Mifumo ya kidunia ilishaamua mwanaume aishi kwa kukandamizwa na kufanyiwa ulaghai/ udanganyifu

Madhara yake ni watu kuwafanyia umafia wenza waliokosana nao na kuwapeleka akhera
Na aliefanyiwa umafia akipona nae anamtafuta wa kumpiga na kitu kizito na uyo victim mpya nae anatafuta victim wake na cycle inaendelea. Ndio maana pale mwishoni nikasema ukiamua kujitoa/kusaidia basi fanya ivyo kwa kiwango ambacho unaweza kustahimili maumivu ya kukipoteza
 
Yap, hawataki tena hilo jukumu. Kwanini? Sababu yeye akibeba mimba miezi 9 wewe uliyempa mimba unafanya nn? Anakuzalia, anakulelea, and then? What do you do? Hilo swali hata sasa hivi mwanamke kabla ya kushika mimba akimuuliza kijana asiyejielewa kwanini abebe mimba yake na katika hiyo miezi 9 ni nini atakuwa anafanya kwa mama ili iwe win-win uwezekano ni jibu litakuwa la hovyo.

Sasa hivi kuna wanawake wanalipwa kubeba mimba za watu wengine. Unataka mtoto? Unanunua yai, zinachukuliwa mbegu zako na yai la mwanamke linatungishwa kwa mwanamke mwingine na unamlipa. Ndo tulipofikia hapo.
Mkuu ninachokukubali huwa siyo mnafiki unaandika uhalisia bila kuwa biased haya mawazo yako angeandika mwanamke angeonekana ameandika tu ili kutetea wanawake wenzake, kumekuwa na kasumba ya wanaume kutaka kuteteana na kuungana mkono kwenye jambo lolote linalokandamiza mwanamke hata kama ni uongo na ujinga, yani mtu ukitetea wanawake kidogo tu utaitwa majina yote ya ajabu bila kuangalia kama hoja uliyoisema ni ukweli au la
 
Unapenda sana kujenga hoja kwa kufanya rejea kutoka uko magharibi. Mkuu jamii zetu ni tofauti kiuchumi, kimaadili na kielemu sio kila sera ya uko magharibi ita-fit hapa kwetu.
Hata haya yanayoendelea kwenye jamii zetu sasa hivi nayo wazee wetu walisema hivyo hivyo kwamba ni ya magharibi na hayatafika kwetu lakini leo hii yako wapi
 
Mimi naona dunia imemsikiliza mwanaume kwa muda mrefu imefika pahala acha sasa imsikilize na mwanamke kwa sababu mfumo dume umemkandamiza mwanamke vya kutosha, wake walipokuwa wanavumilia kukandamizwa miaka yote hiyo ilionekana sawa sasa wameamka baada ya kuchoka na kukataa kukandamizwa wanaume mnaanza kulalamika na mnaona kama mnaonewa, wanawake wamechoka kulalamika wameamua kujibu mapigo kwahiyo tulieni tu dawa iwaingie mpaka pale siku mtakapoongea nao lugha moja
Hii ni agenda ya wanawake au wanaume walioamua kuwainua wanawake ?
 
Mtawala anaweza kuwa kiongozi at the same time, lakini kiongozi ni ngumu kuwa mtawala. Kwa mantiki hyo bac mtawala wa siasa ya familia anaweza kuwa kiongozi vilevile wa familia hyo ..
Mkuu, familia inahitaji kiongozi kuliko mtawala.

Kiongozi anawapenda anaowaongoza, yupo pale kuwahudumia na anawasikiliza na kuzifahamu hisia zao. Maamuzi yake ya mwisho yanazingatia ushauri wa anaowaongoza.

Tofauti na Mtawala yeye ni top na haitaji mjadala, sauti yake haiojiwi hata kama kilichotoka ni ugoro, ni mshauri wa yeye mwenyewe.

Watawala katika familia ni sehemu ya chanzo cha kuibuka wapigania haki za wanawake.

Kiongozi na nyumba ndogo ni tabu sababu muda wote analazimika kuwa karibu na mke wake, mambo ni mengi ya kutatua, miradi ya maendeleo, shule watoto, marejesho. Kila siku kuna jambo la kujadili na mke.

Mtawala na nyumba ndogo ni rahisi sana sababu yeye anatoa maelekezo anaondoka na ole wake mtu asiyafate. Anapoenda hakuna wa kumhoji anafanya nini na atarudi lini.

Huo ni mfano mmoja tu wa utofauti wao
 
Hata haya yanayoendelea kwenye jamii zetu sasa hivi nayo wazee wetu walisema hivyo hivyo kwamba ni ya magharibi na hayatafika kwetu lakini leo hii yako wapi
Tunachoongelea ni usahihi wake sio mazoea ya kusema kama yametoka uko lazima yawe implemented na hapa. Najua threads mbili tatu haziwezi kuleta mabadiliko ya jumla lakini kuna wawili watatu wataamka. Uko magharibi ambapo sera ya 50/50 imetoka wapenzi wakitoka out ni jukumu la kila mmoja kulipa bill nusu kwa nusu je hii 50/50 itafanya kazi tukiileta bongo ambapo wadada washaaminishwa monetary expenses zote ni sharti ziwe sponsered na mwanaume ? Uko magharibi sio ajabu kukuta mke ajui kupika na mume ndio anaingia jikoni je 50/50 itqfanya kazi hapa bongo ambapo wanaume tumeanishwa mambo ya jikoni ni ya wanawake.. tusiangalie tu kwa sababu inqfanyika magharibi basi ni sharti iletewe hapa tuangalie pia usahihi wa kimazingira je inawezekana ikawa implemented hapa?
 
Mkuu, familia inahitaji kiongozi kuliko mtawala.

Kiongozi anawapenda anaowaongoza, yupo pale kuwahudumia na anawasikiliza na kuzifahamu hisia zao. Maamuzi yake ya mwisho yanazingatia ushauri wa anaowaongoza.

Tofauti na Mtawala yeye ni top na haitaji mjadala, sauti yake haiojiwi hata kama kilichotoka ni ugoro, ni mshauri wa yeye mwenyewe.

Watawala katika familia ni sehemu ya chanzo cha kuibuka wapigania haki za wanawake.

Kiongozi na nyumba ndogo ni tabu sababu muda wote analazimika kuwa karibu na mke wake, mambo ni mengi ya kutatua, miradi ya maendeleo, shule watoto, marejesho. Kila siku kuna jambo la kujadili na mke.

Mtawala na nyumba ndogo ni rahisi sana sababu yeye anatoa maelekezo anaondoka na ole wake mtu asiyafate. Anapoenda hakuna wa kumhoji anafanya nini na atarudi lini.

Huo ni mfano mmoja tu wa utofauti wao
halafu aliesambaza uvumi kuwa mtawala huwa hashauriwi na hapokei maoni na hapendi watu wake ni nani?
 
Mkuu ninachokukubali huwa siyo mnafiki unaandika uhalisia bila kuwa biased haya mawazo yako angeandika mwanamke angeonekana ameandika tu ili kutetea wanawake wenzake, kumekuwa na kasumba ya wanaume kutaka kuteteana na kuungana mkono kwenye jambo lolote linalokandamiza mwanamke hata kama ni uongo na ujinga, yani mtu ukitetea wanawake kidogo tu utaitwa majina yote ya ajabu bila kuangalia kama hoja uliyoisema ni ukweli au la
Mkuu, haya matatizo yote ya kimfumo yamesababishwa na mwanaume sio mwanamke. Kuibuka kwa mwanamke ni matokeo tu.
 
halafu aliesambaza uvumi kuwa mtawala huwa hashauriwi na hapokei maoni ni nani?
Sio uvumi ni uhalisia. Kutawala sio kuongoza. Hata wewe hapo, ukishajiona wewe ndo kila kitu, mungu mtu, mwenye maamuzi ya mwisho yasiyojali ushauri wa unaodhani wapo chini yako, upo sahihi wakati wote na unaogopwa hata kutaniwa haiwezekani. Ujue wewe ni mtawala na mwisho wako ni anguko litakalowafanya unaowatawala wapige vigelegele.

Baba unakufa familia nzima inashusha pumzi. Angalau sasa tutapumua, mama nae ataendesha lile gari lake maana mzee alikuwa mkali kama shubiri.
 
Tofauti ya mtawala na kiongozi ni pamoja na mamlaka lakin wote wanashauriwa. Mtawala anashauriwa ingawaje ukishindwa kumshawishi halazimiki kufuata ushauri wako. Angalia wafalme wote hata za wababe walioogopwa na dunia zilikuw na mabaraza ya washauri . Mpk hapa tukubaliane kwanza mtawala pia anashauriwa.
 
Hii sera ya 50/50 hakika ni mbaya sana hasa kwa huu ukanda wa Africa. Imezalisha single mothers wengi sana ambao hupelekea watoto kuwa na maadili mabovu sana na ndio maana vijana wengi huangukia kwenye umalaya na ushoga.

Malezi ya mwanaume kwa mtoto ni ya mwanaume tu ndugu zangu hili wanawake inabidi walitambue.
 
Mtoa mada umesahau kutambua kwamba kila mwanaume anatakiwa aitengeneza Dunia yake mwenyewe na kuiishi......owa mwanamke type yako" utakayeweza kumkontroo kimwili, kiroho na kiuchumi
Haya mambo ya 50/50 yapo humu mitandaoni,...90% ya wanawake duniani hawana taarifa nayo ... ni wewe vile unavyoweza kuchagua na kum-shape to fit in ...in your life (if you have that life)

Nb. Tikisa kichwa kwa nguvu kidogo utanielewa.
 
Ukizaliwa mwanaume we ujue Kila kitu kwako itakuwa ni tabu...

Huu wimbo ulimaliza Kila kitu.
Sio kweli napingana nayo hizi tabu sijawahi ziona maisha yangu yote na ni mume wa mtu mwenye watoto.

Mimi naona kuvuja damu kila mwezi ndio tabu zenyewe, huli hadi unyanduliwe hizi ndio tabu zenyewe, hupewi mchongo bila kuvuliwa chupi hizi ndio tabu zenyewe.

Kifupi alie waambia wanaume tunapata tabu anawadanganya.

Mwanaume kupata tabu au kutopata tabu ni machaguo yake.

Ila kuvuja damu kila mwezi uwe unapenda au hupendi utavuja tu.
 
Tofauti ya mtawala na kiongozi ni pamoja na mamlaka lakin wote wanashauriwa. Mtawala anashauriwa ingawaje ukishindwa kumshawishi halazimiki kufuata ushauri wako. Angalia wafalme wote hata za wababe walioogopwa na dunia zilikuw na mabaraza ya washauri . Mpk hapa tukubaliane kwanza mtawala pia anashauriwa.
Ukishaogopwa huwezi kuwa na washauri. Kinachotokea ni unazungukwa na watu wanaojua unataka kusikia nini na wanasema.

Mara nyingi watawala wanaoogopwa lazima wana kundi nyuma yake wasiomugopa wanaomlinda, hawa huwa hana mamlaka kwao, ila wana objective zinazofanana zenye mlengo wa kutawala. Hawa tu ndo wanaweza kushauriana ila watashauriana kutimiza objective zao za kiutawala.

Wengine wote hawashauri, wanajua mtawala anachotaka kusikia na wanakisema kama ushauri.
 
Tulikosea sana kuipokea hii sera ya 50/50 mbaya zaidi jukumu la kuieneza tukawaachia mafeminia vilaza wa type ya joyce kiria.
Na siku hizi jamii haina habari na boy child

Hawa mafeminia wameharibu dunia
Hii sera tulikosea sana wa Africa, lkn ukweli ni kwamba hii sera imelenga kulinda malengo ya wazungu wakiamini ya kwamba wanawake wakiwa kwenye madaraka kwa udhaifu wao wa kijinsia hawata weza kutaa matakwa yao wazungu.
Refer thread iliyo kuja hapa kuwa Africa inatakiwa iendelee kuwa provider wa raw material forever.
Yaani Africa kuna makosa kibao tumeyafanya kwa kupkea sera za wa Zungu, mfano democracy wanayo imba ni kutaka kuweka watu wao watako kuwa week, na isinge kuwa wanataka tuendelee kuzalisha raw materials nadhani wangeweza hata kutuua lkn ndio hvyo wanashindwa maana kazi tunazo fanya sisi wao hawawezi
 
Usihofu, nature itajishape tu kubalance mambo, kila kitu kina matokeo yake.

Mfano, sasa hivi kuna idadi ya vijana wapo tu wanamaliza vyuo hawana kazi. Kazi zinashikwa na mabinti. Baada ya muda jamii inakuwa na wanaume masikini na wanawake wenye uwezo kiuchumi. Nini kinafata?

Uhaba wa wanaume wenye uwezo wa kumtunza mwanamke, uwepo wa vijana mlenda mlenda na legelege na tegemezi, ongezeko la single mothers, jamii itaanza kuona umuhimu wa uwepo wa wanaume.

Ulinzi wa mtoto wa kiume utaongezeka. Semina za malezi ya mtoto wa kiume na kelele za muandae baba ajae zinashamiri, ajira zitamtazama mwanaume n.k n.k Ni suala la muda tu.
Hii inaweza isitokee mapema kwasababu dunia hii idadi ya watu ishakuwa kubwa hesabu zinataka tupungue kwa usalama wa baadae, kwahiyo wataona bora wanaume tuwe wachache ili uzao uwe kidogo
 
Ukizaliwa mwanaume we ujue Kila kitu kwako itakuwa ni tabu...

Huu wimbo ulimaliza Kila kitu.
Nature Inaonesha Mwanamke ni mtu wa kupokea halafu ana manipulate, refer hata kwenye sex hakuna kincho toka kwa mwamke kuingia kwa mwanaume lkn mwanamke ataingizwa vidole na ataachiwa mbegu zote ndani
 
Mwanaume hawezi kukandamizwa labda kama hajaamua kuwa mwanaume.
mkuu sio kweli. Sheria za masuala ya jinsia na mahusiano zinambeba zaidi mwanamke, kwa mwanaume kuchomoka labda uwe na msuli wa pesa ufanye umafia au uwe innocent to the extent that hakuna kijikisababu chochote cha kukutia hatiani. Mfano hizi kesi za ubakaji zinazowaandama wachezaji uko ulaya usifikiri kwamba walitumia nguvu kwa hao wanawake. Wengi walikubaliana unakuta hata uyo mwanamke alienda mwenyewe kabisa kwenye chumba cha hotel walipopanga kukutana ila mwanamke akatengeneza tu mazingira ya kumtia mwanaume hatiani ili apate pesa au umaarufu
 
Back
Top Bottom