Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki
Thursday, March 3, 2016
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.
Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita, jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.
“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.
Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.
Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.
“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.
“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.
Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.
Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.
“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:
“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.
Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.
Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.
“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”
Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.
“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.
Chanzo Mpekuzi blog
Anabip fani yake anatudanganya anafikiri sisi watoto Tanzania ya Leo sio ya Jana miaka 50 iliyopita yakudanganywa danganywa.Nafikiri kuanzia huyo akyekuwa anasimia uchaguzi na awo wanasheria wawajibishwe kwa kupotosha,kusababisha uvunjivu wa Amani na kuingizia jiji na serikali hasara kwa gharama za uchaguzi uwo.Huyu jackeline mosha ni jipu atumbuliwe mara moja; upande anasema hawakujirudhisha na zuio lile kabla ya kumkabidhi Mmbando then anadai kufanya kazi kitaalamu!? Atumbuliwe huyoo!
Justice delayed is justice denied. Akahojiwe hata kama on her death bed. Mbona anaongea. Serikali isipunguze kasi kwa hili.Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki
Thursday, March 3, 2016
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.
Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita, jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.
“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.
Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.
Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.
“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.
“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.
Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.
Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.
“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:
“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.
Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.
Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.
“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”
Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.
“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.
Chanzo Mpekuzi blog
alafu alivyo mpuuzi anakwambia yeye alipewa asome hakujua,sasa umesomaje kama hukujua au hata kusoma kwahiyo hajui??hivi hawa wanajitengenezea mazingira gani baadae baada ya kuondoka madarakani??wakati mwingine nikijua yale majipu yao nikigundua lilikuwa linatoka kwenye chama lao hata siyaone huruma maan mengi ni masomi ila yanaishi kiuwogouwoga na kinafiki tu,yaani ujanja ujanja wakitotoNimekuwa najiuliza kuwa inawezekanaje ATCL ina wafanyakazi zaidi ya 200 (mwenye data sahihi anikosoe) lakini wana ndege moja tu. Katika utaratibu wa kawaida hawa wote wanafika kazini lakini hakuna anayetambua kuwa 'hawana kazi ya kufanya' na mwisho unasikia umefanyika ufisadi wa US $800,000 (dollar laki nane)!!!!
Na kwa RAS kutoa kauli kama hii angelilinda heshima yake ya kuumbwa kwa kujiuzuru ili kuchochea waliodanganya kufikishwa mbele ya sheria.
Ajabu zaidi ni kuwa songombingo hizi zote zimewafikisha Mh. Mdee na Mh. Mwita mahakamani, vyombo vyetu vya usalama ndio vimewabaini kuwa na makosa!!!!
'kweli Tanzania ya viwanda inawezekana'.
Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki
Thursday, March 3, 2016
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.
Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita, jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.
“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.
Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.
Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.
“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.
“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.
Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.
Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.
“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:
“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.
Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.
Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.
“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”
Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.
“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.
Chanzo Mpekuzi blog
Well said mkuu haya majibu ya huyu Mwanasheria yameniacha hoi kabisanarudia kauli yangu ya kila siku,ukiwa mwanaccm lazima uwe hayawani...!!hebu fikiria mwanasheria makini wa jiji naye anakili kuwa alitoa hilo zuio bila kujua kama limwkwisha muda,vipi kuhusu mikataba wanayotakiwa kutoa ushauri wakisheria kulinda maslahi ya taifa??yaani unakuwa kwenye nafasi nyeti lakini kumbe nimbumbumbu wa kutupwa,chochote kinachokuja mbele yako kisa kimetoka kwa boss unapitisha tu..!!Siku ikiondoka ccm madarakani itabidi magereza yaongezwe maana mapuuzi yakufungwa nimengi sana
simbachawene alikuwa wapi wakati wote huo,yaani kipi hakijui hasa katika hili unataka kunambia wizarani na karemjee ni mbali sana simbachawene achelewe kupata kupata nakala ya zuioHuyu jackeline mosha ni jipu atumbuliwe mara moja; upande anasema hawakujirudhisha na zuio lile kabla ya kumkabidhi Mmbando then anadai kufanya kazi kitaalamu!? Atumbuliwe huyoo!
Labda haamini kama tamko la Mahakama ni la kweli?Yaani hii ni hatari sana, yaani Mwanasheria Kabisa na ambaye ndie mtetezi wa Jiji ndio anajibu hivyo, mimi nna wasiwasi kutakuwa na Mikataba mingi wameusika sasa wanaogopa Mkono wa Sheria na hapa nadhani issue sio chama pekee kuna baadhi ya Watumishi ni wahanga wa hili sakataHivi mnaojiita viongozi nchi hii mnajitambua na kutambua wajibu wenu kwa mnaowaongoza? Nina wasiwasi wa jinsi au njia mlizozitumia kupata hizo nafasi zenu ni ama mlizipata kupitia kwa waganga wa kienyeji kwani wao hukupa masharti ambayo hayakupi nafasi ya kuhoji.
Nayasema haya kwa jinsi waziri, ras na wanasheria wa jiji wanavyojitetea kidhaifu hivi. Waziri mhusika, kama mahakama imekanusha kuhusika na zuio batili lilisomwa unataka ras akuandikie kukuomba radhi au nini labda! Acheni kuleana huku mkivunja amani kwani hamjui chanzo cha moto ni cheche? CCM msiviringie vyombo vya usalama na kuvivuta upande wenu ili kuwanyanyasa walio wengi kwani ipo siku watagoma kuwa upande wenu.
Waziri wachukulie hatua za kinidhamu watendaji wako waliohusika na kadhia hii akiwamo Mmbando.
Haaa haaa ndio wataalamu wetu hao halafu ndio unataka akapamabane kwenye kesi na Tundu LisuSasa utaalam upo wapi hapo wakati nyaraka zenyewe hawazisoma bali wanazi forward kama messangers tu.
aliyet
aliyetengeneza zuio mahakamani masawe, aliyepeleka zuio ukumbini mosha, aliyenyakua zuio kutoka kwa mwenyekiti mdee nyie wachagga acheni kucheza na akili za watu.
Hilo swali ni zuri na anayetakiwa kujibu ni Siro anaye angalia kaangukia wapi badala ya kuangalia kajikwaa wapi ?Haya sasa kwa hao waliofanya upuuzi huo na hao wabunge wanaosumbuliwa kuwekwa mahabusu ni nani hasa anayetakiwa kuwekwa ndani na kushitakiwa kwa tukio hili kama sio hao wanasheria pamoja na huyo mtoa tamko la kuhairisha uchaguzi huo.