Adhabu ya fimbo kwanini wazungu walifanikiwa bila Bakora wakati sisi bila Bakora kuna baadhi ya mambo kwa mtoto hayaendi?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,718
15,696
Binafsi sijawahi kufika Ulaya ila nawafuatilia tu kwenye habari. Hawa jamaa watoto wao kuchapwa fimbo ili wakae kwenye mstari sio kipaumbele kabisa.

LAKINI
Wanafanya uvumbuzi, wanaongoza dunia, kwa ufupi wanategemea duniani. Yaani Ukiacha Mungu anayefuatia ni mzungu/US japo wote tunaakili sawa.

NJOO BONGO SASA
Mfano mzuri mimi, najijua kabisa bila juhudi kali za kuchapwa fimbo na adhabu za hapa na pale kwa walimu wa Shule ya msingi na mzazi (mother) nisingevuka hata darasa la saba.

Je? Kunatofauti kati ya mtoto wa kiafrika na mzungu katika vigezo vya kulelewa? Mbona wenzetu bila fimbo wanaenda tu ila sisi bila fimbo unaweza kukuta mtoto kajisaidia kwenye sufuria la ubwabwa makusudi.

Unakumbuka siku uliyochapwa fimbo na Mwalimu au mzazi au mlezi au jirani. unadhani hiyo fimbo ilikuwa na tofauti yoyote katika kubadilika kwako kulinganisha kama usingechwa kabisa na kushauriwa tu.
 
Una uhakika wazungu hawatumii fimbo?
Wazungu walianza kuwafundisha watoto wao na kuwaadhibu wanapopotoka kwa kutumia fimbo yaani kuwachapa viboko. Angalia methali hii ili kuligundua hilo: "Spare the rod and spoil the child". Lakini kwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda, wakaja wale wanaolinda haki za watoto na kuharamisha adhabu za viboko. Hivyo basi watoto hawachapwi tena viboko. Ila sasa vitendo vingine wavifanyavyo kwa kuitumia hii haki vinatia wasiwasi. Wanayo haki ya kujiunga na makundi mbalimbali ambayo kwetu sisi Waafrika yanatia ukakasi. Hivi mwanao akikuambia yeye ni gay utamfanyaje. Kumpiga huwezi na kumfukuza nyumbani huwezi kwa kuchelea kuvunja haki za huyo mtoto.
 
Acha kudanganywa na media nchi nyingi za ulaya wanaruhusu corporal punishment hata baadhi ya states marekani
 
Mkuu ungelikuwa unafanya utafiti kabla ya kutandaza thread!

Historia ya mboko uJerumani unaiondoaje?

Embu fanya utafiti kidogo, nchi gani ulaya inayoongoza kuadhibu watoto kwa viboko.

Unaambiwa kuanzia kwao, mboko kwa mtoto ni chai kama zilivyo chai za vifungua vinywa ndiyo maana wana akili.

Hiyo ya kupenda kwao mboko ilipelekea wakaiweka hadi kwenye sheria ya adhabu kwa watu wazima.

Mtukutu ama mhalifu akilambwa mboko za maana lazima akili zimsogee.

Mboko zinaleta heshima popote, iwe kwa mtoto hata mtu mzima pia, maana akikumbuka jinsi zinavyowasha lazima atie uoga hata kama ni jeuri.
 
mkuu mimi naamini katika Bakora, Na sijui kwa nini ziliingizwa kwenye siasa eti wanafunzi wasichapwe hadi vigezo flani na watu wasign wakati badala ya Kuweka sheria kwa atakayemuumiza mtoto kwa kuchapa extreme.

Nimekili kwenye uzi kuwa mimi ulaya sio mwenyeji kwa hiyo nakushukuru kwa maelezo mazuri.
 
Ushoga umehalalishwa kwa wazungu kisheria? Kama ndio / hapana, unajua kwa nini?! NB: Nimesoma heading tu.

Main reason ni institution ya marriage imefail. Mtoto analelews na mzazi wa jinsia moja unategemea nini? Hata sisi ndio tunapoelekea huko watu wanajisifu kabisa wanapea mimba wanasepa au kuwatukana single mothers ila 20 years from now tutaona janga na hili janga litamgusa karibia kila mtu wacha watu waendelee kuchekelea ujinga. Mavuno yanakuja
 
Wazungu wamefanikiwa kwa lipi! Labda kiuchumi, maadili ni sifuri na nyie mnaoiga uzungu mnaipata fuleshiii.
 
Mkuu ungelikuwa unafanya utafiti kabla ya kutandaza thread!

Historia ya mboko uJerumani unaiondoaje?

Embu fanya utafiti kidogo, nchi gani ulaya inayoongoza kuadhibu watoto kwa viboko.

Unaambiwa kuanzia kwao, mboko kwa mtoto ni chai kama zilivyo chai za vifungua vinywa ndiyo maana wana akili.

Hiyo ya kupenda kwao mboko ilipelekea wakaiweka hadi kwenye sheria ya adhabu kwa watu wazima.

Mtukutu ama mhalifu akilambwa mboko za maana lazima akili zimsogee.

Mboko zinaleta heshima popote, iwe kwa mtoto hata mtu mzima pia, maana akikumbuka jinsi zinavyowasha lazima atie uoga hata kama ni jeuri.

Viboko vimekuwa kama general solution kwa watoto ambao wapo tofauti.

kuna mtoto bila kujengewa hofu za viboko hafanyi chochote na kuna mtoto anaweza kisikiliza bila hata ya kuchapwa

ubaya wa viboko kwa mtoto wa kundi la pili vinamfanya akose kujiamini na awe mtu aliyejawa hofu kiasi cha kushindwa hata kujielezea mbele za watu...

viboko viwepo kama moja ya solution ila sio main solution. watoto wapo tofauti kwa nini tutumie kitu kimoja kama sala kila mara
 
Wazungu wamefanikiwa kwa lipi! Labda kiuchumi, maadili ni sifuri na nyie mnaoiga uzungu mnaipata fuleshiii.
Siyo kila taifa la wazungu limefeli kimaadili, fanya utafiti tena.

Pia tofautisha kati ya maadili na utamaduni ili twende sambamba.
 
Siyo kila taifa la wazungu limefeli kimaadili, fanya utafiti tena.

Pia tofautisha kati ya maadili na utamaduni ili twende sambamba.

Hapo hapo kwenye utamaduni, ikishakuwa ni utamaduni basi ni vizuri kutambua na kuheshimu tofauti zetu... wazungu kivyao na sisi kivyetu.
 
Back
Top Bottom