Yericko Nyerere azindua Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi

Yeriko alichofanya ni kusoma vitabu vya hadithi (NOVEL) za zamani kijasusi na kuangalia MOVIE za zamani akaziunganisha pamoja habari zake na kutoa hicho kitabu chake anachokiita cha ujasusi!

Ukisoma tu utangulizi unajua alichoandika ni hekaya za miaka ile ya zamani
No offensive, lakini hii inaonyesha jinsi Tanzania tulivyo hoi! Ati nini? Yeriko katunga kitabu cha ujasusi? Tena si tu ujasusi bali ujasusi wa kidola? Na tena ujasusi wenyewe ukiwa umebobea kwenye uchumi! Hii ni kali sana sana! Ni kama sisimizi kujaribu kushusha injini ya scania lori!
 
No offensive, lakini hii inaonyesha jinsi Tanzania tulivyo hoi! Ati nini? Yeriko katunga kitabu cha ujasusi? Tena si tu ujasusi bali ujasusi wa kidola? Na tena ujasusi wenyewe ukiwa umebobea kwenye uchumi! Hii ni kali sana sana! Ni kama sisimizi kujaribu kushusha injini ya scania lori!

Acha hizo na wewe kama una uwezo tunga chako soma novel tazama moves kwa wingi njoo na maandiko sio kuponda tu.Walioandika vitabu wote walisoma vitabu vya wengine ndio wakaweza kuandika vyao.
 
Me nashangaa wabongo kweli bado tupo utumwani, leo nyerere ameandika kitabu wngne mnakidharau hata amjikisoma, ila kingeandikwa mzungu mngekisifiaaa... Achen wivu, upumbavu tuwe wazalendo tuthamin vyetu.
Huhitaji kusoma ili udharau! Kuna vitu vingine duniani inabidi usome maandishi ukutani bila kusubiri tukio. Huyu ni mganga njaa asiye na ubongo wa kuwaandikia watu wenye akili zao kitabu cha aina hiyo!
 
Acha hizo na wewe kama una uwezo tunga chako soma novel tazama moves kwa wingi njoo na maandiko sio kuponda tu.Walioandika vitabu wote walisoma vitabu vya wengine ndio wakaweza kuandika vyao.
Mkuu samahani sana! No! thank you! Kuna vitu vingine just haviwezekani! Na hili ni moja wapo! Tukiwa tunaendekeza mizaha kama hii tutachekwa vibaya sana.
 
ahahaaa hajanitafuta,
huyu jamaa muongooo....facebook yake imejaa tu uongo anaweza kuweka post kesho ni siku ya uhuru ikulu imesema....

Dah, yaani Kaboom alivyoniomba namba ananisisitizia atakutafuta kumbe hajakutafuta? Bora anirudishie namba sasa.

Yericko Nyerere ni Mjasiriamali, Gwiji la mitandao, kuna video aliwahi kuhojiwa Mlimani TV alisema yeye ameanza kutumia mitandao since 1992, ulikuwa darasa la ngapi?
 
Dah, yaani Kaboom alivyoniomba namba ananisisitizia atakutafuta kumbe hajakutafuta? Bora anirudishie namba sasa.

Yericko Nyerere ni Mjasiriamali, Gwiji la mitandao, kuna video aliwahi kuhojiwa Mlimani TV alisema yeye ameanza kutumia mitandao since 1992, ulikuwa darasa la ngapi?
mtandao gani alikuwa anatumia hyo 1992 au yahoo mail nini?
 
Jana tarehe 01/06/2015 kupitia ukurasa wake wa Fb, Twita, na Instal alitangaza rasmi kitabu hicho kuanza kuuzwa....

Mzigo upo dukani tayari kwa mauzo,

Bei ya rejareja 30,000/=

Bei ya Jumla 25,000/=

Fika Dukani House of Wisdom Bookshop lililopo Dar es Salaam, Posta, mtaa wa Samora jengo la NHC Ghorofa ya kwanza.

Kwa walio nje ya Jiji la Dar wanaweza kununua kwa M-Pesa +255755865544 Yericko Nyerere. Utaletewa mahali ulipo kwa njia ya Posta nk.

PIA KWA MAUZO YA JUMLA LIPA KUPITIA BANK YA CRDB

AC NO: 0152241955000.

Name: YERICKO YOHANESY NYERERE.

BRANCH NAME: HOLAND HOUSE

BRANCH CODE: 3319

BANK NAME: CRDB BANK PLC

SWIFT CODE: CORUTZTZ

CURRENCY: TZS.

