Mamelodi ni Overrated, sijui ukubwa waliupataje

Mkuu hata mimi nafahamu kwamba Mamelodi Sundowns ni timu bora, ila kwa sasa hasa msimu huu tukubali tu kwamba imeshuka kiwango, ndio maana nikasema ni either wachezaji wameanza kuchoka au kocha kuna mahali anakosea

Nilikuwa natazama African soccer show kwenye supersports pundits ambao ni wachezaji wengi wa zamani kina mark fish wanasema mamelodi sundowns inakosea kwa kutaka kucheza possession football kwenye knock out stage za caf champions league.

Wakatoa mfano timu kama esperence ni timu yenye uzoefu mkubwa. In last 5 season imebeba ubingwa wa champions league mara mbili. Huku mamelodi hata fainali haijawai kufika in last 5 season. Hivyo ilikuwa ni idea mbaya kwa mamelodi kucheza na esperence kwa same style kama wanayocheza na weak teams. Kosa moja tu esperence anafunga goli sababu ya uzoefu wao wa kucheza mtoano kila msimu.

Pia wakalaumu usajili wa wachezaji wa mamelodi wanaotoka latin america.

Wale wachezaji ni walaini sana kucheza mpira wa ligi ya mabingwa africa. Wakatoa mfano hata waarabu wamelijua hilo ndio maana wanasajili watu weusi kutoka west africa ndio wanawaweka kwenye midfield. Mfano esperence mid field yao bwana mdogo wa miaka 20 wamemtoa nigeria. Ana nguvu kweli kweli kiasi cha kumfanya m chile wa bilioni 6 wa mamelodi asifanye chochote mechi zote 2.

Wameshauri mamelodi iachane na kutumia non african player kwenye mechi za mtoano za caf bali ipange watu wanaoujua mpira wa africa unachezwaje
 
Hakuna timu kubwa ambayo haija dominate ndani tuache kujazana ujinga na hilo ndio tatizo la mashabiki wenzangu wa simba na viongozi wanapitia humo humo kwenye huu ujinga angalia timu zote zilizo kua robo final CAF CL hakuna timu ambayo haifanyi vizuri kwenye ligi ya ndani sasa hivi unaidharau local league utaona umhimu wake tukikosa nafasi ya pili

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mkuu nisome tena sijaidharau ligi ya ndani, ila kumbuka kuwa yanga wanajiona ni bora na kikosi chao kimekamilika, lakini kwenye ligi ya mabingwa wameishia robo fainali sawa na simba tu ambao ni wabovu kwa sasa
 
Nilikuwa natazama African soccer show kwenye supersports pundits ambao ni wachezaji wengi wa zamani kina mark fish wanasema mamelodi sundowns inakosea kwa kutaka kucheza possession football kwenye knock out stage za caf champions league.

Wakatoa mfano timu kama esperence ni timu yenye uzoefu mkubwa. In last 5 season imebeba ubingwa wa champions league mara mbili. Huku mamelodi hata fainali haijawai kufika in last 5 season. Hivyo ilikuwa ni idea mbaya kwa mamelodi kucheza na esperence kwa same style kama wanayocheza na weak teams. Kosa moja tu esperence anafunga goli sababu ya uzoefu wao wa kucheza mtoano kila msimu.

Pia wakalaumu usajili wa wachezaji wa mamelodi wanaotoka latin america.

Wale wachezaji ni walaini sana kucheza mpira wa ligi ya mabingwa africa. Wakatoa mfano hata waarabu wamelijua hilo ndio maana wanasajili watu weusi kutoka west africa ndio wanawaweka kwenye midfield. Mfano esperence mid field yao bwana mdogo wa miaka 20 wamemtoa nigeria. Ana nguvu kweli kweli kiasi cha kumfanya m chile wa mamelodi asifanye chochote mechi zote 2.

