Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
IMG_0269.jpeg


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imehimiza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda mema na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Zanzibar ni nchi yenye historia kongwe ya uvumilivu wa kidini ambapo Uislamu na Ukristo uliingia mapema kuwa sehemu muhimu ya utamaduni uliodumu kwa karne nyingi. Hii inatufundisha kuhusu ustaarabu wa Wazanzibari kuvumiliana kidini na ndio msingi wa mshikamano miongoni mwetu.

Serikali inalaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kufanyika sehemu mbalimbali Zanzibar, kadhia hiyo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini.

Aidha, Serikali inawahimiza wananchi kujizuia kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mtu binafsi katika kuabudu.

Ikumbukwe Zanzibar inaongozwa kwa Katiba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mamlaka ya kullinda Katiba ya nchi na watu wake, hivyo hatua yoyote ile yenye kuhatarisha Umoja, Amani na Mshikamano haitavumiliwa.

Serikali itaendelea kulinda haki na uhuru wa mtu kuabudu kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hivyo, tuendelee kudumisha amani na upendo kama mafundisho ya dini zetu yanavyotutaka, tofauti zetu za kidini zisiwe chanzo cha kuvuruga amani, umoja na mshikamano.

Pia soma:
 
kimsboy jitahidi uwe unatumia akili. Hakuna Katiba ambayo mla hadharani anavunja.

Mkiruhusu watu waishi kama wanyama kujiamua sheria mkononi ni hatari hata kwa dini yenyewe.

Mimi jana nimeshinda sehemu na mafundi. Wamefunga lakini wanatukana kuanzia asubuhi mpaka jioni. Kisha wanaitisha futari wanafuturu.
 
Viongozi wanayachochea wenyewe kwa kisingizio cha mila, desturi, na utaduni wa Zanzibar yakiwashinda wanajidai "kulaani"!

Kama Zanzibar ni ya dini moja wawe tu wawazi na iingizwe kwenye Katiba na sheria ili wasiohusika waondoke Zanzibar wakaishi mahali salama kwao!
 
Back
Top Bottom