WANAKARIBISHWA WAFANYABIASHARA WALIOTAYARI KUWEKEZA KATIKA BIASHARA HII.

Wasiliana kwa simu: +255 715 865 544


..................................................................................................................................

UTANGULIZI

Kwa kuwa ili mtu awe afisa wa idara ya Ujasusi (Intelligence officer) kwamtaka awe mwenye akili iliyotuliza (Intelligent) basi kitabu hiki maalumu kwa wasomaji weledi kiwe kama changamoto na kuonesha umuhimu na/au madhara yake kwa maisha ya wanaadamu. Kutokana na changamoto hiyo, taaluma hiyo itumike kuleta ustawi katika jamii badala ya kudhuru. Aidha kitabu hiki kinakusudiwa kutoa mwanga wa jinsi taaluma hiyo inavyopasa kuendeshwa, pamoja na kuonesha uhalisia wa utendaji wake kinyume na ilivyo kwa baadhi ya mashirika ambapo imefikia jasusi, kachero au afisa usalama kutangaza hadharani kuwa yeye ni muhusika wa shughuli hiyo ili kuwatisha watu kwa maslahi binafsi.
Kadhalika kitabu hiki ni bashraf kwa baadhi ya mataifa ya ulimwengu wa tatu kuhusiana na suala zima la ujasusi wa kimataifa unaofanywa na mashirika kama MOSSAD la Israel katika harakati zake za kutimiza dhamira ya kutawala eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla. Hivyo kitabu hiki kinatoa maarifa ya kijasusi ili kuelewa misingi ya ujasusi na umuhimu wake pamoja na kukamilisha shughuli zake mbali mbali. Mathalani kuna Ujasusi wa Ushindani (Competitive Intelligence) ambao zaidi hutumika katika ulimwengu wa biashara na harakati waweza kuainishwa kama utaratibu wa kiufundi wa kupata habari nyeti za biashara na harakati za malengo, wateja, washindani, maadui, teknolojia na mazingira ya jumla ya harakati na biashara. Habari hizi zaweza kutoka kwa mtu yeyote au vyanzo vyovyote katika eneo husika. Ujasusi unatajwa kama ni taaluma ya pili kongwe duniani; ulikuwepo tangu ulimwengu ulipopata maarifa. Mashujaa katika vita vya kale wanasema kuwa ujasusi ulikuwa sehemu muhimu ya mkakati wakati wa vita.
Kinachomuwezesha kamanda hodari kushambulia, kuteka na kufanya mambo yasiyo ya kawaida yaliyo nje ya uwezo wa kawaida ni ule ujuzi anaokuwa nao kabla ya pambano lenyewe. Na ujuzi huo anaokuwa nao kabla, hautokani na uzoefu au uhodari wa kufanya mahesabu, bali unatokana na taarifa za siri za adui ambazo hupatikana kutoka kwa watu wengine. Aidha ujasusi umekuwa sehemu muhimu ya taasisi za kijeshi na kibiashara. Ulikuwa, na hadi leo umekuwa bado ni chachu ya harakati za Kanisa Katoliki. Punde taarifa zinapopatikana, husambazwa kwa usahihi na kwa wakati kwa watoaji maamuzi wa ngazi zote. CI (Competitive Intelligence) ni ujasusi unaoshughulika zaidi na harakati za kibiashara ambao unatofautiana kidogo na ule wa serikali. Hata hivyo serikali pia inakuwa na idara ya ujasisi wa kibiashara. CI inafuata taratibu na maadili ya biashara ambayo hayafuatwi na taasisi za ujasusi unaohami serikali. CI haufanywi chini ya kinga ya kidiplomasia bali una lengo zaidi la kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuboresha huduma na kukabili mikikimikiki ya ulimwengu kwa ajili ya kujipatia faida na ufanisi wa shughuli husika. Kadhalika CI inatofautiana na ukachero mwingine wa kiserikali ambao huweza kukiuka au kupuuza sheria na taratibu za wengine.
Hii ni kusema shughuli hii, mara nyingi haitazamwi kwa wema, inaonekana kama isiyo na uhalali wa kimaadili. Kwa ajili hiyo, kitabu hiki kinatoa changamoto kwa wajuzi wa taaluma hiyo, washiriki wake na watu wa kawaida kuonesha iwapo fani ya ujasusi itafanywa kitaalamu inavyoweza kuwa ya muhimu kwa kurejea mifano ya wakongwe hasa MOSSAD, CIA (Marekani) KGB (Urusi), M16 (Uingrereza) na wengine walivyoweza kutawala uwanja huo hivyo kudhibiti kila nyanja kwa ajili ya kulinda na kuendeleza maslahi yao sehemu mbali mbali duniani.
Wataalamu wa ujasusi wa baada ya vita kuu ya pili, wametoa tafsiri nyingi kuhusiana na neno ujasusi. Hata hivyo, tafsiri ambayo pengine yaweza kukubalika na wote ni shughuli za uchunguzi wa mambo mbali mbali kwa njia za kificho; mienendo na harakati za siri za usakaji wa habari muhimu na za hakika kuhusu watu na matendo yao, yaliyo ya dhahiri na ya uficho, yanayoyafanywa dhidi ya watu wengine, serikali, jumuiya, taasisi, nchi, Taifa, kabila, biashara au maslahi ya wengine. Aidha ujasusi kitaaluma, ni ufundi wa kunasa taarifa au uwezo wa kupata taarifa nyingi kutoka vyanzo tofauti zenye kulenga kuhami, kushambulia kwa ufanisi zaidi na kuangamiza adui ni shughuli za kimya kimya (covert) zenye malengo mazuri au mabaya kwa maslahi ya mtu, kundi, jumuiya, taasisi au Serikali. Kwa tafsiri ya kiutendaji, ni ukusanyaji na uchambuzi wa ‘data’ na taarifa zinazotoka katika chanzo chochote kile (iwe kwa mtu au chombo). Taarifa zenye mtazamo wa mbali na zinazotoa taswira ya dhamira, nguvu, harakati na athari au matokeo yanayoelekea kutokea. Shughuli za kijasusi ni muhimu katika maisha ya kila siku ya ulimwengu huu wenye matukio mengi.

