Hawa ewura watakuwa wamevuta mpunga kutoka IPTL siyo bure. Wachunguzwe haiwezekani mnajua kabisa hii kitu haitakiwi hata kutangazwa/ kusikika kwenye ofisi za umma mnajitia kimbelembele. Tena nadhani hiyo top management yote waliohusika wanatakiwa kukaa pembeni.
Hah ! Hah! nacheka kwa huzuni kubwa Mkuu, yaani jamaa wa EWURA mishipa ya shingo inamtoka kutetea ''haki ya Kisheria'' ya IPTL bila kujua hasira waliyonayo wananchi kuhusu tulivyopigika kwa ''mienendo ya mashaka'' ya IPTL na washirika wao waliosaini ''mikataba mibovu'' kuiingizia nchi hasara na bili kubwa kwa wateja wa umeme.