Alana Rolmodo
Member
- Jan 9, 2024
- 19
- 25
Karibu nikuandikie script nzuri kwaajili ya FILAMU na nyimbo nzuri zinazoweza kuwa hit song. Karibuni sanaππππππππ
By Alana Mwanafasihi
β¨Sanaa ni kazi kama kazi zingine
(0759161254)
Sample ya script
1.CHUMBANI KWA CHIFU
(Open scene) Mke wa Chifu (Mwamini)anaingia chumbani na kumkuta Msichana mdogo aitwaye Oliga, ambaye anatumikia katika himaya ya kichifu anabakwa na Chifu . Chifu anapomuona mkewe, bila aibu na huruma anamfukuza Mwamini nakumuonya asiingie Tena chumbani.
CHIFU: Kwanini unakatisha raha zangu?
MWAMINI: Mume wangu, unachofanya sio sahihi...
CHIFU: Nitakuua, Toka nje, nimalize suala langu. Na ole wako upanue mdomo wako na kumueleza mtu yeyote.
(Mwamini anatoka nje Kwa huzuni huku machozi yakimteremka.)
2. Anaonekana Mwamini( Mke wa Chifu akiwa amekaa chini ya mti huku analia na kuzungumza peke yake
MWAMINI: Eee Mungu, hivi ni lini haya mambo yatabadilika! Kila mwanakijiji anatambua kwamba, Chifu ni mtu mzuri lkn Mimi msiri wake ndo natambua Kila kitu! Anafanya mabaya mengi lkn mabaya yake yamefichwa! Ipo siku atafichuka na Kila mtu atajua!
( Akiwa anazungumza hayo, Kuna binti alikuwa anamsikiliza Kwa kuibia, baada ya kusikia alichokiongea Mwamini anakimbia kuelekea nyumbani kwao)
3. ( Binti (Mwanahamisi) anamsimulia mama yake alichokisikia Kwa Mke wa Chifu, lakini mama yake anamuonya asije akamwambia mtu yoyote, kwani Chifu ni mtu anayeheshimika sana kijijini.
MAMA MWANA: Mwanangu, mbona umekuja Kwa kuhema sana? Kuna Nini ?
MWANAHAMISI:Mama, kitu nilichokisikia kutoka Kwa Mke wa Chifu! Hata huwezi amini!
MAMA MWANA: (Anamtazama MWANA Kwa makini sana) Umesikia kitu gani?
MWANAHAMISI: ( Anasimulia: Flashback)
MAMA MWANA: Inawezekana Umesikia vibaya! Sasa funga bakuri lako na usije ukamwambia mtu yeyote. Chifu ni mtu tunayemuheshimu hapa kijijini na Kila mtu anampenda kutokana na mema yake.
( MWANA ANAONEKANA KUTOPENDEZWA NA MANENO YA MAMA YAKE, ANASIMAMA NA KUINGIA NDANI)
. 4. Chifu Akwene akiwa na vibaraka wake maeneo ya mtoni, wanamwona msichana(wansila) akiteka maji. Chifu anaonekana kuvutiwa na msichana huyo, anamuagiza mmoja wa vibaraka wake amuite wansila. Wansila anaitika wito Kwa Chifu, wanasogea pembeni kuongea.
CHIFU AKWENE: Binti mrembo na kisura... Upo katika himaya yangu hii! Ni jambo la kustajabisha sana, sijawahi kukuona! wewe ni mtoto wa nani?
WANSILA: Mimi ni mtoto wa Mzee Bashuti
CHIFU AKWENE: Oh! Sawa! Basi nimeshajua u mtoto wa nani! Unaweza kwenda.
WANSILA: ( Anamuinamia Chifu Kwa heshima, Kisha anaondoka) Macho ya Chifu hayaachi kumtazama Wansila huku akiwa anatabasamu.
5.Chifu Akwene anazungumza na kibaraka wake kuhusu Wansila. Wakiwa wanazungumza, Oliga akiwa amejificha nyuma ya migomba, anasikiliza wanachokiongea.
CHIFU AKWENE: Nawaza makubwa juu ya Binti Wansila
NASIR; Mkuu, macho yako yanazungumza upendo mkubwa sana juu ya Binti yule? Nini mpango wako Sasa?
CHIFU AKWENE: Mpango wangu unajieleza! Lazima nimfanye kuwa Mke wangu wa pili.
NASIR: Maamuzi yako na yaheshimiwe kiongozi. ( Anamuinamia Kwa heshima)
CHIFU: Nataka utoe tangazo Kwa Kila mtu, kwamba kesho kutakuwa na sherehe fupi ya kumtambulisha Mke wa pili.
NASIR: Sawa mkuu.
( Oliga aliposikia hivyo, alionekana kusononeka sana, huku uso wake ukiwa umefura hasira, Kisha akaondoka)
6. (Oliga akiwa nyuma ya nyumba, anaonekana akilishika tumbo lake huku akijisemesha peke yake)
OLIGA: kwakuwa nimebeba kiumbe Cha Chifu ndani ya tumbo langu! Sitaruhusu Wansila awe Mke wa pili.
( Wakati anazungumza hivo, Mwamini( Mke wa Chifu alimsikia, hivyo akamuuliza
MWAMINI: Oliga! Una mimba!!!
OLIGA: (Kwa aibu, akamjibu) ndiyo Mama
MWAMINI: Umebakwa, Leo ni siku ya tatu. Imekuaje useme una mimba?
OLIGA: Mama! ( Anashusha machozi) Naomba unisamehe sana, sikuwahi kukuambia, lakini Chifu amekuwa akinifanyia hivyo Kila wakati, Hii ni awamu ya 10 Sasa kunibaka.
MWAMINI: ( Anashindwa kujixuia, Machozi yanamtoka na kuondoka Kwa hasira kuelekea Kwa Chifu)
7.( Chifu anawambia vibaraka wake waandae mazingira mazuri kwaajili ya sherehe, ghafla Mwamini anaingilia kati)
CHIFU AKWENE: Hakikisheni mazingira yote yapo vizuri, mkisaidiana na Vijakazi, mahali pa sherehe papambwe vizuri kwaajili ya kumtambulisha malkia wangu mpya
MWAMINI: Sasa inatosha! Hakuna Sherehe Tena!
CHIFU AKWENE: ( Anasimama! Na kumuangalia Mke wake Kwa hasira) Unathubutuje kusema hivyo?
MWAMINI: ( Anagundua amekosea kuongea Kwa ukali mbele ya Chifu na Vijakazi vyake, Anaomba msamaha na kumuombea waongee pembeni. Baada ya kutoka pembeni, Mwamini Anamtazama mume wake huku machozi yakimteremka.
" Mume wangu! Naomba hairisha hiyo sherehe...
CHIFU AKWENE: Kwanini nihairishe?
MWAMINI: Oliga ni mjamzito. Kama kusudio lako ni kupata Mke wa pili, basi nafasi hiyo achukue huyu kijakazi mjamzito.
CHIFU AKWENE: (Kwa jazba) Hili haliwezekani! nasema haliwezekani!
MWAMINI: Mume wangu, itakuaje Sasa?
CHIFU AKWENE: Ebu niitie Oliga
(Mwamini anaenda kumuita Oliga)
8. OLIGA akiwa mbele ya Chifu, Anaonekana mwenye wasiwasi sana kutokana na jazba inayoonekana machoni mwa Chifu. Chifu anamuambia Oliga Kwa ukali " Binti! Nahitaji unywe dawa ya kutoa hiyo mimba haraka sana!". ITAENDELEA............