Adebayor amtuhumu mama yake kuwa anamroga

Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.

Adebayo aliwahi kuchezea Arsenal
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.
Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.
BBC

Hii ni aibu kwa Adebayor mwenyewe.
 
Jamani,kumhusisha mama yake na uchawi ni jambo zito!!!Labda kuna "mambo yao".ye amejuaje kuwa mama yake mchawi kama na yeye si mchawi?!
 
Kumbe yule jamaa ni mpuuzi hivi! Ngoja akacheze mpira Malaysia sasa kwa ujinga wake.
 
Sisi waafrika ndo zetu hufanyi kitu hadi ndumba zihusike.Kama hao wa mbele hivyo hapa kwetu itakuwaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom