Recent content by Zanzibar-ASP

  1. Zanzibar-ASP

    Kwahiyo hapa RC Chalamila alihalalisha watu kuua tena, aagiza Polisi wafanye hilo waziwazi

    Chalamila amekosea kwa 100%. Hakuna mtu aliyepewa mamlaka ya kuua mtuhumiwa. Hata polisi hawana hayo mamlaka. Suala la kujilinda dhidi ya adui anayetaka kukudhuru lina sheria yake, na sheria hiyo haimpi mamlaka mtu kumuua mtuhumiwa.
  2. Zanzibar-ASP

    Kwanini mpaka sasa RC wa Dar (Chalamila) hajatumbuliwa na kuwekwa ndani?

    Kupitia video inayotembea mitandaoni, mkuu wa mkoa wa Dar, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Albert Chalamila amesikika akitoa kauli hizi tatu kwa ujasiri mkubwa; 1. Amekiri, kujitamba, kujivunia na kujipongeza kwa kuua? mtuhumiwa wa wizi aliyeingia nyumbani kwake mkoani...
  3. Zanzibar-ASP

    Kwahiyo hapa RC Chalamila alihalalisha watu kuua tena, aagiza Polisi wafanye hilo waziwazi

    Hapana, hiyo haijakaa sawa. Ni hatari na makosa makubwa kuua mtuhumiwa. Kwa hili huyo RC hastahili kuendelea kuwa mkuu wa mkoa.
  4. Zanzibar-ASP

    Kafulila: Tunatekeleza agizo la Waziri Mchengerwa ndani ya muda mfupi ujao DART itasaini mkataba na Mbia nia ni kupunguza gharama Kwa wananchi

    Kule Simiyu Kafulila alifanya nini na pesa za wakulima wa Pamba? Hivi wewe bado una imani na tumbili mwenye njaa kwenye shamba la bibi la mahindi?
  5. Zanzibar-ASP

    Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

    Umeshawahi kuishi Tanga? Mimi nimekwambia kitu ambacho ninakifahamu. Viwanda na mashamba ya mkonge yalikuwa mkoa Tanga lakini sio tanga mjini! Viwanda vya kuchakata mkonge vilijengwa ndani ya mashamba ya mkonge na kisha ulisafirishwa na treni kutoka shambani kupelekwa popote. Na makazi makubwa...
  6. Zanzibar-ASP

    Namna mbegu ya Umasikini inavyopandwa na kumea kwenye Familia/Koo

    Usije kujidanganya kuwa na Elimu bora au kuwa na kazi kunaweza kukufanya ukaondokana na umaskini. Nenda chunguza na utagundua kuna utitiri wa wasomi na wafanyakazi ni maskini wa kutupwa. Umaskini ni mtazamo wa kifikra kwa 100% na sio kutokuwa na akili au kukosa pesa, ajira au elimu ya darasani...
  7. Zanzibar-ASP

    Namna mbegu ya Umasikini inavyopandwa na kumea kwenye Familia/Koo

    Wacha kuzunguka mbuyu, Umaskini kwenye familia/ukoo umejikita kwenye haya mambo matano tu. 1. Utegemezi 2. Uvivu 3. Anasa 4. Malezi 5. Ushirikina. Chunguza, utakuja uniambie.
  8. Zanzibar-ASP

    Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

    Kulikuwa kuna kadingi fulani bungeni, sijui kabunge kaCCM kule Nkasi, kalikuwa kanalipukaga balaa wazenji tukianza kufungua midomo bungeni kuhusu huu muungano. Kale kadingi kangekuwepo leo hapo bungeni pasingekalika.
  9. Zanzibar-ASP

    Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

    Huyo mbunge naye kiazi kabisa. Yaani anasema viongozi wa Tanzania wanaotokea Zanzibar wanabaguliwa, halafu hapo hapo anaambiwa yeye ajitambulishe kama mtanzania ili asibaguliwe anakataa kata kata, anang'ang'ania tu kuwa yeye ni Mzanzibar na sio mtanzania!!
  10. Zanzibar-ASP

    Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

    Kiufupi tu wewe fahamu, hakuna kitu kinaitwa jiji la Dar, ni mazoea tu kuita hivyo. Kiofisi na kisheria kwa Dar jiji ni Ilala. Mkoa hauwezi kuwa jiji bali manispaa ndani ya mkoa ndio inayoweza kupandishwa hadhi na kuwa jiji. Hivyo Kinondoni inaweza kupandishwa hadhi na kuwa jiji.
  11. Zanzibar-ASP

    Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

    Naona hapo umechanganya. Halmashauri (wilaya) ya Tanga mjini (sio mkoa wa Tanga wote) imekuwa jiji miaka ya katikati, sio miaka ya 1970. Zao la mkonge halilimwi Tanga mjini bali katika wilaya zingine za mkoa wa Tanga. Umaarufu wa kipesa wa Tanga mjini uliletwa na Bandari na viwanda vikubwa.
  12. Zanzibar-ASP

    Tuboreshe kisiwa cha Mafia kama mbadala wa Zanzibar

    Naona safari hii watanganyika mmedhamiria kweli kweli kutemana na muungano!!
  13. Zanzibar-ASP

    Bunge la bajeti 2024 limesusiwa na kudorora balaa!

    Sijui kama Watanzania wengi wanajua kuwepo kwa vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea Dodoma. Yaani kuanzia mitaani, mitandaoni, redioni, Kwenye Luninga na magazeti hakuna habari wala mijadala mizito inayoibuliwa kutokea bungeni, yaani kumepoa balaa. Mahudhurio ya wabunge ni hafifu mno...
  14. Zanzibar-ASP

    Wanaume tuwe makini na sehemu tunazotaka kuoa

    Hiyo lafidhi na hizo swaga zipo kwa wanawake wa kichaga na kimeru. Yaani ukute ndio ana kazi kaajiriwa, kasoma kiasi na tayari umemuoa na kuzaa naye, basi ngoma inakuwa hivyo.
Back
Top Bottom