Wameshauri mamelodi iachane na kutumia non african player kwenye mechi za mtoano za caf bali isajili watu weusi kama wakina aziz kii. Ambao wana nguvu ya asili ya mtu mweusi
Mkuu hapo kwenye style wanayotumia Mamelodi kucheza nakuunga mkono kwa asilimia mia hiyo style yao ya kucheza possession football ili timu pinzani ifunguke huwa inawasaidia kwa timu dhaifu ila wakikutana na timu kubwa huwa inawacost, lakini hapo uliposema wachezaji weusi wa kiafrika ndio wanafaa kwenye mpira kuliko wachezaji weupe wa mabara mengine kwa sababu ya nguvu za asili sidhani kama uko sahihi, kwa sababu mpira wa sasa unahitaji akili zaidi kuliko nguvu maana ingekuwa unahitaji zaidi nguvu basi timu za afrika ndio zingekuwa zinaongoza kwa ubora duniani lakini wote tunajua hali halisi tena kama hiyo Brazil uliyoisema ndio inajulikana kwa kuwa moja ya nchi zenye vipaji vikubwa vya soka
 
Hivi wewe akili za wabongo kwa ujuaji umezisahau?.Hapo wamekariri tu wanataka hao mamelodi ili wakibali ni timu bora basi wasiwe wanafungwa kabisa.Yaan ili mradi tu tuwe wajuaji hakuna la maana.Mtu anashindwa kuelewa hakunaga timu ambayo haishuki kiwango,na sababu ni nyingi.Kazi tunayo.
Si ndio hapo mkuu yani ndio maana nikasema mashabiki wengi wa yanga wana vigezo vyao wanavyovijua wenyewe vya timu kuitwa bora au mbovu, yani wao wanataka timu ili iwe bora basi isifungwe kabisa sasa jiulize ni timu gani duniani haijawahi kufungwa kama hadi real madrid wenyewe wanaweza kufungwa tena magoli mengi tu na bado hawaitwi timu mbovu, je hawa huku kwetu ni kina nani hadi wasifungwe tatizo watu hawajui kutofautisha kati ya timu mbovu na kushuka kiwango au wanajua ila wanajitoa ufahamu tu
 
Oohh kwahiyo mara hii ninyi mmeshakuwa wabovu siyo bora tena

Ndio sasa kwani hayo yote ni uongo si ni ukweli yani hiyo mbinu mliyoitumia ya kupaki basi timu yoyote hata ihefu wangeitumia wasingefungwa, mshukuru hata watu walivyokuwa wanawahype hao mamelodi iliwasaidia kucheza kiuogauoga, vinginevyo mngerelax mngefunguka mngekula nyingi
Huu ugoro tukaupeleke wapi ulioandika?
 
Nilikuwa natazama African soccer show kwenye supersports pundits ambao ni wachezaji wengi wa zamani kina mark fish wanasema mamelodi sundowns inakosea kwa kutaka kucheza possession football kwenye knock out stage za caf champions league.

Wakatoa mfano timu kama esperence ni timu yenye uzoefu mkubwa. In last 5 season imebeba ubingwa wa champions league mara mbili. Huku mamelodi hata fainali haijawai kufika in last 5 season. Hivyo ilikuwa ni idea mbaya kwa mamelodi kucheza na esperence kwa same style kama wanayocheza na weak teams. Kosa moja tu esperence anafunga goli sababu ya uzoefu wao wa kucheza mtoano kila msimu.

Pia wakalaumu usajili wa wachezaji wa mamelodi wanaotoka latin america.

Wale wachezaji ni walaini sana kucheza mpira wa ligi ya mabingwa africa. Wakatoa mfano hata waarabu wamelijua hilo ndio maana wanasajili watu weusi kutoka west africa ndio wanawaweka kwenye midfield. Mfano esperence mid field yao bwana mdogo wa miaka 20 wamemtoa nigeria. Ana nguvu kweli kweli kiasi cha kumfanya m chile wa mamelodi asifanye chochote mechi zote 2.

Wameshauri mamelodi iachane na kutumia non african player kwenye mechi za mtoano za caf bali isajili watu weusi kama wakina aziz kii. Ambao wana nguvu ya asili ya mtu mweusi
Hao Esperance wana wabrazil wawili, Marcelo Allende ni mtu kazi haswa cheki mechi alizocheza na Al Alhy alivyowasumbua viungo wakina Niang. Lucas Ribeiro ni top scores ligi kuu ya Africa kusini.

Temba Zwane "Mshishi" Tabia yake ya kutaka kupiga chenga kila sehemu ndio inafanya mipira mingi ipotee miguu kwake hata sehemu za maamuzi yeye anapiga chenga, Shalulile ushambuliaji wake wa kuvizia mabeki wakimkamata anakosa hata ontarget. Mamelod ana kikosi kizuri ni mwalimu kutumia wachezaji na mbinu zake
 
Tatizo mashabiki wa mamelodi wanaongeleaga mafanikio mechi kwa matokeo ya timu moja tu Al ahly. Huwezi kuwa bingwa wa africa kwa kumfunga Al ahly tu. Lazima uwafunge na wengine kwenye mtoano ndipo uende fainali ukabebe ubingwa.

Caf champions league inashirikisha timu zaidi ya 50.

Kumfunga al ahly sio kipimo cha wewe kupewa ubingwa.

Ina maana gani kumfunga Al ahly halafu timu zingine zinakuja kukutoa kila msimu fainali hufiki ? Wenzako wanaenda beba kombe na kuzidi kuongeza nyota kwenye logo zao na jezi zao.

Timu yenye bajeti ndogo Kama yanga tu unashindwa ifunga unaanzia wapi kubeba ubingwa wa caf champions league. Mchile Aliende alifanya maajabu gani mechi ya yanga ama mechi na esperence ? Ama mechi na petro ama mechi na tp mazembe ?

Hao latin America ni walaini laini hawafai kukaa kwenye nafasi za viungo kwenye mechi za mtoano za ligi ya mabingwa. Ndio maana hata mkude hakupata shida kuwamudu. Maana hawana nguvu. Africa mpira unachezwa kwa nguvu na kasi.

Esperence ni wa arabu watunisia ila nafasi za viungo wamewapa wa nigeria sababu wanaujua mpira wa africa ulivyo
 
Mkuu nisome tena sijaidharau ligi ya ndani, ila kumbuka kuwa yanga wanajiona ni bora na kikosi chao kimekamilika, lakini kwenye ligi ya mabingwa wameishia robo fainali sawa na simba tu ambao ni wabovu kwa sasa
Malengo ya Simba na Yanga yalika sawa? wao lengo lao ilikua makundi sisi nusu fainali domestically bado wapo kwenye race sisi hatumo unaweza kujilingalisha nao?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Malengo ya Simba na Yanga yalika sawa? wao lengo lao ilikua makundi sisi nusu fainali domestically bado wapo kwenye race sisi hatumo unaweza kujilingalisha nao?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hayo yalikuwa ni malengo ya awali sababu walikuwa bado hawajajiamini na sababu ya historia, yani huwezi kumuambia shabiki eti safari hii tunaenda hadi fainali wakati una miaka zaidi ya 20 hujaingia hata makundi kwahiyo wakaweka kwanza malengo ya kufika makundi, ila walipoingia tu robo fainali bila shaka ulisikia kauli zao mara oo "yanga ni kikosi bora huyo mamelodi atapigwa nje ndani", mara oo "tutafika hadi fainali na hili kombe tutachukua", na kauli kama hizo
 
Acha uongo mamelodi haijaanzishwa mwaka 1996. Mamelodi ipo tangu mwaka 1960s huko.

Weka ushahidi ku prove kama mamelodi ni timu ya mwaka 1996

Ni kweli mkuu nimedanganya sio 1996, ila nawe pia umedanganya sio 1960’s ni 1970.
 
Nimegundua wanaosema Mamelodi ni overrated ni mashabiki wa Yanga wana sababu yao (bado wanaumizwa kutolewa kule ilihali waliona wanawaweza) ni hali tu ya kishabiki.

Mamelody huyu anashindanishwa haswa na timu za Northern Africa Zone, kwa huko ni sahihi kwa timu kama Al Alhy Casablanca wote wawili, Esperance.

