Wakandarasi wa barabara (Nyanza Roadworks) hawafukii mashimo walipochukua vifusi, maeneo ya Iyumbu, Block C, Dodoma na kusababisha HATARI

2Y2

New Member
Dec 27, 2023
1
0
Habari,

Tunaomba ushauri ili tupate msaada kutoka kwa mamlaka husika. Mimi ni mmoja wa wakazi wa Block C, Iyumbu West, Dodoma.

Tuna changamoto ya mashimo / makorongo makubwa yaliyochimbwa na kampuni ya Nyanza Roadworks wakitafuta kifusi kwa ajili ya matengenezo ya barabara, na mpaka sasa wameyaacha hivyo hivyo bila kuyafukia / site restoration (Nimeambatanisha picha).

Tumejaribu kwenda NEMC tukakwama na wakasema hawawezi kutusaidia, tulitakiwa kwenda wakati wanachimba ndio wangewasimamisha.
20231217_123715.jpg
20231217_123721.jpg
20231217_123727.jpg
20231217_123812.jpg
20231217_123910.jpg
20231217_123913.jpg
20231217_123918.jpg
 
Back
Top Bottom