Upelelezi/Ushushu/Ukachero ama Ujasusi kamili, usiishie ndani ya vyombo vya Ulinzi na Usalama tu mfano Jeshi la JWTZ, Usalama wa Taifa, Polisi, Magereza na Uhamiaji tu, hata vyuo vinatakiwa kuwa na wapepelelezi, kampuni za nchini zinatakiwa kuwa na wapelelezi, mashirika ya umma yanatakiwa kuwa na wapelelezi , viwanda vya ndani vinatakiwa kuwa na wapelelezi na wote hawa wanatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa jamii ya watu wao hasa Watanzania.
Nchi zenye maendeleo makubwa zinaendelea na kuendeleza ushindani mkubwa kwenye nyanja hii, kwa mfano taifa la China lilianzisha utaratibu wa kupeleka wapelelezi nchi nyingi duniani ili walete tekinolojia na maarifa kwao, kwa sasa wana mafanikio makubwa sana.
Wakati wa vita kuu ya dunia Marekani waliiba wanasayansi wengi wa Ujerumani ambao walisaidia kujenga uwezo mkubwa wa jeshi lao na taasisi nyingine ndio maana lilikuwa taifa lenye NGUVU duniani kwa kipindi kirefu.
Tunapaswa kukumbuka kazi za ujasusi ni ngumu na zenye siri nyingi na kubwa sana, majasusi wengi pia wana mafunzo ya kujilinda , kupambana, kushambulia na KUUA. Tendo la kuua katika medani za kijasusi ni tendo la hitimisho katika misheni yoyote ikiwa kutakuwa na ulazima na halina kinga ya kisheria wala msingi wa huruma ya kitu, mhimu ni kuwa kuua huwa ni kwa maslahi ya Taifa. Kwa wale majasusi walioptia mfunzo katika nchi za Urusi na China, watakubaliana na hoja ya kuua hasa wakikumbuka hitimisho la juu kabisa la mafunzo ya ujasusi katika mpaka unaozitenganisha nchi hizo ndani ya msitu wa Zabaikalnski kwa upande wa Urusi na Manzhoul kwa upande wa China.

Ujasusi hautumiki kutafuta taarifa mbaya tu, hapana, kuna taarifa nyingine nzuri zinaweza kutumika Vyuoni, Wizarani, majeshini na sehemu nyingine kwa ajili ya kuboresha au kujenga zana na vifaa vya kisasa katika utandawazi wa dunia mpya.
View attachment 352955
Safi sna kaka ongera sna najua wapo watu hapa duniani kazi yao kukatisha tamaa watu kikubwa kukomaa tu tupo pamoja
 
Pole sana MREMBO, Mimi hukerwa mno na watu wenye ahadi mfu. Nipe Mimi namba zako hakika nitakutafuta fastar.
ahahaaa hajanitafuta,
huyu jamaa muongooo....facebook yake imejaa tu uongo anaweza kuweka post kesho ni siku ya uhuru ikulu imesema....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom