KERO Hii Barabara ya Dodoma – Iringa ni hatari kwa usalama wa watu na vyombo vinavyopita

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wenyewe wanakwambia malori makubwa ya kubeba makaa ya mawe kutoka Songea kwenda Rwanda ndio yanaharibu hiyo barabara ...lakini cha ajabu hayaharibu barabara ya kutoka Songea hadi Iringa😀😀
Kwa hiyo wanataka hayo malori yapite wapi??
 
Hii barabara inahitaji kujengwa upya au matengwnezo makubwa, kweli imekua kero kwa watumiaji wa barabara hii
 
Hii barabara inahitaji kujengwa upya au matengwnezo makubwa, kweli imekua kero kwa watumiaji wa barabara hii
Kila siku mtakuwa mnajenga upya
Au ndiyo ule usemi,sisi tukale wapi!

Ova
 
Naunga mkono hoja hii,T5 ni road to hell na ndio maana royal families ni V8 tu kwa kodi yangu,mwenye IST hapo ataibeba mgongoni!,Tanzania barabara ni bado ,siku tukiukubali ukweli huu na kuanza kufanya kazi smart ndio siku tutaanza kutambaa,wenzetu wa Zambia ile T2 yao wanailamba safi sana,yaani in 40 day's kuingia na kutoka border ya Nakonde itakua super,sisi T1 yetu tunatia viraka,nini wanakifanya pale Kitonga Pass sielewi kabisa,serikali ya ccm hawana anything to brag about
 
Habari wana JF, hii video nimeirekodi kwa mikono yangu mwenyewe, inaonesha Barabara ya Dodoma to Iringa jinsi ilivyo hatarishi kwa maisha ya watu wanaotumia, barabara ina viraka vingi na mahandaki mengi sana.

Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.

Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.

Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.

Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.

Jicho la kizalendo ndo lipi? HAKUNA malendo Tanzania.
 
Hao walevi bado hawajawahi kukutana na barabara mbovu kweli.
Wanaendesha mabio kama hivyo na huku wanalalamika.
 
Na haina miaka 15 lakin imechoka vibaya mno
Mkuu hata miaka 10 haijatimiza ilianza kubomoka ikiwa Bado mpya
1713526166903.jpg
 
Kiwango duni cha barabara, utitiri wa malori na hizi mvua kubwa vimechangia sana uharibifu wa barabara. Malori yamekuwa mengi mno
 
Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.

Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.

Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.

Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.
Ninapopita hii barabara, kila ninapoingia shimo kwa nguvu nawatukana Mkuu wa Tanroads, kisha Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Miundo Mbinu, halafu Mbunge wa sehemu nayopita, kisha Mameneja wa Tanroads wa Dodoma au Iringa.

Karibu nitawaingiza viongozi wakuu. Ila uzuri nawatukana nikiwa mwenyewe kweye gari!

Kinachonishangaza ni kwamba, hivi Tanroads hawaoni, maana haya mashimo yanaongezeka kila siku.

Meneja Mkuu wa Tanroads haoni?
Waziri wa Ujenzi haoni?
Waziri wa Miundo Mbinu sijui, haoni?
Wabunge wa maeneo haya hawaoni?
Mameneja wa Tanroads Dodoma na Iringa hawaoni?

Na sasa, Majaliwa haoni?
Na Samia je, haoni?

Na hasira zangu zaidi ni kwamba kwa kilakilomita nayoendesha gari kwenye hii barabara, nakuwa nimechangia urekebishaji wa mashimo. Shukurani Tanroads wanazonipa ni kuingia shimo na kuharibu shockk ups zangu. Hawa watu sijui tuwafanye nini kwa kweli.

Hivi kwa kuwa wao wanatumia V8 zinafukia haya mashimo basi sisi wengine sio muhimu na IST zetu?
 
Tunajenga na nani?
Ova
😄 basi mkuu nmekuchokoza
Ila wahusika wakuu wenyewe kujenga barabara ikatayo kaa miaka 50,au 70 hawataki

Ova
Mchina hana shida, unawapa gavoo bajeti 30B wanakwambia ipunguze fanya kwa 20B, kampuni nayo inataka hela akikataa project wapo watakaofanya hata kwa 15B, so anakupa kitu cha hela yako.
Mjapani ndomana alijiondokea zake

Ova
 
Back
Top Bottom