MKATA KIU
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,906
- 6,381
Mkuu hata mimi nafahamu kwamba Mamelodi Sundowns ni timu bora, ila kwa sasa hasa msimu huu tukubali tu kwamba imeshuka kiwango, ndio maana nikasema ni either wachezaji wameanza kuchoka au kocha kuna mahali anakosea
Nilikuwa natazama African soccer show kwenye supersports pundits ambao ni wachezaji wengi wa zamani kina mark fish wanasema mamelodi sundowns inakosea kwa kutaka kucheza possession football kwenye knock out stage za caf champions league.
Wakatoa mfano timu kama esperence ni timu yenye uzoefu mkubwa. In last 5 season imebeba ubingwa wa champions league mara mbili. Huku mamelodi hata fainali haijawai kufika in last 5 season. Hivyo ilikuwa ni idea mbaya kwa mamelodi kucheza na esperence kwa same style kama wanayocheza na weak teams. Kosa moja tu esperence anafunga goli sababu ya uzoefu wao wa kucheza mtoano kila msimu.
Pia wakalaumu usajili wa wachezaji wa mamelodi wanaotoka latin america.
Wale wachezaji ni walaini sana kucheza mpira wa ligi ya mabingwa africa. Wakatoa mfano hata waarabu wamelijua hilo ndio maana wanasajili watu weusi kutoka west africa ndio wanawaweka kwenye midfield. Mfano esperence mid field yao bwana mdogo wa miaka 20 wamemtoa nigeria. Ana nguvu kweli kweli kiasi cha kumfanya m chile wa bilioni 6 wa mamelodi asifanye chochote mechi zote 2.
Wameshauri mamelodi iachane na kutumia non african player kwenye mechi za mtoano za caf bali ipange watu wanaoujua mpira wa africa unachezwaje