Huyu Al Alhy ndio timu ina makombe mengi duniani kwa timu official, imewazidi timu nyingi sana za ulaya, sio mchezo wa jamaa wapo serious na wanamipango ndani na nje ya uwanja. Zamalek amewazidi akina Chelsea, Arsenal City.

Ubora unapimwa kwa namna mbali mbali, both official na personal (kutegemea na interest). Official inapimwa kwa mafanikio yao ndani na nje ya uwanja. Personal ndio kama hivyo mpira mzuri, upinzani wa kiderby n.k.

Bwana hawa jamaa tuseme tu Yanga wameongezeka ubora na sio wabovu kama wengi wanavyojaribu kuwa rate. Hakuna timu ya Tz imewahi kupenya hiyo Nusu Hakuna na huenda tukachukua muda karata zisipochangwa vizuri.

Kwenye ukanda huu wa jangwa la sahara bado tunajikongoja kuwafikia akina Mamelody, akina TP Mazembe na hao wa ukanda wa Kaskazini mwa Afrika.

Mamelody kwa sasa wanastruggle sana , Mamelody ile ya Pitso Mosimane ilikuwa timu nzuri bana”,. Kumchezesha mwarabu hamsa hamsa sio jambo dogo ujue, Al Alhy wazee wa kujiuliza wakasema ni nini hiki kitu nyuma yake kuna nani wakagundua ni Pitso Mosimane wakambeba.
 
Watu wanaangalia performance yao ya hivi karibuni msifikiri wanaropoka tu, msimu uliopita tu hapo walimpiga Al Ahly goli 5 na msimu huu wamechukua kombe la AFL, huku wakimtoa Al Ahly kwenye semi finals

Bado hatujaongelea AFCON iliyoisha mwaka huu, timu ya SA ilivyoperform vizuri hasa ilipoitoa Morocco tena huku ikiondoka na clean sheet, na zaidi ya nusu ya first eleven ya SA walikuwa ni Mamelodi Sundowns

Sema basi tu kwa vile walikutana na Nigeria ambayo wachezaji karibu wote wanachezea vilabu vikubwa Ulaya, ndio wakatolewa wakaishia kuwania na kushinda nafasi ya tatu, kwahiyo siyo kwamba ni timu ndogo inawezekana labda imeanza tu kushuka viwango au kocha kuna mahali anakosea
Nadhani ninyi ndio mlioleta sifa za uongo mitandaoni.
Al Ahly kufungwa goli 6 kwa mbinu za nje ya uwanja siyo ajabu.
Hizi zikikuwa figisu tu kama za yanga kwa Simba.Uchawi jumlisha kuchezesha timu kwenye uwanja wenye mazingira magumu haiwezi kuipa sifa mlizokuwa mnatoa
 
Ni kweli mkuu nimedanganya sio 1996, ila nawe pia umedanganya sio 1960’s ni 1970.

Screenshot_20240503-114340_Firefox.jpg

Mimi sijadanganya.

Official Website ya Mamelodi sundowns inasema timu yao imeanzishwa miaka ya mwanzoni ya 1960s.

Mimi sijadanganya. Wewe ndio muongo unaesema mamelodi imeanzishwa mwaka 1996
 
Nadhani ninyi ndio mlioleta sifa za uongo mitandaoni.
Al Ahly kufungwa goli 6 kwa mbinu za nje ya uwanja siyo ajabu.
Hizi zikikuwa figisu tu kama za yanga kwa Simba.Uchawi jumlisha kuchezesha timu kwenye uwanja wenye mazingira magumu haiwezi kuipa sifa mlizokuwa mnatoa
Al Ahly hafungwi na Mamelodi kwasababu ya mbinu za nje ya uwanja bali kwasababu ya kuzidiwa mbinu na uwezo uwanjani. Laiti kama ingekuwa ni swala la mbinu za nje ya uwanja basi Mamelodi wangekuwa wanafungwa na Al Ahly wakienda Misri. Lakini cha ajabu mara ya mwisho Mamelodi kufungwa na Al Ahly pale Misri ni mwaka 2021 ambako Al Ahly alishinda goli 2:0 hatua ya robo fainali klabu bingwa mkondo wa kwanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom