KERO Hii Barabara ya Dodoma – Iringa ni hatari kwa usalama wa watu na vyombo vinavyopita

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa hapo kwa shetani ni Dom au Iringa! 😀
Hii barabara lami yake ni ile ya kihuni ile unatanguliza udongo halafu lami ujiuji flan hivi halafu wanamwagia Kokoto zile ndogo mnaruhusiwa kupita pita inajishindilia.
Dodoma kikugu na Iringa kuanzia Nduli ndio kuna lami ile lami tunayoijua
 
Habari wana JF, hii video nimeirekodi kwa mikono yangu mwenyewe, inaonesha Barabara ya Dodoma to Iringa jinsi ilivyo hatarishi kwa maisha ya watu wanaotumia, barabara ina viraka vingi na mahandaki mengi sana.

Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.

Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.

Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.

Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.
Ilianza kuharibika mara baada tu ya kuzinduliwa hata mwaka haukuisha hasa kipande cha Dodoma-Mtera. Hapo Hayati alipigwa kama hakupiga yeye.
 
Barabara zote mpya zimechakaa balaa. Kuna ile ya kutoka Mbeya kwenda Chunya. Wamepanga hadi iende Tabora. Mashimo matupu. Sema waambie jamaa wasiwe wanaendesha wakiwa kinywaji, ni hatari kuliko mashimo:D
 
Na mbunge wa wakati ule malechela alichelewa sana kuwaletea maendeleo watu wa huko,hiyo barabara ilitakiwa ijengwe miaka 30 huko iliyopita

Ova
 
Barabara zote mpya zimechakaa balaa. Kuna ile ya kutoka Mbeya kwenda Chunya. Wamepanga hadi iende Tabora. Mashimo matupu. Sema waambie jamaa wasiwe wanaendesha wakiwa kinywaji, ni hatari kuliko mashimo:D
Kuna uhuni sana ktk ujenzi wa barabara unaofanyika
WANAJIHUJUMU WENYEWE HAWA

Ova
 
Habari wana JF, hii video nimeirekodi kwa mikono yangu mwenyewe, inaonesha Barabara ya Dodoma to Iringa jinsi ilivyo hatarishi kwa maisha ya watu wanaotumia, barabara ina viraka vingi na mahandaki mengi sana.

Nimeiangalia kwa jina la kizalendo na kugundua kuwa hii barabara inahitaji matengenezo makubwa.

Barabara hii ni mzigo kwa Serikali na walipa kodi.

Mbaya zaidi Wakala wa Barabara - TANROADS Dodoma wao wanachimba wanajaza udongo wanaondoka, tofauti na upande wa Iringa ambao wao wanaziba mashimo na wanajitahidi ku-maintain barabara.

Wananchi tumelalamika sana kuhusu hii changamoto, ukiangalia hapo kwenye video utaona jinsi gani ambavyo dereva unahitaji kuwa makini, la sivyo unaweza ajali ni nje-nje au kuharibu magari.
TANROADS POKEENI HII, INAWAHUSU.
 
Miaka hiyo mb malechela tunaenda huko njiaa ni ya vumbi
Unajiuliza hii dodoma to iringa Road,mbona ni barabara muhimu sana kwa kuunganisha iringa dom
Lakini haifanyiki kitu
Malechela hata siku moja sijawahi msikia akililia itengenezwe sana sana yeye anajltulia kwake mvumi tu

Ova
 
Barabara nzuri niliona Mbeya kwenda Sumbawanga ila ni miak imepita sijui nako sahiz hali ipoje
 
Toka miaka ya 2020 ilikuwa imeshabomoka sana
Hasa mkikaribia Dodoma mkishavuka mtera kule,ni noma sana.

Ni vile wengine tumetokea vijiji vya barabara za vumbi mwanzo mwisho tukawa tunaona normal tu.
 
Aisee vijana wa 2000 mna matatizo sana.
Si tumekesha hiyo njia enzi ni matope tunakunywa ulanzi tunaendelea na safari.
Hatujawai kuloloma.
We umekuta lami unaloloma,
Kanywe uji kwenu
 
Naunga mkono hoja hii,T5 ni road to hell na ndio maana royal families ni V8 tu kwa kodi yangu,mwenye IST hapo ataibeba mgongoni!,Tanzania barabara ni bado ,siku tukiukubali ukweli huu na kuanza kufanya kazi smart ndio siku tutaanza kutambaa,wenzetu wa Zambia ile T2 yao wanailamba safi sana,yaani in 40 day's kuingia na kutoka border ya Nakonde itakua super,sisi T1 yetu tunatia viraka,nini wanakifanya pale Kitonga Pass sielewi kabisa,serikali ya ccm hawana anything to brag about
Mkuu ivi
Mm huwa napenda kusoma alama za barabara lakin
Izi sijui T1 AU T2 au T16 huwa zizielewi
Msaada please??
 
Shujaa ndie aliesimamia barabara hiyo akiwa waziri wa ujenzi
Na ndiye aliyeizindua akiwa Rais... Na wakati anaizindua tayari ilikuwa imeshaanza kuwekwa viraka... angemfokea nani wakati yeye ndiye alikuwa waziri wakati inajengwa????
 
Kwa hii komenti yako unaonyesha ni jinsi gani ulivyo kiazi! Kama taifa tuna hasara kubwa sana ya kuwa na vijana wa dizaini yako .
Punguza hasira kamanda, sio mimi niliyesababibisha mvua jijin hali usafir ni daladala. Lazima uwe na hasira tu 😂😂
 
Back
Top Bottom