Yanga na katibu mpya Mkenya

Wanachama wa yanga wamemkataa rasmi katibu toka kenya maana ni aibu nchi ya watu zaidi ya milion 40 wenye kila aina ya ujuzi halafu wanataka leta mgeni.maana yake ni nini?

Mkuu naback up tu maneno yako kutoka kwa Bin Zubeiry.

[h=3]KIMENUKA YANGA SC, WANACHAMA WALIANZISHA KUPINGA MABADILIKO YA SEKRETARIETI[/h]
Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013 SAA 3:42 USIKU
KITENDO cha uongozi wa Yanga kufanya mabadiliko ya sekretarieti ya klabu kimezua tafrani kubwa- na pamoja na wanachama kupinga, lakini pia kimeingilia mchezo wa kirafiki uliokuwa ufanyike Jumamosi kati ya klabu hiyo na Tusker ya Kenya.
Kiongozi ameng'oka; Mwalusako katikati akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro kulia na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, wadhamini wakuu wa Yanga, George Kavishe

Yanga imemuengua Katibu Lawrence Mwalusako na kuajiri Mtendaji Mkenya, Patrick Naggi na wanachama wa klabu hiyo wamepinga vikali hatua hiyo na kesho wamepanga kukutana na Waandishi wa Habari kuelezea msimamo wao.
Lakini pia, mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Tusker ya Kenya ulioandaliwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) hautakuwepo tena kwa sababu haijulikani nani ataidhinisha mechi hiyo baada ya mabadiliko haya na vurugu zinazoendelea.
Bosi mpya; Naggi ana uzoefu wa kuongoza soka Kenya, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ligi Kuu Kenya, FKL.
Sasa DRFA imeamua kufuta kabisa ziara ya Tusker nchini ambayo ilikuwa pia icheze na Simba SC jumapili.
Mwalusako wa pili kushoto, kabla ya kuwa kiongozi aliichezea klabu hiyo na ni kipenzi cha wanachama wa Yanga SC.
 
Tuanataka klabu iendeshwe kisasa siyo kwa kukariri.Hii ni klabu kubwa siyo kama mnyama wa kupakatwa......
 
Mkuu naback up tu maneno yako kutoka kwa Bin Zubeiry.

KIMENUKA YANGA SC, WANACHAMA WALIANZISHA KUPINGA MABADILIKO YA SEKRETARIETI

Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013 SAA 3:42 USIKU
KITENDO cha uongozi wa Yanga kufanya mabadiliko ya sekretarieti ya klabu kimezua tafrani kubwa- na pamoja na wanachama kupinga, lakini pia kimeingilia mchezo wa kirafiki uliokuwa ufanyike Jumamosi kati ya klabu hiyo na Tusker ya Kenya.

Kiongozi ameng'oka; Mwalusako katikati akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro kulia na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, wadhamini wakuu wa Yanga, George Kavishe

Yanga imemuengua Katibu Lawrence Mwalusako na kuajiri Mtendaji Mkenya, Patrick Naggi na wanachama wa klabu hiyo wamepinga vikali hatua hiyo na kesho wamepanga kukutana na Waandishi wa Habari kuelezea msimamo wao.
Lakini pia, mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Tusker ya Kenya ulioandaliwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) hautakuwepo tena kwa sababu haijulikani nani ataidhinisha mechi hiyo baada ya mabadiliko haya na vurugu zinazoendelea.

Bosi mpya; Naggi ana uzoefu wa kuongoza soka Kenya, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ligi Kuu Kenya, FKL.
Sasa DRFA imeamua kufuta kabisa ziara ya Tusker nchini ambayo ilikuwa pia icheze na Simba SC jumapili.

Mwalusako wa pili kushoto, kabla ya kuwa kiongozi aliichezea klabu hiyo na ni kipenzi cha wanachama wa Yanga SC.

Nafikiri wa pili kulia au???
 
Vita ya panzi............... Huo ndio utakua mwanzo wa yanga kuacha ubingwa mapemaa. Historia inaonyesha timu hizi kubwa hapa TZ (Yanga na Simba) zikiwa ktk migogoro huboronga kwenye mechi zao. Hivyo nafurahi sana kusikiatayari zengwe lina fukuta ndani ya club ya yanga najua ndio wakati wa Azam kuwa bingwa. Endeleeni kulumbana ikibidi mpaka kocha mtimueni.
 
Nafikiri wa pili kulia au???

Kweli ni wa pili kutoka kulia, mimi nilikopi na kupesiti tu; lakini kwa hili mimi nawaunga mkono wanayanga, haiwezekani mashabiki zaidi ya milioni kumi na wanachama kibao akose mtu makini wa kuwa katibu wa timu hadi aje mkenya na mhasibu mhindi(huenda katoka India huyu), wanshindwa kumchukua hata ndugu yangu Makoye Matale au Mandieta au wewe mwenyewe Ulimakafu, au mwalimu gfsowin(sijui nimepatia jina)
 
Tatizo wabongo uaminifu ni zero
wakenya na wahindi ndio waaminifu? mara mia aibe mbongo pesa ya bongo kuliko kutoka nje maana mbongo unaweza nufaika naye kama si wewe ndugu yako ama rafiki yako
 
Wanachama wa yanga wamemkataa rasmi katibu toka kenya maana ni aibu nchi ya watu zaidi ya milion 40 wenye kila aina ya ujuzi halafu wanataka leta mgeni.maana yake ni nini?
Kwa uelewa mdogo ni kuwa kwa sasa soka sio tena la Ridhaa ni la kulipwa na nasikia huyo Mkenya amelikuwa CEO wa Kenya Premier League kwa hali ya mambo yanavyoenda sasa Tanzania kuhusu kuandaa klabu inayotaka kuwa na umiliki wa wanachama ni lazima kuwe na mtendaji aliesomea na kuyafanyia kazi kwa maana ya uzoefu wa uendeshaji wa klabu ya mpira wa miguu kwa yeye kama alifanya Kenya na ana sifa sidhani kama kuna tatizo na hiyo ni hatua kubwa kwa Yanga kuelekea kwenye mafanikio angalia AzamFc wanajiendesha kwa kuwa kuna watu wanaoelewa fedha zitarudi vipi na ndio maana hata Rais alisema Yanga na Simba mbadilike muwe kama AzamFc ndio haya sasa yanayotokea Mwenyekiti anaonyesha njia wengine wanasema sijui tunaonekana hatuwezi, Wahenga walisema mjinga ni kujifanya unajua huku hujui kitu sasa kuna mikataba ya Azam Media Ltd,Vodacom Tanzania,TBL na nk hivi bila ya kuwa na Katibu Mkuu ambae ndio mfuatiliaji wa hayo mambo Bodi ya Yanga nani atailetea Taarifa za mwezi,mwaka nk za maendeleo ya klabu ? Maana Mkiti,M/kiti na wajumbe ni watu wenye kazi zao sio kwamba wanalipwa kwa kazi za Yanga ni kujitolea sasa wameona mbali tulete mwenye uelewa atuelimishe ili miaka ijayo tukae wenyewe tunaanza kulalamika,Kenya wameanza kutoa mafunzo ya usimamizi wa klabu za mpira kwenye chuo kimojawapo Nairobi kupitia Super Sport ya SA,sasa uliza kama kuna timu yoyote ya Tanzania kama imepeleka mtendaji wake akasomee ili aje kuiendelez
a klabu yao huku kwetu kama utasikia ila kulalamika tuko mbele,Leo Uingereza wameanza kuunda kamati ya kuchunguza kwanini timu zao za Premier League zina wageni wengi kuliko wazawa na wanaweka uwiano wa wageni kwenye vilabu vyao sisi tunaweka uwiano bila kuzipa nguvu mashindano ya timu za watoto,maana kila kwenye mechi ya Vodacom Premier League kuna timu za watoto wa klabu husika zinaanza kucheza sasa hawana hata mdhamini na sijawahi kusikia bingwa wa timu za watoto zaidi ya mashindano ya kombe la BancABC,Tutafakari tuchukue hatua !

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Yanga inatarajia kuleta katibu mpya mkenya.mimi binafsi siungi mkono hapa makamu mwenyekiti clement sanga umechemka na unaendeleza sera ya kutukuza wageni. Hapo kwanza tayari tunapunguza ajira ya mtanzania na pia tunaendeleza ile dhana kuwa wakenya wanaweza kuliko sisi
Pia huyo katibu mpya sio mwanachama wa yanga(hana kadi)
Katibu mwenyewe anashutuma kibao za uwizi alipokuwa kiongozi chama cha mpira wa kenya
Kocha Ernst Brandts kadi yake namba ngapi?
 
Nauliza Kama Kuwa na card ya uanachama Ndio Tatizo je Coach Ernist Brandt Alikuwa nayo? Razak siwa je? Hii ni nafasi ya ajira si ya kupendekezwa au kuchaguliwa Hawa wazee imefika mahali watulie waache timu ziendeshwe kifaida sio kila kitu Mpaka watake wao. Zinadine zidane ni Mfaransa kweni Real Madrid hawana waspaniola wenzao Mpaka technical director atoke ufaransa manager awe mtaliano? Haya Ndio matatizo yetu kuhendekeza njaa Akilimali na akiliufukara
 
Yanga inatarajia kuleta katibu mpya mkenya.mimi binafsi siungi mkono hapa makamu mwenyekiti clement sanga umechemka na unaendeleza sera ya kutukuza wageni. Hapo kwanza tayari tunapunguza ajira ya mtanzania na pia tunaendeleza ile dhana kuwa wakenya wanaweza kuliko sisi
Pia huyo katibu mpya sio mwanachama wa yanga(hana kadi)
Katibu mwenyewe anashutuma kibao za uwizi alipokuwa kiongozi chama cha mpira wa kenya
wewe unashangaa hilo, sisi wenzako tumefikia hatua ya kutaka raisi wa nchi atakayetawala kuanzima mwaka 2015 awe mwingereza au mjerumani au mmarekani , tuone atatusaidiaje kuweka katiba ya wananchi na kutujengea uchumi baada ya wazarendo kushindwa kujenga uchumi kwa miaka 51 ya uhuru. tone kama pesa za mabilion ya uswiss zitarudi hapa nchi!
 
ndugu yangu kenyans wapo mbali sana katika uzalendo wa kujenga uchumi kuliko sisi. sisi tupo mbali sana kupita nchi zote africa kwa kujenga na kuimalisha chama. kumbuka miaka ya sabini mwanzoni walivyokuwa wajanja kenyans kwa kuitangaza dawa ya aspro na kipindi chao cha kweli na aspro. tazama jinsi walivyitangaza sabuni ya ommo katika TV na kipindi chao cha ommo. halafu tazama jinsi walivyo opoa matajiri wengi wa ulaya kuinvest Kenya. sasa njoo kwetu sisi na uone kama tuna bidhaa gani za viwanda tuliwahi kuzitangaza africa mashariki au nje ya mipaka.

Ila kama wao wanataka waimba kwaya za kusifia chama, mgambo na makada wa kueneza propaganda sisi tupo tayari kumwaga watanzania kenya. Yanga imehangaika sana kisoka hapa africa tangia iolipotibuliwa misingi yake bora ya kuwa wakali wa soka mwaka 1975. Yanga ina umri wa miaka 75 lakini haina maendeleo ya kutisha kisoka hivyo katika kutafuta vichwa vya mawazo , hatua yao ya kumleta Mkenya inaungwa mkono. wewe kaaa pembeni uje kusherehekea ubingwa wa africa mwaka 2014!
 
