tunadai nini kwasababu BAE hawakuvunja hazina, ilikuwaje pesa tulizokopa Baklays zikatoka tena na ziada bila kujua.
3.waziri wa mambo ya nje alikuwa JK je naye hakujua suala hilo? na inakuwaje serikali ya uingereza ndio ianze kuhoji uhalali.
4. serikali yetu imekana mara nyingi kuwa hakukuwa na uhalifu, sasa tunapata wapi nguvu ya kuuita uhalifu na kama kulikuwa na makosa je wahusika wamewajibika kisiasa na kisheria?
5.Membe alishawahi kusema PCCB inafanyia kazi pamoja na SFO, matokeo ya uchunguzi ni nini?
6.Nina akina nani walihusika kwa upande wa Tanzania na wamechukuliwa hatu gani?
7. Je pesa zilitoka kwa idhini ya mtu binafsi au makubaliano ndani ya baraza la mawaziri?
8.Ni nani amepanga matumizi ya pesa hizo na zipo katika fungu gani la serikali?
9. Kama hazitarudi ina maana hakuna mpango wa kujenga vyoo na kununua vitabu hadi tupate pesa hizo?
10 Kama kazi ya bunge ni kusimamia serikali wamesimami nini juu ya Kagoda, meremeta na Tangold
11. Kwanini serikali ikomalie pesa za BAE na iache Airtel ambazo ni mara tatu zaidi ya hizo?
12. Ni nani ametudhalilisha, walioshiriki wizi ambao ni viongozi wetu au BAE waliofanya dili?
13, 14 ............., 100

Nilichokiona na kusikia ni propaganda na waulizaji hawana ufahamu wa aina yoyote, kinyume na matarajio yangu kuwa wao kama watu wenye 'exposure' mtazamo wao ungekuwa mpana zaidi. Urban Pulse this is abysmal and too low. With all respect to your organization, Im saying shame on you!
 
Yaani hii mibunge minigine bana.............yaani inazungumza upuuzi wakifikiri watu woote ni wapuuzi kama wao...............damn.........
 
Nilimsikia kiongozi wa ujumbe wa wabunge waliokwenda Uingereza kutembeza bakuli la chenji ya rada (ungo) Naibu Spika Job Ndugai akidai kuwa Bunge litasimamia matumizi ya hizo hela zikirudishwa serikalini. QUOTE]

Naibu Speaker Ndungai ama anatudhihaki sisi watanzania na kutoana hatuna akili timamu au YEYE ni mtu wa kusema asichokiamini wala kujua.
Report ya mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali (CAG) inaonesha kupotea kwa hela za umma takribani 25% kwa mwaka mmoja wa fedha pekee. Hapa tunaongelea trillions na sio hivi vijibilioni vya Rada! Pili, hela za stimulus package (Tsh 1.7+ trillion) hazijulikani zili-stimulate kampuni gani au sekta ipi? hakuna maelezo? Huyu Naibu Speaker Ndungai hajasikika mahali popote akihoji upoteaji wa hizi hela!

Ndungi na hao wabunge walioenda London wanaweza kutueleza watanzani ni kwanini Bunge halikusimamia serikali ili kuzuia huu upeteaji wa ma-trillions wa shilingi za walipa kodi? Na hata baada ya report ya CAG kuwasilishwa Ndungai na bunge lake wamefanya nini ili walau waliofuja hela wasiendelee kufuja?

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi kuonesha dhamira ya kweli ya kusimamia serikali na ndio maana hata maazimio 18 ya yalitokana na kamati ya Dr. Mwakyembe yamegeuka hewa! Bunge limekuwa linazuisha mijadala na hata maswali yanayogusa maisha wa watanzania kujadiliwa bungeni kwa kisingizio cha kutoingilia uhuru wa mihimili mingine ya dola. Leo hii serikali inafanya inavyotaka, hela zinapotea kwa matrilioni kwa sababu wawakilishi wa wananchi waliopewa dhamana ya kusimamia serikali wameguka na kuwa taasisi ya serikali! Leo hii Speaker anakuwa msemaji wa serikali, naibu wake anaenda London kudai hela kwa niaba ya serikali, huku wabunge wakipitisha sheria za hovyo na za kinyonyaji zinazoruhusu misamaha ya kodi. Naibu Speaker Ndungai anasimamia nini?
 
