Amazon kuzindua mshindani wa Starlink mwaka 2024

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,527
2,299
Project Kuiper ya Amazon ambayo itatoa huduma ya mtandao kwa kupitia satelite inatarajiwa kuanza kazi 2024. Huduma hiyo itakuwa na spidi zifuatazo.
Standard 400Mbps
Ultra-compact (Dish ndogo) 100 Mbps
Pro hadi 1Gbps.

Bei zitatangazwa huku mbele ila zinategemewa kuwa shindani na Starlink.

Jeff Bezos mwanzilishi wa Amazon tukumbuke naye ana kampuni ya rocket Blue Origin ila hizi satelite zitarushwa na kampuni mbalimbali za rocket.

CNBC

20230314_204313.jpg
20230314_204303.jpg
20230314_204231.jpg
20230314_204235.jpg
20230314_204239.jpg
 
Bora mkuu usubirie mchina, maana hata Hio Starlink tunaongea sababu haipo, ikishakuja Tutaanza kulaumu tena ni Gharama, inakata kata, na matatizo kibao.
Umesema kweli wengi hatutaweza afford gharama za Starlink huu ni ukweli hasa gharama za installation yake tu ni mtiti kwa mtanzania wa kawaida, kuhusu kukata kata nimeona sehemu mbali mbali wamarekani baadhi wanayoitumia wanalalamika inasumbua hasa kukiwa na mawingu na sehemu yenye miti mirefu na pia ina athiriwa na roaming..
 
Ping yake ni level za 3G, na pia haimaintain muda wote, gamers wengi wanalalamika disconnection kwenye servers.

Sema ni Nzuri kwa wale ambao hawana matumizi ya ping, wanaoshusha mizigo torrent, kudownload games, movies na mambo mengine.
 
mkuu nilikua nacheki youtube wanaijeria wanalipa 43$ per month, mi naona ni far better kuliko 120K ya vodacom kwa speed ya 30mbps, kati starlink wao inarange kwenye 150+mbps.
 
Mbunge wa mtama atapinga hii.. In short telecome zinatakiwa zibadilike la sivyo cha moto watakiona. Hizi kampuni zinatakiwa zianze kuleta internet nyumbani kwa cable la sivyo watakosa soko sana kama kwako kuna internet data utakuwa unatumia kidogo ukiwa haupo home
 
mkuu nilikua nacheki youtube wanaijeria wanalipa 43$ per month, mi naona ni far better kuliko 120K ya vodacom kwa speed ya 30mbps, kati starlink wao inarange kwenye 150+mbps.
Hii ni Hela aliotangaza Musk ila wanalipa zaidi Nigeria.

Tu Assume unalipa $40 kwa mwezi, installation fee pekee ni zaidi ya Milioni 1 wangapi wanaweza Ku Afford?

Pia kama nilivyosema juu Satelite internet ina matatizo ya Ping, watu washazoea internet za Mitandao ya simu, hii ina Disconection za mara kwa mara. Kama unaangalia youtube, Netflix, kudownload ama kufanya kitu ambacho sio live huwezi ona tofauti, ila kama unafanya video call, kuangalia mpira, kucheza games na vitu vingine vya live hizi Disconection zitakuhusu.

Pia issue ya Mvua na Upload speed bila hata Mvua speed inakua chini.

Kwa matumizi mazuri ya Nyumbani 30mbps yenye ping ya 1ms ama 2ms ni bora kuliko 150mbps yenye 40ms na Disconection.

Huyu jamaa kaelezea Vizuri hapa
 
Mkuu samahani,nje ya mada kidogo.Hivi hapa JF kama natumia browser kwenye simu nafanyaje ili niweze ku-upload picha au video nyingi kwa wakati mmoja bila ya ku-upload moja moja?
Unaclick attach kisha unabrowse hadi kwenye picha unazotaka ku upload halafu unagusa bila kuachilia mpaka picha iwe highlighted kisha unachagua picha zote na ku upload kwa pamoja. Zita upload na kukaa chini ya post, pale chini click instert utachagua iwe full picture ama thumbnail
 
Shukrani mkuu!
 
Mkuu nikigusa sehemu ya attach files inanigomea na kuniletea ujumbe ufuatao
487648.jpg
 
Attachments

  • 487648.jpg
    487648.jpg
    61.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom