Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,720
- 35,114
Siyo siri,
Rais wetu mpendwa ameshughilishwa mno na hoja zetu mbalimbali kama wananchi juu ya huu mkataba ambao serikali ilisha usaini mwezi february 2022 na kuja kuridhiwa na Bunge 30 Juni 2023.
Siyo siri
Kuna wakati hoja zetu wananchi zinavuka mipaka hata kuutweza utu na wafhifa wa Rais ambapo huu ni utamaduni mpya tulioletewa na CCM yetu ambapo imekuwa inawatweza utu wao wanaoikosoa serikali hata wengine kugharimu maisha yao.
Siyo siri.
Wasaidizi wa Rais wameonekana kupwaya kwa kiwango kikubwa. Waziri mwenye dhamana ya Habari amenyooshewa vidole kwamba amedhibiti vyombo vya habari hususani kuruhusu ama kukataza taarifa zinazoenda kwa umma kupitia vyombo hivyo, wasaidizi wengine wamechagua kutumia kauli zinazoleta ufa mkubwa kati ya serikali na raia wake. Wengine wamegoma kuuishi ukweli kwa kuamua bora liende kwa kutotoa ushauri, maoni wala msimamo wao juu ya sakata hili tata
Siyo siri,
Setikali yaani watawala wameweza kudhibiti mihimili mingine ya serikali yaani Bunge na Mahakama, mihimili hiyo imejikuta katika mazingira ya kukubaliana na kila jambo linalotakiwa na watawala. Bunge siyo sauti ya wananchi tena. Mahakama siyo Hekalu la HAKI tena. Tumeona pia matumizi mabaya ya vyombo vya dola kinyume na kabisa na katiba, sheria wala uzingativu wa haki za binadamu vikifanywa ili kiwardhisha watawala.
Siyo Siri,
Inatia huzuni kuona watawala wakitumia jukwaa na udini kupenyeza hoja zao na kulitumia jikwaa hilo hilo la udini kuwapasua na kuwagawa Watanzania.
Siyo siri,
Mkataba baina ya Taifa letu na Dubai ni sehemu ya mikataba kadhaa ambayo tayari imeshaingiwa,na kinachosubiriwa ni utekelezaji wake mmoja baada ya mwingine.
USHAURI WANGU KWA WATAWALA.
Maadam mkataba umeshapitia ngazi zote husika na kupitishwa, lakini raia wamekuja juu kuhoji, kupinga hata kujiapiza dhidi ya mkataba huo,.
Pia kwa sababu wapo wananchi ambao nao wanaona hii ni fursa adhimu na wanakubaliana na serikali kwenye taratibu, dhumuni hata malengo ya mkataba huu.
BASI
Serikali iitishe na kuandaa kura ya maoni. Kura ya wazi ambayo haitahusisha mitaguso ya kisiasa wala mabaraza ya dini.
Kupitia Kura ya Maoni tupate msimamo kama nchi wa kuingia ama kuachana na mkataba huu.
Serikali iunde kamati huru itakayojumuisha makundi yote kwenye jamii kusimamia kura hii ya maoni.
Uzalendo haujengwi kwa kupinga ama kukataa daima, bali uzalendo ni jambo la kuitakia mema, ustawi na siha njema nchi yako