WAWATIBU MALARIA KWA DAWA YA USINGIZI.
Mgonjwa wetu wa tanga, twamlilia nyikani.
Na nduguye ni majanga, ni yule wa visiwani.
Madokta wamewapanga, wawili wote wodini.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Hapa pana siri kali, kuwatibu watu hawa.
Mara dozi ziwe mbili, wakasema wenye...
MWANAMKE ZAKE SIFA.
Kipindi wamtokea, ulimsifia kwanza.
Ndipo kakukubalia, leo ndio wake mwenza.
Upendo unafifia, kusifu ukipunguza.
Mwanamke yake sifa, usiache kusifia.
Sio mali kutumia, eti utamtuliza.
Nyumbani ukiingia, kama bubu wanyamaza.
Mkeo anaumia, au mume namkwaza?
Mwanamke zake...
TUNDA LA AJABU.
Nimetulia mtini, nala tunda liso kokwa.
Laini shinda maini, ladha kuku wa kupakwa.
Chumvi nitake ya nini, nala bivu si kidakwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.
Tunda sikukuta chini, liangani likadakwa.
Ladha yake ulimini, akili zangu zarukwa.
Ladha zazidi...
NATAKA KUOA:
Naogopa majaribu, kuoa nimenuia.
Kwa kukwepa maswahibu, yaliopo kwenye ndoa.
Nimepanga taratibu, sifa za anae faa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.
Namtafuta bubu, awe na kiziwi pia.
Huyu huwa hana gubu, hatosikiza umbea.
Nitaziepuka tabu, tutadumu kwenye ndoa.
Natafuta wa...
TWABORONGA KISWAHILI.
Twajua neno ONESHA, kwa chenye kuonekana.
ONESHA kuwa ONYESHA, hapa ni lugha gongana.
ONYESHA kunyumbulisha, ONYA, ONYO, ONYEANA.
Twajiita waswahili, kiswahili twaboronga.
TWASIKIA kwa SIKIO, lugha yenye burudani.
SIKIO kuwa SHIKIO, tunalishikisha nini?
SHIKIO kwa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.