Zitto Kabwe ajisalimisha polisi

Kweli ngoja tusubiri tuone nini kinatokea; tena naomba wadau tuwe kimya na wavumilivu ili tuanze kuthibitisha hofu yetu kuwa, kile kinachoitwa "chaguo la Mungu" kinabadilika na kuwa zimwi lisilotujua. Kweli Tanzania inafikia hapa; viongozi wa kisiasa kukamatwa, kudhalilishwa na kuzuiwa wasifanye siasa? Kweli tumefikia mahala ambapo sasa hatupaswi tena kujadili mambo yanayohusu taifa hili kwa uwazi na eti tukithubutu tunaweza kukamatwa. Hii ni aibu ya kutisha!

Natoa wito kwa wanaharakati na wazee/viongozi wastaafu; wasomi na wanasheria kuunganisha nguvu na kuzuia (kisheria na kwa maridhiano) muendelezo wa udhalimu unaowezekana kukita mizizi yake katika taifa hili. Mikakati hii ya kukaba/kubaka democrasia haiwezi kuachwa kuendelea, kwa sababu mwisho wa siku Mungu atawahukumu wadhalimu lakini sisi tutakaoendelea kuuona udhalimu ukiendelea bila kufanya chochote kuusitisha, hukumu yetu itakuwa ni kali zaidi.

Na tumuombe Mungu alete uvuvio na hekima kwa viongozi wa kisiasa; wadau wa utawala bora ili watawala wafanye mageuzi chanya ili waiongoze nchi hii katika misingi sahihi ya kujenga nidhamu ya hiari na upendo badala ya vitisho na chuki.

MUNGU ibariki Tanzania
 
Katika Taarifa ya Habari ya TBC1 ya Saa kumi Jioni Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya DSM amekaririwa akisisitiza kwamba Polisi bado wanamtafuta Zitto Kabwe na kwamba watahakikisha anakamatwa ikiwa hatajisalimisha kama kweli yeye ni mzalendo.

UPDATES

Mwenyekiti moja ya kamati za Chama ametuma ujumbe huu

Habari.
Nimepata simu ya Kamanda wa Polisi Wambura saa tisa na nusu. Na akaniomba nimfikie Kiongozi wa Chama na kumwambia afike kituo cha polisi cha kati.

Mimi, Kiongozi wa Chama na Mwanasheria tuko njiani kuelekea kituoni.
Kiongozi wa chama ameomba tuwe watulivu tukawasikie wanachoitaji na tutawajuza yanatoendelea.



Vipi wamempiga mbata? Itakuwa kazi bure kama Askari wetu hawajamtia mbata!
 
Kwa hii nchi yetu ilivyo huitaji kutumia nguvu kubwa kuwazuia wapinzani, waletee watanzania maendeleo uone kama utapata upinzani mkubwa, pamoja ukosefu wa elimu tulionao watanzania ila wengi ni wenye busara na hekima.

JPM alivyoanza utawala wake wachache sana walimpinga, wengi tulimsapoti na hata wapinzani tulikosa hoja, hata harakati zilipungua, ila sasa kwa kitendo cha kuminya demokrasia na kubana uhuru wa vyama vya upinzani kufanya harakati zao kisiasa, zinaondoa umoja wa kitaifa.

Serikali inatakiwa ijue upinzani sio kina Mbowe peke yao, hata kwenye maofisi ya umma kuna wapinzani wengi tu.
 
Ina maana zitto ametafutwa na polisi kwa siku mbili bado hawajampata,sasa amewezaje kuongea na waandishi wa habari?Yaani polisi wameshindwa kumpata zitto? Naanza kuhisi zitto ni beyond sirro kinetwork ndani ya jeshi la polisi au hakuna wakujitoa kafara direct kumtia nguvuni ? mwisho wa siku polisi kama hakuna report yoyote ya uvunjifu mbona wanampa coverage ?
 
Back
Top Bottom