Wimbi kubwa la vijana kuanzisha NGOs ajenda zile zile

Tengeneza Njia

Senior Member
Jul 29, 2022
121
204
Ndugu zangu,

Kabla ya wiki kuisha nimeona niwashirikishe hili. Wiki hii nimehudhuria warsha kadhaa hapa mjini na nimeona kitu ambacho naweza kusema ni wimbi la uwepo wa vijana wengi wasomi ambao nadhani wamevutiwa na idea nzima ya kuitwa/ kujulikana kama waanzilishi au ma-ceo katika makampuni na taasisi zao binafsi.

Silipingi hili ila nadhani wengi wao wanapata msukumo instagram na kudhani kufanya mambo kama haya ni kuhudhuria warsha na mikutano pekee, kupiga picha na watu maarufu, kuongeza wigo wa kujulikana bila kweli kuwa na lengo madhubuti la kuleta matokeo huku mtaani.

Unajua biashara (hata kama ni NGO) ya kuja na wazo la mradi, kuliandikia proposal, kulitafutia watendaji, na baadae kuripoti na kusuka suka matokea ni suala rahisi sana, nimeongea na baadhi yao na kufanya uchunguzi, wengi wanafanya hivyo!

Sasa, tunapaswa kuamini tena nguvu zinazofanywa na hizi asasi?

Vijana wengi kwa woga wa kuajiliwa au kubaki mtaani bila ajira wanakimbilia huku, lakini hakuna kinachofanyika kwa hawa wanufaika ambao wanatajwa sana kwenye makabrasha yao (maproposal). wengine wanapata na fedha kutoka kwa wafadhili lakini haziwafikii kweli wahusika.

Nadhani wahusika waangalie upande huu kwa jicho la tatu, angalieni sana hizi asasi za mjini hasa zinazoanzishwa kwa madai eti ya kuwanufaisha vijana, wasichana, walemavu. Vi-NGO uchwara.

Lakini nitoe rai kwa hawa hawa wenzetu, ukishajikita katika maeneo haya basi msijikite zaidi katika kuhudhuria warsha na mikutano na kupiga tuu picha ili taasisi zenu zionekane zipo busy kufanya kitu na unakuta wanaofanya hivi ni sura hizo hizo wengine katika taasisi hawapati fursa.

Basi, wacha hii iwafikirishe!

Na
 
Ngo zakuaminika ni Afya pekee hizo zingine ni uchwara ..

Japo kwenye afya nako kumeingia wapigaji
 
Kwa hiyo wewe unaamini wameanzisha hizo NGO kwa Lengo la kuwanufaisha hao walengwa?..Hayo unayoona wakifanya ndio malengo yao haswaa
 
Hawata kuelewa..wanataka majina makubwa makubwa kama founder ceo etc.

Wakati matokeo sifuri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom