Jemima Mrembo
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 2,797
- 8,039
Zumaridi ameudhihirishia umma wa Watanzania kuwa yeye ni mhitaji wa tiba ya afya ya akili.
Zumaridi amekuwa akijibasibu kwamba yeye ni mungu na amekuwa akipata wafuasi ambao wanamuamini na kumheshimu. Pia wapo ambao wamediriki kuachia shughuli zao zote za kimaendeleo ili tu wamtumikie Zumaridi mungu wao.
Hamna mungu asiye na maskani. Yahwe au Jehova maskani yake ni mbinguni, sakafu za dhahabu na huko ni kusifu na kuabudu.
Allah, maskani yake ni peponi, kwenye wanawake wazuri, mito ya pombe tamu na starehe za kila aina.
Shiva maskani yake ni mlima mtakatifu wa Keilash. Mlima ambao hamna kiumbe ambaye amewahi kuukwea..
Zumaridi yeye ni mungu wa namna gani asiye na maskani? Anaenda kutembea kwa Mungu wa mbinguni?
Sifa kuu ya mungu yeyote ni wivu. Kila mungu anataka aabudiwe yeye tu na si mwingine, ndio maana vita za kidini hazikomi kila mtu kumtetea mungu wake.
Zumaridi apelekwe haraka Mirembe. Asije akawachoma waumini wake kama Kibwetere.