Ahsante sana kwa clip.
Nimekuwa disappointed si kwa ujumbe wa Ndugai na majibu, bali kwa hao wanaoitwa waandishi wa habari na wote walioaanda mazunguzo haya.
Naomba kama kuna uwezekano yawepo mahojiano na KHL (mwanakijiji).
Nasema hivi kwasababu ni wazi kabisa hao waliouliza maswali hawajui undani wa suala lenyewe au wamekirimiwa. Insikitisha sana.
Niliangalia mahojiano ya Ndugai na BBC (Zuhura Yunus) yalivyokuwa bora kuliko haya.

Ndugai ameeleza kuanzia hukumu iliyotolewa kama anavyotuimbisha waziri Membe. Wasichosema ni chanzo cha wizi, yaani wanataka tuangalie tulipoangukia na si kujikwaa

Kwanza walitakiwa waulize hiyo kamati maalumu imeundwaje na kwa utaratibu gani tukizingatia Membe alifikisha jambo hili bungeni kwanza.
2.Wlitakiwa waulize tunadai nini kwasababu BAE hawakuvunja hazina, ilikuwaje pesa tulizokopa Baklays zikatoka tena na ziada bila kujua.
3.waziri wa mambo ya nje alikuwa JK je naye hakujua suala hilo? na inakuwaje serikali ya uingereza ndio ianze kuhoji uhalali.
4. serikali yetu imekana mara nyingi kuwa hakukuwa na uhalifu, sasa tunapata wapi nguvu ya kuuita uhalifu na kama kulikuwa na makosa je wahusika wamewajibika kisiasa na kisheria?
5.Membe alishawahi kusema PCCB inafanyia kazi pamoja na SFO, matokeo ya uchunguzi ni nini?
6.Nina akina nani walihusika kwa upande wa Tanzania na wamechukuliwa hatu gani?
7. Je pesa zilitoka kwa idhini ya mtu binafsi au makubaliano ndani ya baraza la mawaziri?
8.Ni nani amepanga matumizi ya pesa hizo na zipo katika fungu gani la serikali?
9. Kama hazitarudi ina maana hakuna mpango wa kujenga vyoo na kununua vitabu hadi tupate pesa hizo?
10 Kama kazi ya bunge ni kusimamia serikali wamesimami nini juu ya Kagoda, meremeta na Tangold
11. Kwanini serikali ikomalie pesa za BAE na iache Airtel ambazo ni mara tatu zaidi ya hizo?
12. Ni nani ametudhalilisha, walioshiriki wizi ambao ni viongozi wetu au BAE waliofanya dili?
13, 14 ............., 100

Nilichokiona na kusikia ni propaganda na waulizaji hawana ufahamu wa aina yoyote, kinyume na matarajio yangu kuwa wao kama watu wenye 'exposure' mtazamo wao ungekuwa mpana zaidi. Urban Pulse this is abysmal and too low. With all respect to your organization, Im saying shame on you!

Mkuu nakubaliana na wewe. Interview ilikuwa so poor and disorganized.
 
Waingereza siyo Mazezeta kama hawa Wabunge wanavyofikiri. Hawa Waingereza walishawahi kutawala nusu ya dunia yote wakati fulani na wanajua ushenzi na unafiki wa aina zote zilizopo. Hili zoezi wanalofanya hawa wanne ni kazi bure.

Halafu uwongo wenyewe wanaotumia, eti wanataka kujenga nyumba 1,000 za walimu, madawati laki 2 n.k. Hawa hawa waliokarabati nyumba ya Gavaa kwa Sh. Billion 2. Hawa hawa waliojenga Twin Towers kwa USD 500 Million!

Waachane na hiyo kitu waandike hasara tu.

kwanza hao BAE in practical wanatujua vizuri sana
kazi yao yenyewe kutengeneza zana za kijeshi niko na hakika walia nusa hela kuliwa
na jamaa walisha andaa midomo sasa wanashukwa na ute
 
Si TULINDE rasilmali zilizopo? Hili la BAE watu walishakula. Maamuzi magumu hakuna.+
 
Binafsi sina imani na serikali iliyopo madarakani kama hizi fedha zitatumika kwa manufaa ya watanzania wanyonge na masikini wa kutupwa,ninachojua ni kwa kwamba hizi fedha zitakuwa misused completely.Hii ni sawa na kesi ya tumbili apelekewa nyani akatoe uamuzi,wakati hawa ni jamii hileile,hivyo daima hawawezi kutosana!!
 
Watu wanakuheshimu - hata pasipo wewe kudai wakuheshimu - pale mtu unapojiheshimu. Na tuelewe kwamba katika culture zingine mla rushwa na yule anayetetea rushwa wanahesabiwa kama watu wasiojiheshimu na hivyo hawapewi heshima yoyote.
 
quote_icon.png
By Edson
Hansard 30 January 2007
Sale of Radar System (Tanzania) [30 Jan 2007]
30 Jan 2007 : I made the decision to cut back our promised a
id by £10 million and went to see
President Mkapa-a man I greatly respect and who did a good job by his country. He
told me that the contract had been signed
before he came to office, a deposit had been
paid and there was a penalty clause if Tanzania did not go ahead.

ina maana hii kitu ni dhambi ya mwinyi pia au hapo kwenye bold sijaelewa
namba ufafanuzi kabla sijapiga mishale kwa kukurupuka
mimi siku zote najua ili kitu katuletea chinga hapa naona kama napata nuru mpya vile
nani alikuwa jeshi na wamasiliano wakati huo wa mwinyi?

Mkuu kuna utatanishi kama makubaliono yalifanyika wakati wa utawala wa mwinyi au Mkapa. Kuna hii post nimeipost kwennye thread nyingine, nai paste hapa uisome.

Makubaliono kati ya SFO na BAE (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ems-yaliyoiweka-nje-serikali-ya-tanzania.html) yanaonyesha kuwa negotiations zilianza tokea mwaka 1992 kati ya serikali na Seamen Plessey Systems Ltd. Hiki kilikuwa kipindi cha awamu la pili ya utawala wa Mwinyi. Sijui ni nani aliyekuwa anaongoza wizara husika. Mkataba ulisainiwa Septemba 1997. Hiki kilikuwa kipindi cha utawala wa Mkapa. Sijui kama wizara husika bado ilikuwa chini waziri yule yule wa wakati wa majadiliano. Pamoja na kusaini mkataba haukuwa effective kutokana na kutoafikiana juu ya malipo. Mkataba huu ungeigharimu Tanzania dola za Kimarekani milioni 88. Kwa hiyo majadiliano yaliendelea.

Mwaka 1997 BAE Systems iliinunua Seamen Plessey Systems Ltd. Baada ya kununuliwa, mwaka 1998 Seamen Plessey Systems Ltd ilibadilisha jina na kuitwa British Aerospace Defense System Ltd. Mwishoni mwa mwaka 1999, mkataba mpya wa kuuza radar ulisainiwa kati ya serikali ya Tanzania kampuni ya British Aerospace Defense System Ltd ambao uligharimu dola za kimarekani milioni 39.97. Hizi gharama zilikuwa chini ya nusu ya gharamza za makubaliano ya awali (mwaka 1997). Sijui wizara husika ilikuwa chini ya nani.

Kwa hiyo, hapa kulikuwa na mikataba miwili. Mkataba uliosaniwa mwaka 1997 lakini hakuwa effective kwa vile majadiliano juu ya malipo bado yalikuwa yanaendelea, na mkatata uliosaniwa mwaka 1999. Documents hazionnyeshi kama mkataba wa kwanza ulikuwa ni mwendolezo wa majadiliano ya mkataba wa kwanza, au ulikuwa ni mkataba mpya uliotokana na majadiliano mapya kabisa.

Lakini la muhimu zaidi ni Hansard za Bunge la Uningereza za tarehe 30 Januari 2007 kuhusiana na mauzo ya radar Tanzania. Katika Hansard hizo, Clare Short (waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wakati huo) ambaye alikuwa anapinga vikali Tanzania kuuziwa radar, alisema alienda kumwona Mkapa, mtu anayemweshimu ana ambaye ameifanyia mengi Tanzania. Mkapa alimwambia kuwa mkataba wa kununua radar ulisainiwa kabla hajawa Rais, na kuwa deposit ilkuwa tayari imeshalipwa kitu ambacho Tanzania ingepigwa faini kama ingevunja mkataba. Lakini makubaliano kati ya SFO na BAE yanaoneysha kuwa mikataba yote miwili ilisaniwa wakati Mkapa akiwa madarakani. Ukiangalia hapo kuna contradiction kati ya Hansard za Bunge la Uingereza na makubaliano kati ya SFO and BAE.
 
Tatizo ni kuwa Mwinyi yupo na Mkapa yupo lakini hakuna aliyewahi kuulizwa ilikuwaje! Kikwete tena alikataa waziwazi (alipokuwa Uingereza) kutaka Mkapa ahojiwe kuhusu rada.
 
Mkuu kuna utatanishi kama makubaliono yalifanyika wakati wa utawala wa mwinyi au Mkapa. Kuna hii post nimeipost kwennye thread nyingine, nai paste hapa uisome.

Makubaliono kati ya SFO na BAE (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ems-yaliyoiweka-nje-serikali-ya-tanzania.html) yanaonyesha kuwa negotiations zilianza tokea mwaka 1992 kati ya serikali na Seamen Plessey Systems Ltd. Hiki kilikuwa kipindi cha awamu la pili ya utawala wa Mwinyi. Sijui ni nani aliyekuwa anaongoza wizara husika. Mkataba ulisainiwa Septemba 1997. Hiki kilikuwa kipindi cha utawala wa Mkapa. Sijui kama wizara husika bado ilikuwa chini waziri yule yule wa wakati wa majadiliano. Pamoja na kusaini mkataba haukuwa effective kutokana na kutoafikiana juu ya malipo. Mkataba huu ungeigharimu Tanzania dola za Kimarekani milioni 88. Kwa hiyo majadiliano yaliendelea.

Mwaka 1997 BAE Systems iliinunua Seamen Plessey Systems Ltd. Baada ya kununuliwa, mwaka 1998 Seamen Plessey Systems Ltd ilibadilisha jina na kuitwa British Aerospace Defense System Ltd. Mwishoni mwa mwaka 1999, mkataba mpya wa kuuza radar ulisainiwa kati ya serikali ya Tanzania kampuni ya British Aerospace Defense System Ltd ambao uligharimu dola za kimarekani milioni 39.97. Hizi gharama zilikuwa chini ya nusu ya gharamza za makubaliano ya awali (mwaka 1997). Sijui wizara husika ilikuwa chini ya nani.

Kwa hiyo, hapa kulikuwa na mikataba miwili. Mkataba uliosaniwa mwaka 1997 lakini hakuwa effective kwa vile majadiliano juu ya malipo bado yalikuwa yanaendelea, na mkatata uliosaniwa mwaka 1999. Documents hazionnyeshi kama mkataba wa kwanza ulikuwa ni mwendolezo wa majadiliano ya mkataba wa kwanza, au ulikuwa ni mkataba mpya uliotokana na majadiliano mapya kabisa.

Lakini la muhimu zaidi ni Hansard za Bunge la Uningereza za tarehe 30 Januari 2007 kuhusiana na mauzo ya radar Tanzania. Katika Hansard hizo, Clare Short (waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wakati huo) ambaye alikuwa anapinga vikali Tanzania kuuziwa radar, alisema alienda kumwo na Mkapa, mtu anayemweshimu ana ambaye ameifanyia mengi Tanzania. Mkapa alimwambia kuwa mkataba wa kununua radar ulisainiwa kabla hajawa Rais, na kuwa deposit ilkuwa tayari imeshalipwa kitu ambacho Tanzania ingepigwa faini kama ingevunja mkataba. Lakinimakubaliano kati ya SFO na BAE yanaoneysha kuwa mikataba yote miwili ilisaniwa wakati Mkapa akiwa madarakani. Ukiangalia hapo kuna contradiction kati ya Hansard za Bunge la Uingereza na makubaliano kati ya SFO and BAE.

mkuu nimekusoma mimi nakwenda na ya bunge la uingereza nina imani nao hiyo ya SFO na BAE ina mapungufu ya
taarifa maana kikwete alishagoma mkapa hasiojiwe

nadhani ndio maana anataka mwinyi mtoto hachukue nchi ili kimlinda baba yake mzee rukusa.

wakati wa kusaidi aliyekuwa waziri hawamu ya tatu ni MWANDOSYA na ni yeye katika ununuzi wa ndege pia
huyo jamaa ni tajiri kwa kula hii migao
 
mimi napendekeza hawa oxfam wapewe wanajua jinsi ya saidia wananchi na wanauzoefu wa muda mrefu nadhani ndio walengwa wa BAE

OXFAM yaipa changamoto LHRC

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeombwa kuandaa mtaala wa masomo ya kisheria utakaofundishwa kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu ili kuwasaidia wananchi kujua haki zao za msingi kuanzia wakiwa watoto wadogo.

Wito huo ulitolewa jana na wanasheria wanaotetea haki za binadamu kutoka shirika la misaada la Uingereza la OXFAM ambao wako nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya kisheria na haki za binadamu yanayofanywa na LHRC.
Akizungumza katika mkutano uliojumuisha wadau wa sheria ya haki za binadamu na waandishi wa habari, Miriam Gonzaler kutoka Oxfam alisema msaada wa kisheria unaotolewa na LHRC pekee hauwezi kutosheleza mahitaji kutokana na kuwepo kwa wananchi wengi wasio na uelewa wa kisheria.
"Tunaomba muandae mtaala wa masomo ya kisheria utakaofundishwa kuanzia katika shule za msingi hadi elimu ya juu, ili uweze kuwasaidia wananchi kufahamu kwa undani zaidi haki zao za msingi kwani LHRC pekee haitoshelezi," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Francis Kiwanga, aliueleza ujumbe huo kuwa wako katika utekelezaji wa mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu kuwa sheria, ambao utawasaidia watoe msaada kwa urahisi zaidi kwa watu wasiojua sheria.

CHANZO: NIPASHE
 
Serikali imeumbuliwa bungeni ikidaiwa kuwasilisha taarifa za uongo kupitia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ugawaji wa madawati yaliyonunuliwa kwa ‘chenji ya rada'. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alitoa tuhuma hizo jana, wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema Serikali imewadanganya wabunge kwa kuwa hakuna kitu kilichofanyika.

Alisema katika majibu ya Serikali kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa kuwa imetangaza kununua madawati 93,740 na kuyagawa katika halmashauri mbalimbali nchini wakati siyo kweli. Alisema kwa mtindo huo, Serikali imelidanganya Bunge pamoja na Watanzania kwa kuwa imetangaza madawati hewa ambayo hayapo.

"Wabunge kama kweli mnatimiza majukumu yenu na hampo hapa kwa masilahi yenu tu, hebu hojini halmashauri zetu zimepelekewa haya madawati 93,000 yanayozungumzwa humu au mnapiga makofi tu? Serikali inadanganya tunatakiwa tuihoji tuiwajibishe," alisema.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa mfano wa mgawo huo kwenye Halmashauri ya Ikungi, Singida kwamba ilitangazwa kupelekewa madawati 508 lakini amekwenda jimboni na hakukuta dawati hata moja. Alisema uchunguzi wake umebaini kuwa hata katika wilaya mbalimbali ikiwamo ya Iringa, hakuna kitu kama hicho.

"Jana sikuwa hapa bungeni nilikwenda kwenye halmashauri yangu, hakuna dawati hata moja. Hata Halmashauri ya Iringa kwa Mchungaji Msigwa (Peter) hapa ananiambia hakuna dawati hata moja, mnatudanganya ili iweje?" Aliwashauri wabunge wengine kufanya utafiti katika maeneo yao iwapo kuna madawati ambayo yamepelekwa kutokana na fedha zilizorejeshwa na Serikali kama chenji ya rada.

Lissu alisema ni maneno matupu ambayo yamekuwa yakiwahadaa wabunge na kuwafanya wasahau wajibu wao wa kuisimamia Serikali na kujikuta ni washangiliaji wakati wote. Lissu alisema kinyume na taarifa hizo za Waziri Mkuu, Bunge jana lilikuwa limeelezwa na Naibu Waziri (hakumtaja) kuwa madawati hayo hayajagawanywa.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa akijibu swali la nyongeza la Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe - CUF), kuhusu madawati hayo, alisema kwa kuwa madawati hayo bado yanagawanywa, watakaa na kuangalia utaratibu mzuri wa kuyafikisha Zanzibar.

Majaliwa

Hata hivyo, Majaliwa akizungumza na gazeti hili jana jioni alisema inawezekana Lissu hakumwelewa au amefanya makusudi kupotosha kile ambacho yeye alikizungumza ili kujipatia sifa kwa umma.

"Nilichokisema hakitofautiani na kile kilichomo kwenye jedwali la hotuba ya Waziri Mkuu, nimesema kwamba hadi sasa tunaendelea kugawa madawati ya plastiki katika halmashauri za wilaya 41 na hivi ninavyozungumza halmashauri ya mwisho inayopelekewa madawati leo (jana) ni Temeke," alisema Majaliwa na kuongeza:

"Kwa upande wa madawati ya mbao, ambayo yeye (Lissu) ameyaita ya chuma, nayo yanaanza kusambazwa katika halmashauri zilizobaki 123, na kazi hiyo itaendelea na ifikapo Agosti 15 mwaka huu kila halmashauri itakuwa imepata mgawo wake."

Alisema tayari Serikali imetangaza zabuni ya utengenezaji wa madawati awamu ya pili ambayo itafunguliwa Jumatatu ijayo na kwamba baada ya taratibu kukamilika utengenezaji huo utaanza na kukamilika katika muda wa miezi miwili. Alisema katika awamu ya kwanza, kila halmashauri inatarajiwa kupata madawati 756, sawa na madawati 123, 984.

"Kama unakumbuka awali tulipanga madawati haya yapelekwe kwenye wilaya kama sita nadhani, lakini wabunge walishauri kwamba kila wilaya inufaike na ndicho tulichokifanya," alisema.
 
Back
Top Bottom