Naomba mawazo yenu wakina dada (hata wakina kaka mkichangia sio mbaya)

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,583
10,086
Tuiangalie dhana ya 50/50 katika nyanja ya uchumi kwenye mahusiano. Hapo zamani mwanamke akupewa access yoyote kiuchumi kuanzia ajira, elimu, kumiliki mali, uongozi n.k katika hali kama iyo ni sharti ahudumiwe na mwanaume. Mwanamke hana ajira, hana makazi, hana mali sasa ataishi vipi lazima mwanaume awajibike kuhudumia hapo, that was a fair game.

Baadaye yakaibuka mambo ya haki sawa mpaka kufikia leo hii mwanamke kapewa access zote za kujipambania sasa hapa hili game liwe fair maana yake ule wajibu wa mwanaume kumuhudumia mwanamke lazima uondolewe, hapa lazima mwanamke akubali usawa unakuja na wajibu.

Lakini ukiangalia mwenendo wa mahusiano pamoja na kwamba tupo kwenye zama za 50/50 ambapo kila mtu anawajibika kujipigania mwenyewe inaonekana bado kuna privileges ambazo mwanamke alikua anazipata kutoka kwa mwanaume katika zama za mfumo dume na hataki kuziachia kwenye zama hizi za 50/50 ikiwepo takwa la kuhudumiwa na mwanaume.

Tunaomba mawazo yenu wakina dada, mnataka 50/50 ili mpewe access zote za kujitafutia muwe mnatoka nyumbani kutafuta mkate na mna-share sawa sawa na mwanaume cost zote za kumantain mahusiano/ndoa kuanzia mitoko, mahitaji ya nyumbani, bata n.k au mnataka mfumo dume na muondolewe access zote za kuwawezesha kujitafutia mfano ajira,elimu, kumiliki mali n.k ili muwe mnashinda nyumbani na kuhudumiwa na mwanaume?
 
Why does it have to be one OR the other??

Hakuna wanawake wanaochangia maendeleo ya familia?? Hakuna wanawake wanao-support wanaume wao pale uchumi wao unaposuasua??? Na je, hao wanawake waliopata "PREVELEDGE" ya ajira, elimu, kumiliki mali na uongozi, hawatimizi majukumu mengine kwa waume/wapenzi wao??? Kama mtu yupo kwenye mahusiano anayoona anatumika kuliko anachopata in return, then kosa ni lake binafsi kwakuchagua partner asiyeweza kukidhi mahitaji yake.

Kwenye mahusiano tunategemeana kuliko mnavyotaka kuaminishana vijana wa sasa. Kuanzia emotionally, financially, socially, and practically. Nyie mmeshikilia financial dependence tu ambayo hata sio wanawake wote wanaishi humo.

Anyway, mwisho wa siku kila mtu afanye maamuzi kuendana na mahitaji yake. Wale wanao-value true/genuine companionship watajitoa kadri wawezavyo kwa wanaowapa companionship bila kuona wananyonywa, because they don't feel like they are losing. Na wengine watalipia na kuhesabaiana services, like any other business.
 
Why does it have to be one OR the other??

Hakuna wanawake wanaochangia maendeleo ya familia?? Hakuna wanawake wanao-support wanaume wao pale uchumi wao unaposuasua??? Na je, hao wanawake waliopata "PREVELEDGE" ya ajira, elimu, kumiliki mali na uongozi, hawatimizi majukumu mengine kwa waume/wapenzi wao?...
Nahisi wewe dada/mama angu ni kizazi cha wanawake wa 80's kurudi nyuma haujui mtazamo wa kizazi cha wanawake wa kuanzia late 90's ambao ndio batch ya wanawake waliobebwa zaidi na upepo wa 50/50 na ferminism, hapa umeongea kwa hisia zaidi au kujijengea picha wewe binafsi bila kuangalia mwenendo kwenye jamii nzima. kwa kizazi cha sasa asilimia kubwa sana ya mahusiano maintanance costs zinabebwa na mwanaume, wanawake wanaochangia costs wapo lakini ni percent ndogo sana yaani tuseme 5% katika 100%
 
Why does it have to be one OR the other??

Hakuna wanawake wanaochangia maendeleo ya familia?? Hakuna wanawake wanao-support wanaume wao pale uchumi wao unaposuasua?...
Umeolewa?

Pisi kama wewe lazima muangukie kwa walugaluga dizaini ya mleta uzi sijui kwanini, ila umetoa madini sana bibie.

Hujalazimishwa kua na huyo mtu, ukiona hakupi kile kinasuuza roho yako unatemana nae tu, tafuta yule anaetaka kua mama wa nyumbani mbona wapo sana, na ni wengi mno.
 
Umeolewa??

Wewe hata haujaelewa lengo la mada. Kwa faida ya slow learners wenzako, lengo la mada sio kutaka kila mwanamke awe mama wa nyumbani au mpambanaji.

Lengo ni kujua wanawake wanataka kusimama upande upi maana uhalisia unaonesha ni vigeugeu wanachambua vile vipengele ambavyo wanaona hapa kuna masilahi yaani ukiongelea suala la nani anawajibika ku-provide cost za kudumisha mahusiano wanataka mfumo dume, tukisema basi mwanaume anaebeba izo cost apewe kipaumbele kwenye nyanja za kiuchumi ili aweze kubeba kwa utimilifu ilo jukumu hapo wanawake wanataka 50/50.

Hapa ndipo inatakiwa kuchagua kama wanataka 50/50 basi iwe applicable kwa ujumla wake na kama wanataka mfumo dume basi uwe applicable kwa ujumla wake. Umenielewa wewe kilaza?
 
Mahusiano ni kusaidiana, watu waliokatika mahusiano ni wale walioamua kusaidia kwa njia yeyote ile yaani wapo ‘interdependent’

ukishaleta mada za 50/50 kwenye mahusiano hayadumu

kama mtaamua kusaidiana saidianeni after all ni maisha yenu
 
Vipi hii assertion ya kusema mwanamke anahitaji huduma. Hauoni inatengeneza mazingira ya kuonekana mwanaume ni provide tu na mwanamke ni receiver tu? Maana mahitaji ya chakula, makazi, mavazi, bata n.k na mwanaume pia anahitaji kwanini hii assertion isiwe mutualy badala ya kuwa favoured kwa mwanamke tu?
 
Wewe hata haujaelewa lengo la mada. Kwa faida ya slow learners wenzako, lengo la mada sio kutaka kila mwanamke awe mama wa nyumbani au mpambanaji. ...
Usikwepe majukumu yako.

Kaa na mwenzi wako muulize hayo maswali, mjue mnalishaje familia yako.

Huyo bibie hapo Dr Lizzy kakujibu vyedi tu ndg.

Hoja yako si kua unataka upendelewe kwenye fursa, upate kamseleleko kisa unahudumia (una risiti za hizo huduma?).

Yaani wewe una mfumo dume kishenzi ndgu yangu.

Narudia hiyo sio ishu ya jamii ni ishu yako na mwenza wako, unataka mwanamke asisomeshwe, asipewe ajira ?? Kwanini uminye uhuru wa mwanamke kwasababu ya tamaa zako kiuchumi na kimamlaka?

Wanawake wote Tz wanataka mahusiano? Wanataka ndoa? Wanataka kuhudumiwa na Me?

Akili mgando hizo ujue aloo.
 
Wewe hata haujaelewa lengo la mada. Kwa faida ya slow learners wenzako, lengo la mada sio kutaka kila mwanamke awe mama wa nyumbani au mpambanaji....
Hii 50/50 ni ajenda ya kishetani kupitia watu wa magharibi, feminism, NGO's za kutetea wanawake nk. ni ajenda ya kishetani tangu awali kuharibu taasisi ya ndoa na familia kiujumla na kuifanya dunia kuwa mahali pa fujo, zinaa, uzinzi na vurugu za kila aina.

Kila kilichochema na chenye maadili kinaanzia na stability ya familia, tangu awali Mwanaume ndie aliewekwa mtawala na kiongozi. tabia na sifa zote za mwanamke zipo wazi na zinajulikana tangu awali, tabia na sifa zote za mwanaume zipo wazi na zinajukikana tangu awali.

Eti unadai 50/50, unadai mwanaume ndie awe mlishi na mtunzaji wa familia kiuchumi kwa sheria zilezile za zamani na akati fursa zote za ajira na kipaombele umemwekea mwanamke, yaani ajjra ukatoe kwa mwanamke, afu jukumu la kuwa provider wa familia akaabidhiwe mwanamue😀😁, hii dunia hii inakokwenda sio kabisa aisee.
 
Vishu Mtata soma hii paragraph uenda ikasaidia kidogo ku-unlock huo ubongo wako mgumu kuelewa
 
Why does it have to be one OR the other??

Hakuna wanawake wanaochangia maendeleo ya familia?? Hakuna wanawake wanao-support wanaume wao pale uchumi wao unaposuasua??? Na je, hao wanawake waliopata "PREVELEDGE" ya ajira, elimu...
Chukua maua yako kwa kuimombo inaandikwaje mkuu..☺
 
Nahisi wewe dada/mama angu ni kizazi cha wanawake wa 80's kurudi nyuma haujui mtazamo wa kizazi cha wanawake wa kuanzia late 90's ambao ndio batch ya wanawake waliobebwa zaidi na upepo wa 50/50 na ferminism, hapa umeongea kwa hisia zaidi au kujijengea picha wewe binafsi bila kuangalia mwenendo kwenye jamii nzima. kwa kizazi cha sasa asilimia kubwa sana ya mahusiano maintanance costs zinabebwa na mwanaume, wanawake wanaochangia costs wapo lakini ni percent ndogo sana yaani tuseme 5% katika 100%
Eishhh...mbona waniita mama tena??🙄Bado sijafikia umri wa kuwa na kijana wa umri wako bana, unless you are still in primary school.

Anyway, kwani jamii ni mkusanyiko wa nini kama sio individuals mpaka nisitumie hisia, mtazamo, na values zangu binafsi kujenga hoja??

Kwa jinsi ulivyoweka mada yako, ni dhahiri unajua wanawake tunataka nini, na kwamba hatuko tayari kuchagua kimoja. So...option zenu ni kukubaliana na hiyo "hali halisi" , au kuweka misimamo yenu itakayotulazimu sisi kuchagua kati ya usawa au utegemezi.
 
Anyway, mwisho wa siku kila mtu afanye maamuzi kuendana na mahitaji yake. Wale wanao-value true/genuine companionship watajitoa kadri wawezavyo kwa wanaowapa companionship bila kuona wananyonywa, because they don't feel like they are losing. Na wengine watalipia na kuhesabaiana services, like any other business.
Girl! :iLOVEyou:
 
Eishhh...mbona waniita mama tena??🙄Bado sijafikia umri wa kuwa na kijana wa umri wako bana, unless you are still in primary school.
Nimekisia uenda ukawa mama au dada fulani hivi wa makamo sio hiki kizazi cha 2000's
Kwa jinsi ulivyoweka mada yako, ni dhahiri unajua wanawake tunataka nini, na kwamba hatuko tayari kuchagua kimoja. So...option zenu ni kukubaliana na hiyo "hali halisi" , au kuweka misimamo yenu itakayotulazimu sisi kuchagua kati ya usawa au utegemezi.
Hapa sasa naona umenielewa vizuri na ndipo nilipo hitaji kujua mtazamo wenu ni upi. Usawa ili tuchangie costs au tegemezi ili turudi kwenye mfumo dume?
 
Umeolewa??
Pisi kama wewe lazima muangukie kwa walugaluga dizaini ya mleta uzi sijui kwanini, ila umetoa madini sana bibie.

Hujalazimishwa kua na huyo mtu, ukiona hakupi kile kinasuuza roho yako unatemana nae tu, tafuta yule anaetaka kua mama wa nyumbani mbona wapo sana, na ni wengi mno.
Kwanini mlugaluga lakini??😁

Honestly though, mi nashangaa sana wanaume wanaolalamika kila siku. Mfumo uliopo, upo kwasababu umekubalika/endelezwa/endekezwa kwa namna moja ama nyingine. Wasioukubali kweli wanaweza kuondoa kwa lazima kwa kukataa kujihusisha na wanawake wasioleweka/taka kuamua kama ni "wategemezi" au la.
 
Sio kila mtu anae-adress suala lililopo kwenye jamii maana yake analalamika kuna wanaoongelea tu ishu kwa kuguswa na masaibu yanayowakuta wengine, mimi katika kila nyanja ya maisha nina principles zangu kabla ya kuingia katika mahusiano na mwanamke lazima nimfanyie tathmini kama anaweza kuingia kwenye mfumo wangu mfano mimi siwezi kuhudumia girlfriend nishajiwekea kanuni mwanamke nitakaekuja kumuhudumia ni mke wangu tutakaekua tunaishi pamoja kama familia kwa maana iyo siwezi nikapalamia slay queens. Mimi mpenzi nilienae anaingia kwenye mfumo wangu lakini naishi na jamii kwaiyo napata taarifa kuhusu yanayoendelea kwenye mahusiano mengine, hata ivyo mada yangu haikua na lengo la kutaka tusimike mfumo dume au 50/50. Nimeongelea nafasi ya mwanamke katika mifumo yote miwili na nikataka kujua bila kutanguliza masilahi yenu, je mna-prefer upande upi
 
Kwanini mlugaluga lakini??😁

Honestly though, mi nashangaa sana wanaume wanaolalamika kila siku. Mfumo uliopo, upo kwasababu umekubalika/endelezwa/endekezwa kwa namna moja ama nyingine. Wasioukubali kweli wanaweza kuondoa kwa lazima kwa kukataa kujihusisha na wanawake wasioleweka/taka kuamua kama ni "wategemezi" au la.
Kabisa kabisa mkuu, mimi huwa nashangaa zaidi kuona mwanaume anamlalamikia mwanamke kwenye matumizi, si umuache ubebe unaeyeona anafaa kwako.

Huo ni ulugaluga
 
Back
Top Bottom