yanga inatarajia kuleta katibu mpya mkenya.mimi binafsi siungi mkono hapa makamu mwenyekiti clement sanga umechemka na unaendeleza sera ya kutukuza wageni. Hapo kwanza tayari tunapunguza ajira ya mtanzania na pia tunaendeleza ile dhana kuwa wakenya wanaweza kuliko sisi
pia huyo katibu mpya sio mwanachama wa yanga(hana kadi)
katibu mwenyewe anashutuma kibao za uwizi alipokuwa kiongozi chama cha mpira wa kenya
umeshahesabu tuuma za wizi za mwenyekiti wako?
  1. kagoda/epa
  2. tanesco
  3. uda
  4. nssf & ppf
  5. meremeta
  6. ubungo godowns
  7. salamander building
  8. bakwata shell deal(temeke plot)
  9. dowans.............zote ni tuhuma mkuu hazijathibitishwa
 
Kweli ni wa pili kutoka kulia, mimi nilikopi na kupesiti tu; lakini kwa hili mimi nawaunga mkono wanayanga, haiwezekani mashabiki zaidi ya milioni kumi na wanachama kibao akose mtu makini wa kuwa katibu wa timu hadi aje mkenya na mhasibu mhindi(huenda katoka India huyu), wanshindwa kumchukua hata ndugu yangu Makoye Matale au Mandieta au wewe mwenyewe Ulimakafu, au mwalimu gfsowin(sijui nimepatia jina)

Kwa akili matope kama hizi basi soka la Tz lina safari ndefu bado. Wengi wa waswahili wanajidai kufuatilia soka la ulaya bila kuelewa mfumo unaotumiwa na vilabu vya huko. Hakuna kitu nakichukia kwenye mfumo wa vilabu vyetu kama kamati ya wazee wa klabu. Hawa hujiona daima kuwa wanalifahamu soka vizuri kuliko viongozi wa vilabu. Hutaka wawe na maamuzi ya mwisho vilabuni. Hata kama angeletwa David Levy kusimamia vilabu, angejikuta akilazimika kupokea orders kutoa kwa waharibifu hawa. Katika ulimwengu ambao soka ni sayansi, ni aibu kubwa kuwa na mtazamo kama huu wa wazee hawa. Management ya timu ni zaidi ya upenzi. Wangefanya hivi Azam FC wasingekuwa na tatizo kwa vile wana mfumo wa soka la kisasa. Ingeonekana ni hatua kuelekea soka la kisasa.

Tubadilike ndugu zangu. Nina uhakika hakuna mwanachama hata mmoja wa Yanga aliye na uzoefu wa mfumo wa soka unaotumika na vilabu vilivyopiga hatua barani Afrika na ulaya. Wooote wanaelewa soka la fitna za kibingo bongo ambalo limeprove failure. Tunataka management ya kisayansi na si kikundi cha opportunists wanaoamini katika ndoto za alinacha.

Thanks.
 
Mkuu - hiyo management ya kisayansi inawezekana tu kama vilabu vitakuwa ni makampuni na wenye hisa wanajulikana. Kwa mfumo wa vilabu vyetu ni kazi kubwa. Maana ni vilabu na vina katiba. Ingekuwa ni kampuni sauti ya maamuzi inatokana na ukubwa wa hisa. kwa kifupi vilabu ni mali za watu kama mali zingine. Washabiki wanabakia kuwa washabiki lakini wenye hisa kwa kiasi fulani wanaweza kuzingatia matakwa yao lakini si lazima!!

Mimi nina wasiwasi sana kuhusu uwanja katika mfumo huu tulionao. Kutoka mfumo huu kwenda ule wa kibiashara kwa sasa haikwepeki. Lakini akina Akilimali watakubali? Wanachama wengine wenye njaa zao watakubali?
 
Hawa ndiyo hatari zaidi kuliko. Huwa sielewi majukumu yao katika soka la kisasa. Hata hivyo uongozi unafanya mabadiliko taratibu, ili kupata watu watakaoendana na mfumo wa kisasa. Haiwezekani kutia divai mpya kwenye viriba vikuu kuu. Vitapasuka tu. Ndio maana nasema huwezi kutumia wanachama waliolelewa katika mmfumo wa Simba na Yanga kuleta mabadiliko ya kweli. Ni ngumu mno kwani ni sawa na kipofu kumwongoza kipofu.
 
Back
Top Bottom