YATOKANAYO na taarifa za kamati mbili za makinikia ni kusaka fidia!

Well said Mkuu, ACACIA wao walitumia mgongo wa Makampuni ya awali yenye usajili baada ya kubadili jina hawakupata "certificate of compliance" ndio shida ilipo mkuu
OK nashukuru kwa nyongeza kuhusu mahali ulipo ukweli wa tatizo
 
Mahakama ilishatusaidia sana ila hatukuitumia humukumu hiyo vizuri.
Makahama ilshasema TAKRIMA NI RUSHWA, ilibidi tuanzie hapo kwamba viongozi wote waliongia madarakani kwa kutumia takrima (rushwa) hawana uhalali, Hii ingelifuta bunge lote la wakati huo na serikali yote ya wakati huo na hivyo tungefuta maamuzi yote na mikataba yote iliyiongiwa na serikali hiyo, na kufuta sheria zote zilipotungwa na bunge hilo la takrima.
Nadhani hatujachelewa, tufuatilie hukumu hiyo (bahati nzuri hakuna aliyeipinga). Tukishafanikiwa hilo then hata hizo kinga za ajabu ajabu na makaburi yasiyofukulika yatakufukulika - NGUMU KUMEZA!
 
Dawa si kufumua mikataba tu bali pia kufumua na katiba inayolinda maovu yote haya. Magufuri amesema katiba siyo kipaumbele chake. Kwa katiba hii hii na yeye atafanya madhambi akijua katiba inamlinda
 
Yote uliyooandika yawezekana yana uzito, sasa kama challenge kwako, twaomba uandike kwa mtiririko huo huo ya ACACIA na BARRICK kwenye machimbo yote nchini, kuanzia makosa yao na walichotakiwa kufanya na wafanye nini sasa tafadhali..
 
Mahakama ilishatusaidia sana ila hatukuitumia humukumu hiyo vizuri.
Makahama ilshasema TAKRIMA NI RUSHWA, ilibidi tuanzie hapo kwamba viongozi wote waliongia madarakani kwa kutumia takrima (rushwa) hawana uhalali, Hii ingelifuta bunge lote la wakati huo na serikali yote ya wakati huo na hivyo tungefuta maamuzi yote na mikataba yote iliyiongiwa na serikali hiyo, na kufuta sheria zote zilipotungwa na bunge hilo la takrima.
Nadhani hatujachelewa, tufuatilie hukumu hiyo (bahati nzuri hakuna aliyeipinga). Tukishafanikiwa hilo then hata hizo kinga za ajabu ajabu na makaburi yasiyofukulika yatakufukulika - NGUMU KUMEZA!
Mkuu, umeufunga uzi. Sioni kama kuna comments zaidi zitakazoleta maana kuliko hii yako. Watanzania tufike mahali tuache unafiki wa vyama, hasa CCM wakubali makosa, turekebishe tusonge mbele.
 
Yote uliyooandika yawezekana yana uzito, sasa kama challenge kwako, twaomba uandike kwa mtiririko huo huo ya ACACIA na BARRICK kwenye machimbo yote nchini, kuanzia makosa yao na walichotakiwa kufanya na wafanye nini sasa tafadhali..
Mkuu hao Barrick na ACACIA walikua na baraka za mikataba iliyosainiwa na mawaziri wetu maana nikisema mawaziri wa serikali ya CCM huwezi kunielewa. Wakosaji ni sisi watanzania tuliokua tunasainia mikataba hadi huko mahotel ya nje. Ni sisi Watanzania tuliokua tunapitisha miswada kwa hati za dharula tunaambiwa tunawafukuza wapinzani nje ya Bunge ili tupitishe vizuri tena kwa vigelegele.
 
Pamoja tunaohoji tunaitwa wasaliti lakini uhuru wetu wa kukosoa uko palepale na hapa ninautumia kikamilifu bila hata chembe ya khofu yoyote:-

1) Udhaifu mkubwa wa tathmini za kamati zote mbili ni kukadiria na dhana potofu kuwa makinikia yote kwenye makonteina kuanzia 1994 hadi leo ni sawa.

Hakuna mahakama duniani itakubaliana na ushahidi wa kuhisia. Tathmini ya hizi kamati ni porojo kwa maana ya kuwachukulia hatua wachimbaji migodi watuhumiwa kwa sababu hatuna ushahidi na hisia siyo ushahidi.

