Waziri Ridhiwani Kikwete afanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
510
732
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran aliyeongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo

#KaziInaendelea
IMG-20240816-WA0018(1).jpg

IMG-20240816-WA0005.jpg

IMG-20240816-WA0055.jpg
IMG-20240816-WA0056.jpg
 
IMG-20240816-WA0008.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, Ijumaa tarehe 16 Agosti 2024

Bi. Ndomba Doran aliyeongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha amechukua nafasi hiyo kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuhudumu katika Wizara hiyo. Pia alimueleza kuhusu mikakati mbalimbali ya Chama Cha Waajiri kwa maslahi ya Waajiri nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Kazi amefurahi kukutana na Bi. Ndomba-Doran ambapo pia amemhakikishia ushirikiano wa wizara hasa katika kutekeleza dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuona vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wanapata ajira zinazozalishwa na sekta mbalimbali nchini.

IMG-20240816-WA0009.jpg

IMG-20240816-WA0006.jpg

#KaziInaendelea
 
Attachments

  • IMG-20240816-WA0007.jpg
    IMG-20240816-WA0007.jpg
    72.3 KB · Views: 1
Riz na hao ATE wahakikishe na wanadhibiti uingiaji wa wafanyakazi wageni kiholela.
Wahakikishe wana mfumo wakuingiza wageni ambao kweli tunawahitaji na sio kuingiza tu watu hovyohovyo kutoka China, India, Pakistan, South Africa nk ilihali wapo mamilioni ya Watanzania wanaoweza kufanya hizo kazi.

Upatikanaji wa vibali vya kazi umekuwa rahisi sana maeneo mengi ilihali hizo kazi watanzania wengi wanaweza kuzifanya na kulipwa vizuri.
Tatizo la ajira ni kubwa tusipokuwa makini kulinda ajira za wazawa vijana wetu wengi watabaki mtaani hohehahe.
 
Hakuna lolote, kwani hao waajiri wamezificha ajira mfukoni mwao, kwamba wakiongea na Ridhiwani Kikwete ndiyo watazitoa?
 
Riz na hao ATE wahakikishe na wanadhibiti uingiaji wa wafanyakazi wageni kiholela.
Wahakikishe wana mfumo wakuingiza wageni ambao kweli tunawahitaji na sio kuingiza tu watu hovyohovyo kutoka China, India, Pakistan, South Africa nk ilihali wapo mamilioni ya Watanzania wanaoweza kufanya hizo kazi.

Upatikanaji wa vibali vya kazi umekuwa rahisi sana maeneo mengi ilihali hizo kazi watanzania wengi wanaweza kuzifanya na kulipwa vizuri.
Tatizo la ajira ni kubwa tusipokuwa makini kulinda ajira za wazawa vijana wetu wengi watabaki mtaani hohehahe.
 
Riz na hao ATE wahakikishe na wanadhibiti uingiaji wa wafanyakazi wageni kiholela.
Wahakikishe wana mfumo wakuingiza wageni ambao kweli tunawahitaji na sio kuingiza tu watu hovyohovyo kutoka China, India, Pakistan, South Africa nk ilihali wapo mamilioni ya Watanzania wanaoweza kufanya hizo kazi.

Upatikanaji wa vibali vya kazi umekuwa rahisi sana maeneo mengi ilihali hizo kazi watanzania wengi wanaweza kuzifanya na kulipwa vizuri.
Tatizo la ajira ni kubwa tusipokuwa makini kulinda ajira za wazawa vijana wetu wengi watabaki mtaani hohehahe.
Shida ya watanzania wengi ni wezi wanachowaza ni kuiba tu wakiajiriwa viwanda vingi vya wahindi na wachina wameajiri wahasibu kutoka kwao sababu wanajua wabongo walivyo waharibifu sijui Nini kifanyike
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, Ijumaa tarehe 16 Agosti 2024
Hajatupa ndoana hapo kweli?
Ametoka hivihivi!!
Hata hisia tu!!!
 
Ajira zipo nyingi Tanzania.
Tatizo ni kwamba Serikali Haifuatiliii masuala ya ajira Sekta Binafsi.

Sekta Binafsi Ajira Ni Tele ila Mwajiriwa Mmoja anashikilia Ajira Tatu hadi Nne kwa malipo ya Ajira Moja.

Labor Officers hawafuatilii kabisa. Unakuta mtanzania anakubali Nyongeza ya majukumu bila nyongeza ya maslahi kwa kuogopa kutimuliwa.
Na pia wataalamu wanapewa mikataba mifupi wakishaumwaga utaalamu wao wanaondolewa inabakia cheap labor.
 
Back
Top Bottom