Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 29,496
- 84,084
Sasa mbona unajikaaanga, Men uim
Kwahiyo nikiwa namhudumia lakini yeye anafanya kazi nyumbani na hatuna watoto, inamaana hatutagawana mali?
Sasa ambacho hujaelewa ni nini wewe kumhudumia ni jukumu lako kama naye anavyotimiza majukumu yake sasa ulitaka hizo huduma apate wapi wakati umemuoa ni mama wa nyumbani, kwenye kugawana ni kwa sababu mnahesabika mmechuma wote yeye ametimiza majukumu yake kama mke ili wewe ufocus kwenye kutafuta hizo pesa tu, hivyo naye ana mchango wake na ndio maana mnagawana hachukui zoteKama sababu ya kumlipa mwanamke 50% kisa wakati anafanya kazi za nyumbani nilimpotezea muda, kwamba nisingemuoa pengine angekuwa anafanya kazi mahala, angepata pesa, je namimi nisingemuoa si ningekuwa nina pesa nyingi tu? Kwasababu kala chakula changu, kavaa nguo zangu, katibiwa kwa pesa zangu, na bado mizinga ya baba mkwe na mashemeji, huoni kuwa sababu uliyoitoa haina mashiko?
Kama unaona hiyo ni hasara basi mruhusu naye atafute pesa kama wewe ili usiwe unamhudumia hapo hata mkigawana itakuwa afadhali, maana angalau naye alikuwa anachangia pato la familia lakini ndio ukubali kwamba majukumu ya nyumbani inabidi asifanye yeye tena bali muwe na msaidizi, au kama vipi muwe mnasaidiana wenyewe na pia ukubali kupoteza ile full authority kama mwanaume kwa sababu humhudumii
Waliotunga hizi sheria siyo wajinga waliona kwamba wasipoweka huu utaratibu wanawake watakuwa wanaachika sana huku wakiondoka mikono mitupu, kwa sababu jamii ilishajenga mtazamo kwamba mwanaume kuoa na kuacha mara kwa mara ni kawaida ila mwanamke kuolewa na kuachwa mara kwa mara ni umalaya, kwahiyo hili liliwafanya wanawake wajitahidi kuvumilia maovu ya wanaume na wapambanie ndoa ili wasiachike
Sababu wanajua wakiachika jamii itawatukana huku wanaume kwao kuacha siyo shida, muda wowote akijisikia kumuacha mkewe kwa sababu yoyote ile hata kama ni ya kijinga, anamuacha tu sababu anajua jamii haitamfanya chochote
Kama mnaona huu wanaofanyiwa wanawake ni upendeleo basi sidhani kama kuna jinsia iliyopendelewa kama yenu, maana enzi za wazee wetu wanaume mlipendelewa zaidi hata ya wanawake wanavyopendelewa leo hii, lakini mliona sawa na mlifurahia wanawake walipokuwa wanavumilia manyanyaso yenu sasa meza zimegeuka mnaona kama mnaonewa