2) Acacia kukosa leseni ya biashara hata kama ni kweli lakini kusajiliwa kwenye soko la Hisa la Dar Stock Exchange kunatuweka pabaya. Pia hukumu mbali mbali za African Barrick Gold zilizotolewa hapa nchini zinathibitisha Acacia Gold mine ndiyo jina jipya badala ya African Barrick Gold. Sasa Brella au mahakama ipi maamuzi yake ni final?

Pia, kuwaruhusu kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa kwa miaka yote hii kutachukuliwa ni kampuni ilikuwa ikiendeshwa kwa jina la zamani la kampuni.

3) Taarifa hizi mbili kudhaniwa zinaweza kutumika kujadiliana ili tulipwe kodi za nyuma ambazo watumishi walioaminiwa na serikali walithibitisha takwimu zote ni sahihi. Huku ni kujitapeli wenyewe

4) Haya Makonteina yaliyokamatwa yanapaswa kuchenjuliwa ili kubaini takwimu za kweli na kuachana na makadirio ambayo hayana nafasi mbele ya vyombo vya sheria.

5) Hatua za kijinai nazo ni shughuli pevu kama tutatumia taarifa za ukadiriaji. Tukipata taarifa halisi baada ya uchenjuaji basi waliohusika kuzipika taarifa za sasa tu ndiyo wana kesi ya kujibu na wala siyo kabla ya hapo.

6) Viongozi waandamizi serikalini kuanzia mwaka 1994 hadi sasa wanaweza kuwajibishwa kwa criminal negligence kwa mikataba mibovu ambayo walishauri au hata kusaini.

7) Kama ni kweli, Acacia hawajasajiliwa uongozi mzima wa BOT, Brella, TRA, TMMA na Dar Stock Exchange unapaswa kuondolewa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

8) Waliojilimbikizia mali wana kesi ya kujibu watueleze walizipataje?

9) Viongozi wa vyombo vya usalama waliofumbia macho haya madudu nao wajumuishwe kwenye uwajibikaji wa kijinai au criminal negligence

10) Kuwatisha wananchi kukosoa hatua za serikali huo ndiyo uzandiki na wakosoaji ndiyo wazalendo namba moja.

11) Taarifa hizi zina msaada kwa kesho yetu na siyo jana yetu

12) Mawaziri wa zamani walikuwa wakitekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo kuwatoa mhanga wao tu mahakama zitakataa

14) Hoja ya kudai tumeibiwa huku tumejiibia khalafu tudai fidia kwa tuhuma za wizi tulioshiriki kuufanya sisi wenyewe ni kujitapeli wenyewe.

Haiwezekani tupande mbigiri kesho tudai kuvuna shayiri kwa minajili ipi?

15) Kama jina la Acacia halijasajiliwa basi mmiliki halali wa migodi husika anabaki msajiliwa wa awali African Barrick Gold kwa hiyo khoja za yakuwa migodi haina mwenyewe ni njozi za abunuwasi.

16) Tatizo kubwa la huu utawala ni kuwatafuta wachawi bali siyo kujenga misingi ya utawala wa kisheria.

Yakija mambo ya maana na weledi kama kuboresha katiba hudai hawakukampeni kwenye hilo lakini ikija kwenye kufukazana na ngozi baada ya mnofu kuliwa utashangaa bila tone la aibu hujitokeza kimasomaso ati nao ni watetezi wa mustakabali wa taifa hili!

Give us a break, man! They either put up or shut up!

17) CCM wawe wa kweli haya makampuni ndiyo wafadhili wao wakubwa wa chaguzi kuanzia 1995-2015. Huwezi ukavuna ambacho hujapanda! Tumepanda dhuluma sasa tunaivuna hiyo dhuluma.

18) Uvunjaji wa seals za makonteina bila search warrant au amri ya msuluhishi ni kuvuruga ushahidi na hili kuisaidia sana Acacia.

19) Kutafuta usuluhishi kinyume na masharti ya mkataba kwa maana ya msuluhishi ni ukiukwaji wa mkataba na madhara yake ni kazi za kamati zote mbili ni batili machoni pa vyombo vya utoaji wa haki.

Ni sawa kabisa na kutwanga maji kwenye kinu na kutegemea upate makande yaliyoiva!

Mkuu huwezi kueleweka kwa sasa watu washalishwa limbwata kuwa tunaibiwa wameziba masikio wanapiga kulele tuuu kwa sasa wakitulia watakuelewa ila itakuwa baadae sana....
 
Back
Top Bottom