Mwanadiplomasia Mahiri
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 489
- 1,898
Leo nimeona niwaletee kisa cha Zambia kupoteza marais wao wawili wakiwa madarakani ndani ya kipindi cha miaka 6.
Levy Patrick Mwanawasa alikuwa Rais wa awamu ya tatu na Rais wa Kwanza kufia madarakani kutokana na stroke mnamo August 2008.
Mwanawasa alifarikia Paris alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nchini Misri alipohudhuria mkutano wa AU hivyo kupelekea kukodi Air Ambulance na kukimbizwa Paris, Ufaransa kwa matibabu zaidi.
Lakini baada ya wiki kadhaa za tetesi kuhusu kifo chake huko Zambia, huku maafisa wa serikali wakikanusha.
Asubuhi ya 19 August 2008 mwanafamilia wa Mwanawasa ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani, akatangaza kuwa Mwanawasa amefariki Dunia. Ilipofika jioni serikali kupitia Makamu wa Rais, Rupiah Banda wakathibitisha rasmi kifo cha Rais Levy Mwanawasa na mipango ya Mazishi ya Kitaifa ikaandaliwa.
Michael Charles Sata alikuwa Rais wa awamu ya 5 nae akawa Rais wa pili wa Zambia kufa akiwa madarakani hii ikiwa ni Oktoba 2014.
Huyu bwana alikuwa Rais wa kuonekana kwenye matukio kila uchwao ila ilipofika mwaka 2014 akaanza kuadimika katika matukio ya hadharani.
Minong’ono nchini Zambia ikaanza kuwa Rais anaumwa ndio maana haonekani hadharani kama ilivyo desturi yake. Minong’ono ikaenda mbali zaidi kuwa nchi inaongozwa na wengine kutokana na afya ya Rais kuzorota. Hii ilipingwa vikali na maafisa wa serikali yake.
Mwezi oktoba hali ikawa tete, akashindwa kuhutibia Taifa, ilipofika 19 Oktoba ikabidi akwee pipa na kwenda London, Uingereza kwaajili ya kufanya check-up ya afya yake.
Rais Michael Sata wakati anaondoka akamuachia nchi aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Edgar Lungu badala ya Makamu wa Rais.
Wengi walipigwa na bumbuwazi kutokana na safari hiyo huku Zambia ikiwa imebakiza siku tani kabla ya kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru wao na ikiashiria kuwa Rais hatokuwa sehemu ya sherehe hizo na ikatoa picha kuwa hali ya afya yake ni tete.
Jioni ya Oktoba 28 mwaka 2014 ikatangazwa Rais Michael Sata amefariki Dunia huko London alipoenda kucheki afya yake. Taratibu za mazishi ya kitaifa zikaanza kuandaliwa.
NB
Kwa katiba ya Zambia, Rais akifa madarakani, makamu wa Rais anakaimu nafasi kwa muda wa siku 90 na kuitisha uchaguzi wa kumchagua Rais mpya. Hivyo hakuna mambo ya urithi.
Pia, Marais wote wa Zambia huzikwa Embassy Park, eneo maalum la kuzikia Marais wa nchi hiyo na eneo hilo lipo jijini Lusaka.
Embassy Park ndipo walipozikwa Kenneth Kaunda, Fredrick Chiluba, Levy Mwanawasa, Michael Sata, Rupiah Banda hao wote walipata kuwa Marais wa Zambia.