Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 8,787
- 15,513
Wajuzi wa masuala ya kimataifa. Nigeria wanachagua Rais tarehe 25 mwezi huu wa pili. Nini kinaendelea huko? Nani anauwezekano mkubwa wa kushinda?
=======
Siku ya Jumamosi, tarehe 25 Februari 2023, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika itapiga kura kumchagua rais wao ajaye, Makamu wa Rais pamoja na wajumbe wa bunge la kitaifa. Uchaguzi wa Ugavana na Mabunge ya Majimbo utafanyika Machi 11, 2023.
Wengi wa wanaowania urais ni wakongwe wa kisiasa ambao wamekuwa kwenye siasa kwa miaka mingi. Je, yeyote kati ya wagombea wa urais ataweza kurejesha ndoto ya Nigeria?
Mamia ya Wanigeria walionyesha nia yao ya kugombea nafasi hiyo ya juu zaidi nchini humo, hata hivyo, ni wagombea kumi na wanane (18) tu walioidhinishwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC).
Hii si mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Nigeria kukumbwa na kinyang'anyiro hicho cha watu wengi, katika uchaguzi wa urais wa 2019 ulijumuisha idadi kubwa zaidi ya wagombea katika historia ya Nigeria. Vyama 73 kati ya 91 vilivyosajiliwa wakati huo, viliwasilisha wagombea katika uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi, Februari 16, 2019.
2. Al-Mustapha Hamza – Action Alliance (AA)
3. Sowore Omoyele – African Action Congress (AAC)
4. Kachikwu Dumebi – African Democratic Congress (ADC)
5. Sani Yabagi Yusuf – Action Democratic Party (ADP)
6. Tinubu Bola Ahmed – All Progressives Congress (APC)
7. Umeadi Peter Nnanna – All Progressives Grand Alliance (APGA)
8. Ojei Princess Chichi – Allied People’s Movement (APM)
9. Nnamdi Charles Osita – Action Peoples Party (APP)
10. Adenuga Sunday Oluwafemi – Boot Party (BP)
11. Obi Peter Gregory – Labour Party (LP)
12. Musa Rabiu Kwankwaso – New Nigeria Peoples Party (NNPP)
13. Osakwe Felix Johnson – National Rescue Movement (NRM)
14. Abubakar Atiku – Peoples Democratic Party (PDP)
15. Abiola Latifu Kolawole – Peoples Redemption Party (PRP)
16. Adebayo Adewole Ebenezer – Social Democratic Party (SDP)
17. Ado-Ibrahim Abdumalik – Young Progressives Party (YPP)
18. Nwanyanwu Daniel Daberechukwu – Zenith Labour Party (ZLP)
Mwanamke mmoja tu kwenye kinyang'anyiro
Kuna mgombea mmoja tu wa urais ambaye ni mwanamke kati ya wagombea 18. Ojei Princess Chichi wa chama cha Allied People’s Movement (APM). Chichi ambaye ana umri wa miaka 44 anatokea katika Jimbo la Delta na aliibuka mara ya kwanza kama mgombea wa kiti cha umakamu wa rais na baadaye kuwa mgombea urais wa Allied Peoples' Movement (APM) baada ya mwenyekiti wa chama hicho, Yusuf Mamman Dantalle kujiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Wanaotazamiwa zaidi kuibuka kidedea
Ikiwa kuna jumla ya wagombea 18 wanaowania kiti cha urais, mchuano mkubwa ni kati ya Bola Tinubu kutoka chama tawala cha All Progressives Congress (APC), Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP) na Peter Obi wa chama cha Labour, ambaye anaongoza katika baadhi ya kura.
Kutokea kushoto: Bola Tinubu, Atiku Abubakar na Peter ObiKura za Maoni
Katika kura za maoni za hivi karibuni zilizofanywa na mashirika mawili; ANAP na Kwakol Research, mgombea urais wa Nigeria Peter Obi aliibuka kama mgombea anayependwa zaidi kumrithi Rais Muhammadu Buhari.
Katika utafiti wa Premise Data Corp. uliotolewa hivi karibuni, 66% ya washiriki ambao waliosema wameamua jinsi ya kupiga kura walimchagua Obi wa Chama cha Labour badala ya Bola Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress na Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party.
Kura nyingine ya maoni iliyofanywa na shirika la SBM Intelligence lenye makao yake mjini Lagos haioni inaeleza kwamba Obi na Abubakar wanaweza kupata idadi ya kutosha kufikia 25% ya kura katika majimbo 24 kati ya 36 ya Nigeria.
Utabiri huo ni tofauti na ule wa Political Africa Initiative (POLAF) ambao uchunguzi wake uliwahoji watu milioni tatu na kutabiri mchuano wa karibu kati ya chama cha upinzani cha PDP (38%) na chama tawala cha APC (29%).
Wananchi 93,469,008 wamesajiliwa kupiga kura
Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC)imeeleza kuwa wapiga kura 44,414,846 waliojiandikisha ni wanawake na 49,054,162 ni wanaume.
Wakati huo huo, kati ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha, idadi ya vijana kati ya 18 na 34 imefikia 37,060,399, ikiwa ni asilimia 39.65 ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha. Wazee kati ya umri wa miaka 50 na 69 wamefikia 17,700,270, wakiwakilisha 18.94% ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha.
Upigaji kura umeanza saa 2:30 asubuhi katika vituo vya kupigia kura kote nchini Nigeria, na utamalizika saa 8:30 mchana, lakini yeyote ambaye tayari ameidhinishwa na yuko kwenye mstari wa kupiga kura bado ataruhusiwa kufanya hivyo.
Wakazi wa mji wa Kwankwaso katika jimbo la Kano wakiwa katika vituo vya kupigia kura.
4:45 Asubuhi: Tinubu azungumza baada ya kupiga kura yake
Mgombea urais wa chama cha All Progressives Congress Asiwaju Bola Ahmed Tinubu amezungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura yake. Tinubu ameelezea mchakato huo kuwa unaendelea vizuri huku akionesha matumaini juu ya idadi kubwa ya wapiga kura kujitokeza.
4:34 Asubuhi: Makamu wa Rais Osibanjo na mkewe wapiga kura katika Jimbo la Ogun
Makamu wa Rais wa Nigeria Prof. Yemi Osibanjo na mkewe wamepiga kura katika kituo cha 14 cha Ikenne, Jimbo la Ogun. Makamu wa Rais ni wa Chama cha All Progressives Congress ambacho mgombea wake wa urais ni Bola Ahmed Tinubu.
4:03 Asubuhi: Rais Muhammadu Buhari apiga kura katika Jimbo la Kastina, asema ana imani wagombea wa APC watashinda
Rais Muhammadu Buhari amepiga kura katika kituo chake cha PU 003 katika kata ya Sarkin Yara A, huko Daura, Katsina. Rais Buhari amekaa madarakani kwa miaka 8 na atakabidhi kwa serikali mpya Mei 29, 2023.
Rais Buhari amesema ana imani kuwa wagombea wa chama cha All Progressives Congress (APC) wataibuka washindi katika uchaguzi mkuu wa leo Februari 25 na Machi 11.
Akizungumza kwa Kiingereza na Kihausa, alisema: "Nimefurahishwa sana na mchakato wa uchaguzi. Nimefurahishwa na idadi ya wapiga kura."
3:15 Asubuhi: Peter Obi anafika kitengo cha kupigia kura
Mgombea urais wa Chama cha Labour, Peter Obi, amefika katika kituo chake cha kupigia kura cha PU 019, Umudimakasi Square, Agulu, Jimbo la Anambra. Ameonesha matumaini yake ya ushindi huku pia akisema hatafuti nafasi katika baraza la mawaziri la wapinzani wake.
3:11 Asubuhi: Mgombea urais wa PDP Atiku Abubakar anapiga kura Adamawa
Aliyekuwa Makamu wa Rais na mgombea urais wa Chama cha People's Democratic Party amepiga kura yake katika kituo chake cha kupigia kura huko Ajiya 02, katika Wadi ya Gwadabawa, Serikali ya Mtaa ya Yola Kaskazini ya Jimbo la Adamawa.
3:04 Asubuhi: Usalama waimarishwa maeneo mbalimbali ya Lagos
Wanajeshi wameweka vizuizi katika maeneo tofauti ya jimbo la Lagos katika kutekeleza operesheni inayolenga kuhakikisha utulivu wakati wa uchaguzi wa 2023.
Wanajeshi wakiimarisha usalama jijini Lagos
Shambulizi kwa timu za ufuatiliaji wa uchaguzi
Timu za ufuatiliaji wa uchaguzi za Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha, EFCC, zimeshambuliwa leo Jumamosi, Februari 25, 2023 huko Abuja na Jimbo la Imo.
Shambulio hilo lilifuatia kukamatwa kwa mwanamume mmoja kwa madai ya kupanga utaratibu wa ununuzi wa kura katika kituo cha kupigia kura katika Shule ya Msingi ya Sayansi, Bwari.
Msemaji wa EFCC Wilson Uwujaren amesema wahudumu walimkamata mwanamume wa makamo na kupata orodha ya wanufaika ambao tayari aliwalipa pesa kupitia benki.
Tume ya Uchaguzi yatuhumiwa kutokuwa na uwazi katika matokeo
Vyama vya Upinzani vya PDP na Labor Party vimesusia mchakato wa Utangazaji Matokeo kwa madai kuwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) imeonesha kuwepo kwa uchakachuaji wa Matokeo yanayoendelea kutolewa.
Hadi sasa ni takriban Theluthi Moja ya Kura za Majimbo 36 zimetangazwa ambapo kwa mujibu wa BBC Mgombea wa Chama Tawala (APC), #BolaTinubu ana 47% ya Kura zilizopigwa, Kiongozi wa Upinzani, #AtikuAbubakar 27%, na #PeterObi ana 22%.
Hata hivyo, Matokeo yanayoendelea kutoka kwenye maeneo ya Kaskazini na Kusini-Mashariki mwa Nigeria yanaonekana kuwa ngome za PDP na Labour Party na kufanya Matokeo ya mwisho kutotabirika.
Rais Mstaafu Obasanjo aitaka Tume ya Uchaguzi kuepusha hatari ya machafuko
Rais wa zamani Olusegun Obasanjo ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko yanayoendelea kuibuka kuhusu kutokuwepo uwazi kwenye Matokeo ya Kura zilizopigwa ikiwa ni pamoja na Tume kusoma Matokeo ya Kura ya mkononi badala ya Tovuti ya Tume.
Obasanjo amemtaka Rais #MuhammaduBuhari kufahamu kuwa kuna dalili za kuibuka Vurugu za Uchaguzi na kushauri Matokeo yote ambayo hayajakidhi Vigezo na yasiyokuwana Uwazi yafutwe mara moja
Aidha, Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wamesema Mchakato wa Utangazaji Matokeo umekosa Uwazi kutokana na Tume ya Uchaguzi (INEC) kutumia Matokeo yaliyokusanywa kwa Mikono badala ya yanayotakiwa kuwa kwenye Tovuti ya Tume.
Wanahabari wakamatwa, kushambuliwa au kunyanyaswa wakiripoti uchaguzi
Takriban wanahabari 14 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wamezuiliwa, kunyanyaswa, au kushambuliwa wakati wakiripoti uchaguzi mkuu wa Nigeria, akiwemo mmiliki wa tovuti binafsi ya habari ya WikkiTimes Haruna Mohammed Salisu, ambaye bado anashikiliwa na polisi bila kufunguliwa mashtaka.
Inaelezwa kuwa Polisi walimshikilia Salisu mnamo Februari 25 katika mji wa Duguri, kusini-mashariki mwa jimbo la Bauchi, muda mfupi baada ya yeye na waandishi wengine kukutana na gavana wa jimbo hilo, kwa mujibu wa mhariri wa WikkiTimes Yakubu Mohammed, ambaye alizungumza na CPJ.
Kwa mujibu wa Mohammed, ambaye alimtembelea Salisu baada ya kuhamishiwa makao makuu ya polisi huko Bauchi, Polisi walisema walimkamata ili kumlinda baada ya wafuasi wa gavana huyo kumvamia alipokuwa akiwahoji wanawake wa eneo hilo waliokuwa wakiandamana, lakini wakakataa kumwachilia.
Raia, vikundi vya kisiasa, na vikosi vya usalama vilitishia, kushambulia, au kukamata angalau waandishi wengine 13 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi. Hii ni kwa mujibu wa CPJ.
05: 30 BOLA TUNUBU AONGOZA KWA TOFAUTI KUBWA
Bola Tinubu kutoka chama tawala cha Nigeria amechukua nafasi thabiti ya uongozi katika matokeo yaliyotolewa mpaka sasa akiwa na 36% ya kura zote huku wapinzani wake, makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar akiwa na 29% na Peter Obi ana 25% ya kura zote zilizohesabiwa.
Vyama vya Atiku na Obi vimeitisha uchaguzi huo ufutwe na ufanyike upya wakiituhumu tume ya uchaguzi kushindwa kuweka matokeo kwenye tovuti yake kuonesha ulivyochezewa.
Anayewania Urais anahitaji kupata kura nyingi zaidi kitaifa na angalau robo ya kura zote katika majimbo 25 kati ya 36 ikiwemo Abuja ili aweze kutangazwa mshindi. Kama mgombea atashindwa kufikia vigezo hivyo, uchaguzi unarudiwa kwa wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi.
06:30 BOLA TINUBU ATANGAZWA MSHINDI
Tume ya uchaguzi ya Nigeria imemtangaza Bola Tinubu kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa Nigeria. Tinubu ametangazwa katika tafrija fupi ambapo wapinzani wake wakuu wawili wamekacha kuhudhuria.
Gavana huyo wa zamani wa jiji la Lagos amekusanya kura milioni 8.79 dhidi ya Atiku(milioni 6.9) na Pete Obi(milioni 6.1)
=======
Siku ya Jumamosi, tarehe 25 Februari 2023, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika itapiga kura kumchagua rais wao ajaye, Makamu wa Rais pamoja na wajumbe wa bunge la kitaifa. Uchaguzi wa Ugavana na Mabunge ya Majimbo utafanyika Machi 11, 2023.
Wengi wa wanaowania urais ni wakongwe wa kisiasa ambao wamekuwa kwenye siasa kwa miaka mingi. Je, yeyote kati ya wagombea wa urais ataweza kurejesha ndoto ya Nigeria?
Mamia ya Wanigeria walionyesha nia yao ya kugombea nafasi hiyo ya juu zaidi nchini humo, hata hivyo, ni wagombea kumi na wanane (18) tu walioidhinishwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC).
Hii si mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Nigeria kukumbwa na kinyang'anyiro hicho cha watu wengi, katika uchaguzi wa urais wa 2019 ulijumuisha idadi kubwa zaidi ya wagombea katika historia ya Nigeria. Vyama 73 kati ya 91 vilivyosajiliwa wakati huo, viliwasilisha wagombea katika uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi, Februari 16, 2019.
Orodha ya wagombea Urais nchini Nigeria 2023
1. Imumolen Christopher – Accord Party (AP)2. Al-Mustapha Hamza – Action Alliance (AA)
3. Sowore Omoyele – African Action Congress (AAC)
4. Kachikwu Dumebi – African Democratic Congress (ADC)
5. Sani Yabagi Yusuf – Action Democratic Party (ADP)
6. Tinubu Bola Ahmed – All Progressives Congress (APC)
7. Umeadi Peter Nnanna – All Progressives Grand Alliance (APGA)
8. Ojei Princess Chichi – Allied People’s Movement (APM)
9. Nnamdi Charles Osita – Action Peoples Party (APP)
10. Adenuga Sunday Oluwafemi – Boot Party (BP)
11. Obi Peter Gregory – Labour Party (LP)
12. Musa Rabiu Kwankwaso – New Nigeria Peoples Party (NNPP)
13. Osakwe Felix Johnson – National Rescue Movement (NRM)
14. Abubakar Atiku – Peoples Democratic Party (PDP)
15. Abiola Latifu Kolawole – Peoples Redemption Party (PRP)
16. Adebayo Adewole Ebenezer – Social Democratic Party (SDP)
17. Ado-Ibrahim Abdumalik – Young Progressives Party (YPP)
18. Nwanyanwu Daniel Daberechukwu – Zenith Labour Party (ZLP)
Mwanamke mmoja tu kwenye kinyang'anyiro
Kuna mgombea mmoja tu wa urais ambaye ni mwanamke kati ya wagombea 18. Ojei Princess Chichi wa chama cha Allied People’s Movement (APM). Chichi ambaye ana umri wa miaka 44 anatokea katika Jimbo la Delta na aliibuka mara ya kwanza kama mgombea wa kiti cha umakamu wa rais na baadaye kuwa mgombea urais wa Allied Peoples' Movement (APM) baada ya mwenyekiti wa chama hicho, Yusuf Mamman Dantalle kujiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Wanaotazamiwa zaidi kuibuka kidedea
Ikiwa kuna jumla ya wagombea 18 wanaowania kiti cha urais, mchuano mkubwa ni kati ya Bola Tinubu kutoka chama tawala cha All Progressives Congress (APC), Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP) na Peter Obi wa chama cha Labour, ambaye anaongoza katika baadhi ya kura.
Kutokea kushoto: Bola Tinubu, Atiku Abubakar na Peter Obi
Katika kura za maoni za hivi karibuni zilizofanywa na mashirika mawili; ANAP na Kwakol Research, mgombea urais wa Nigeria Peter Obi aliibuka kama mgombea anayependwa zaidi kumrithi Rais Muhammadu Buhari.
Katika utafiti wa Premise Data Corp. uliotolewa hivi karibuni, 66% ya washiriki ambao waliosema wameamua jinsi ya kupiga kura walimchagua Obi wa Chama cha Labour badala ya Bola Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress na Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party.
Kura nyingine ya maoni iliyofanywa na shirika la SBM Intelligence lenye makao yake mjini Lagos haioni inaeleza kwamba Obi na Abubakar wanaweza kupata idadi ya kutosha kufikia 25% ya kura katika majimbo 24 kati ya 36 ya Nigeria.
Utabiri huo ni tofauti na ule wa Political Africa Initiative (POLAF) ambao uchunguzi wake uliwahoji watu milioni tatu na kutabiri mchuano wa karibu kati ya chama cha upinzani cha PDP (38%) na chama tawala cha APC (29%).
Wananchi 93,469,008 wamesajiliwa kupiga kura
Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Nigeria (INEC)imeeleza kuwa wapiga kura 44,414,846 waliojiandikisha ni wanawake na 49,054,162 ni wanaume.
Wakati huo huo, kati ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha, idadi ya vijana kati ya 18 na 34 imefikia 37,060,399, ikiwa ni asilimia 39.65 ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha. Wazee kati ya umri wa miaka 50 na 69 wamefikia 17,700,270, wakiwakilisha 18.94% ya jumla ya wapiga kura waliojiandikisha.
UPDATES: FEBRUARI 25, 2023
Upigaji kura umeanza saa 2:30 asubuhi katika vituo vya kupigia kura kote nchini Nigeria, na utamalizika saa 8:30 mchana, lakini yeyote ambaye tayari ameidhinishwa na yuko kwenye mstari wa kupiga kura bado ataruhusiwa kufanya hivyo.
Wakazi wa mji wa Kwankwaso katika jimbo la Kano wakiwa katika vituo vya kupigia kura.
4:45 Asubuhi: Tinubu azungumza baada ya kupiga kura yake
Mgombea urais wa chama cha All Progressives Congress Asiwaju Bola Ahmed Tinubu amezungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura yake. Tinubu ameelezea mchakato huo kuwa unaendelea vizuri huku akionesha matumaini juu ya idadi kubwa ya wapiga kura kujitokeza.
4:34 Asubuhi: Makamu wa Rais Osibanjo na mkewe wapiga kura katika Jimbo la Ogun
Makamu wa Rais wa Nigeria Prof. Yemi Osibanjo na mkewe wamepiga kura katika kituo cha 14 cha Ikenne, Jimbo la Ogun. Makamu wa Rais ni wa Chama cha All Progressives Congress ambacho mgombea wake wa urais ni Bola Ahmed Tinubu.
4:03 Asubuhi: Rais Muhammadu Buhari apiga kura katika Jimbo la Kastina, asema ana imani wagombea wa APC watashinda
Rais Muhammadu Buhari amepiga kura katika kituo chake cha PU 003 katika kata ya Sarkin Yara A, huko Daura, Katsina. Rais Buhari amekaa madarakani kwa miaka 8 na atakabidhi kwa serikali mpya Mei 29, 2023.
Rais Buhari amesema ana imani kuwa wagombea wa chama cha All Progressives Congress (APC) wataibuka washindi katika uchaguzi mkuu wa leo Februari 25 na Machi 11.
Akizungumza kwa Kiingereza na Kihausa, alisema: "Nimefurahishwa sana na mchakato wa uchaguzi. Nimefurahishwa na idadi ya wapiga kura."
3:15 Asubuhi: Peter Obi anafika kitengo cha kupigia kura
Mgombea urais wa Chama cha Labour, Peter Obi, amefika katika kituo chake cha kupigia kura cha PU 019, Umudimakasi Square, Agulu, Jimbo la Anambra. Ameonesha matumaini yake ya ushindi huku pia akisema hatafuti nafasi katika baraza la mawaziri la wapinzani wake.
3:11 Asubuhi: Mgombea urais wa PDP Atiku Abubakar anapiga kura Adamawa
Aliyekuwa Makamu wa Rais na mgombea urais wa Chama cha People's Democratic Party amepiga kura yake katika kituo chake cha kupigia kura huko Ajiya 02, katika Wadi ya Gwadabawa, Serikali ya Mtaa ya Yola Kaskazini ya Jimbo la Adamawa.
3:04 Asubuhi: Usalama waimarishwa maeneo mbalimbali ya Lagos
Wanajeshi wameweka vizuizi katika maeneo tofauti ya jimbo la Lagos katika kutekeleza operesheni inayolenga kuhakikisha utulivu wakati wa uchaguzi wa 2023.
Wanajeshi wakiimarisha usalama jijini Lagos
Shambulizi kwa timu za ufuatiliaji wa uchaguzi
Timu za ufuatiliaji wa uchaguzi za Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha, EFCC, zimeshambuliwa leo Jumamosi, Februari 25, 2023 huko Abuja na Jimbo la Imo.
Shambulio hilo lilifuatia kukamatwa kwa mwanamume mmoja kwa madai ya kupanga utaratibu wa ununuzi wa kura katika kituo cha kupigia kura katika Shule ya Msingi ya Sayansi, Bwari.
Msemaji wa EFCC Wilson Uwujaren amesema wahudumu walimkamata mwanamume wa makamo na kupata orodha ya wanufaika ambao tayari aliwalipa pesa kupitia benki.
UPDATES: FEBRUARY 27, 2023
Tume ya Uchaguzi yatuhumiwa kutokuwa na uwazi katika matokeo
Vyama vya Upinzani vya PDP na Labor Party vimesusia mchakato wa Utangazaji Matokeo kwa madai kuwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) imeonesha kuwepo kwa uchakachuaji wa Matokeo yanayoendelea kutolewa.
Hadi sasa ni takriban Theluthi Moja ya Kura za Majimbo 36 zimetangazwa ambapo kwa mujibu wa BBC Mgombea wa Chama Tawala (APC), #BolaTinubu ana 47% ya Kura zilizopigwa, Kiongozi wa Upinzani, #AtikuAbubakar 27%, na #PeterObi ana 22%.
Hata hivyo, Matokeo yanayoendelea kutoka kwenye maeneo ya Kaskazini na Kusini-Mashariki mwa Nigeria yanaonekana kuwa ngome za PDP na Labour Party na kufanya Matokeo ya mwisho kutotabirika.
Rais Mstaafu Obasanjo aitaka Tume ya Uchaguzi kuepusha hatari ya machafuko
Rais wa zamani Olusegun Obasanjo ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko yanayoendelea kuibuka kuhusu kutokuwepo uwazi kwenye Matokeo ya Kura zilizopigwa ikiwa ni pamoja na Tume kusoma Matokeo ya Kura ya mkononi badala ya Tovuti ya Tume.
Obasanjo amemtaka Rais #MuhammaduBuhari kufahamu kuwa kuna dalili za kuibuka Vurugu za Uchaguzi na kushauri Matokeo yote ambayo hayajakidhi Vigezo na yasiyokuwana Uwazi yafutwe mara moja
Aidha, Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wamesema Mchakato wa Utangazaji Matokeo umekosa Uwazi kutokana na Tume ya Uchaguzi (INEC) kutumia Matokeo yaliyokusanywa kwa Mikono badala ya yanayotakiwa kuwa kwenye Tovuti ya Tume.
Wanahabari wakamatwa, kushambuliwa au kunyanyaswa wakiripoti uchaguzi
Takriban wanahabari 14 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wamezuiliwa, kunyanyaswa, au kushambuliwa wakati wakiripoti uchaguzi mkuu wa Nigeria, akiwemo mmiliki wa tovuti binafsi ya habari ya WikkiTimes Haruna Mohammed Salisu, ambaye bado anashikiliwa na polisi bila kufunguliwa mashtaka.
Inaelezwa kuwa Polisi walimshikilia Salisu mnamo Februari 25 katika mji wa Duguri, kusini-mashariki mwa jimbo la Bauchi, muda mfupi baada ya yeye na waandishi wengine kukutana na gavana wa jimbo hilo, kwa mujibu wa mhariri wa WikkiTimes Yakubu Mohammed, ambaye alizungumza na CPJ.
Kwa mujibu wa Mohammed, ambaye alimtembelea Salisu baada ya kuhamishiwa makao makuu ya polisi huko Bauchi, Polisi walisema walimkamata ili kumlinda baada ya wafuasi wa gavana huyo kumvamia alipokuwa akiwahoji wanawake wa eneo hilo waliokuwa wakiandamana, lakini wakakataa kumwachilia.
Raia, vikundi vya kisiasa, na vikosi vya usalama vilitishia, kushambulia, au kukamata angalau waandishi wengine 13 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi. Hii ni kwa mujibu wa CPJ.
UPDATES: MARCH 01, 2023