KERO Hii Barabara ya Dodoma – Iringa ni hatari kwa usalama wa watu na vyombo vinavyopita

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Habari wana JF, hii video nimeirekodi kwa mikono yangu mwenyewe, inaonesha Barabara ya Dodoma to Iringa jinsi ilivyo hatarishi kwa maisha ya watu wanaotumia, barabara ina viraka vingi na mahandaki mengi sana.

Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.

Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.

Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.

Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.
Pia barabara ya makambako njombe , barabara ya mwanza[nyerere road](nyanguge hadi lamadi)
 
Ila yule mkandarasi aliyejenga barabara ya Uyole Mbeya hadi Malawi ni mkandarasi bora kuliko wote katika barabara zote nilizopita,barabara ina zaidi ya miaka 25 lakini iko fresh
 
Jamaa alikua waziri, na nasikia alikataa kuizindua hiyo Barabara kwasababu hakuridhishwa na kiwango cha ujenzi. Lakini boss wake akaenda kuzindua.
Aliizindua Magufuli mwenyewe akiwa Rais. Sasa kama yeye ndiyo alikuwa Rais, bosi wake alikuwa nani!?
 
Ila yule mkandarasi aliyejenga barabara ya Uyole Mbeya hadi Malawi ni mkandarasi bora kuliko wote katika barabara zote nilizopita,barabara ina zaidi ya miaka 25 lakini iko fresh
upo sahihi mkuu... barabara bora sana ile
 
Back
Top Bottom