Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza katika mabasi yaendayo kasi

Natumaini alirudi pia na hilo basi hadi Ferry!

Kuhusu matumizi ya tiketi, hao DART wangeweka wakaguzi wa tiketi ambao wanakuwa wanafanya ukaguzi randomly. Na mtu akikamatwa apigwe faini kubwa; akishindwa apewe adhabu ya kufanya community service. Kumkamata na kumpeleka polisi ni kutumia fedha za umma vibaya, maana watakamatwa wengi sana. DART kwa kushirikiana na Jiji watengeneza by-laws zitakazotumika katika kutoa miongozo kwa abiria ya namna ya kutumia mabasi hayo, haki zao kama wateja/abiria, na adhabu pale watakapofanya kinyume na miongozo. Hakuna haja ya ku-invent the wheel, wakati tunaweza kuiga kwa wenzetu walioanza kutumia mfumo huo wa usafiri toka kitambo.
 
Mhhhhh, maigizo mengine buana, aliposafiri Lowassa waliosema anatafuta kura
 
Ilipaswa unapoanzia Huo usafiri kuwa na Parking kubwa ya kulipia kwa mfano mtu anaeishi Kibamba au Mbezi mwisho anakuja na usafiri wake mpaka hapo ndio anautumia huo wa Umma, sio rahisi sana mtu wa kibamba mwny gari yake aipark home aparamie maboda boda na mabasi mpaka zinapoanzia BRT na akirudi kutokea japo asumbuke tena
Foleni inaweza kupungua kwa kuboresha Miundombinu ila inaweza kuisha kwa ku discourage magari kwenda Mjini!
Mkuu umenena! Tatizo ya viongozi wetu hakuna anaeiona kesho
 
Waziri Mkuu Majaliwa: Vyombo vingine vya moto kutumia njia ya mabasi ya kasi kutasababisha ajali zisizokuwa za muhimu.

Ajali za muhimu ni zipi?
 
Afadhali majaliwa kaja kikazi kuliko yule alipanda basi gongo la mboto kuwanesha wananchi kwamba yupo nao,uchaguzi umeisha hatujamuona tena akipanda dala dala
 
Waziri Mkuu Majaliwa: Vyombo vingine vya moto kutumia njia ya mabasi ya kasi kutasababisha ajali zisizokuwa za muhimu.

Ajali za muhimu ni zipi?
Matamko ya huyu PM huwa hayaendani na hadhi yake. Rejea lile tamko la kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.
 
Mkuu umenena! Tatizo ya viongozi wetu hakuna anaeiona kesho

Wakuu, while I agree with you, lets learn to appreciate. Kiukweli Tanzania ni nchi ngumu sana, not least because tumejaliwa viongozi wabovu who are incredibly corrupt. Lakini lazima tukubali pia kwamba tuna competing priorities. Huwezi kusema kwamba ufanye allocation ya resources zote kwa miundombinu ya DART....I mean kuna mashule, watoto wanakaa chini, kuna hospitali watu wanalala chini nk nk.....In fact kuna matatizo mengi ya nchi hii only the government can intervene. Ni rahisi sisi tulioko mjini kwenye comfort zone kusema hiki kipo hiki hakipo..lakini I doubt my Brother Magufuli has that luxury. Maana inabidi awatumikie watanzania wote. na resources hazitoshi. Kuna MATATIZO humu wengine tunayasoma kwenye mitandao..tuu.....kwamba watu wanakula mizizi....entire generation haijaenda shule nk....all these need proper planning. Na wote wanaiangalia serikali hiyo hiyo tunayoilaumu kila siku.

Again, I am not out there defending incompetence. Lakini naamini kwa dhati kabisa, hii DART, with its imperfections, bado ni hatua kubwa.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
na resources hazitoshi. Kuna MATATIZO humu wengine tunayasoma kwenye mitandao..tuu.....kwamba watu wanakula mizizi....entire generation haijaenda shule nk....all these need proper planning. Na wote wanaiangalia serikali hiyo hiyo tunayoilaumu kila siku.

Again, I am not out there defending incompetence. Lakini naamini kwa dhati kabisa, hii DART, with its imperfections, bado ni hatua kubwa.
huwezi kunambia resources hazitoshi wakati serikali inaenda kununua ma lori 700 ya washa washa wakati nchi hii ukimwaka Land Rover tatu tu za polisi mnafunga Kariakoo nzima. TANESCO imetoa tenda za kuagiza transformer India wakati hapa tuna TANELEC ambao TANESCO ni mmiliki mbia, na kuna nchi za jirani zinakuja kununua hizi hizi za TANELEC. Imagine that!

Juzi bungeni Waziri wa Muungano anasema wameipa tenda kampuni ya UK iwashauri jinsi ya kugawana mapato Tanganyika na Zanzibar. Jamani, jamani, hivi UK inaweza kuwalipa wachumi wa University of Dar-es-Salaam waende kuwashauri Scotland, England na Ireland jinsi ya kugawana mapato ndani ya UK? Incredible wasteful spending.

Na unaposema Tanzania ni nchi ngumu. Mimi nadhani hakuna nchi rahisi kuiongoza kama Tanzania. Rais anaweza kutoa tamko kwamba leo nafuta national holiday pesa zikajenge barabara, na inakuwa. Huwezi fanya hivyo nchi za wenzetu, hapa kwetu jamani kuongoza is a walk in the park.

Waziri anasimama bungeni anasema kuanzia kesho marufuku mtu kuuza shamba lake, ukitaka lipeleke Halmashauri waligawe! Na ikawa. Ni kama Mwenyezi Mungu alivyoumba mbingu na nchi, aliwapa watendaji wake siku saba tu, akawa anatoa matamko tu na inakuwa. Kiongozi anaweza kuleta breathtaking changes in Tanzania kwa mdomo tu! Kwa agizo la Rais!
 
Back
Top Bottom