Huko ni kuuwa biashara za watu. Coaster zetu tuzipeleke wapi sasa ? mikoani au nje ya jiji kabisa?Tajirijasiri, hebu fungua ndani humo usome habari kiundani kwanza. Mimi nimesikia kwamba watazuia daladala tu kuanzia next week ili wanaotumia daladala ndo wapande hayo magari ya mwendo kasi.
Zikija huko gongo la mboto nadhani zitakuwa zinatoka kwa foleni. Hii siyo nzuri.Bora hizo daladala zitakazo ondelewa huko zije huku gongo la mboto maana kuna abiria wengi balaa
Nafikiri wanaokurupuka ni wewe na wenzio mnaovamia vichwa vya habari bila kusoma. Tafuta taarifa ya PM uisome uone kama alichoongea ndio kilichoandikwa, hivi watu gani wale walifananishwa na nyumbu?awamu ya kukurupuka,rais anakurupuka,waziri mkuu anakurupuka ,mkuu wa mkoa anakurupuka.
impact ya kiuchumi kuzuia hayo magari kuingia town ni kubwa sana,hao wauzaji wa mafuta watasimamisha biashara zao maana mapato yatashuka pia itaathiri mfumo wa kodi na ajira
Yaani mkuu Watanzania wengi ni watu wa ajabu sana. Wako so negative, wanaombea vitu visifanikiwe sijui ni kwa faida ya nani? Watu wa aina hii hawana tofauti na wachawi.Kupitia uzi huu ndio utajua kuwa sisi Watanzania tumebeba negative minds kuliko kiumbe yeyote......
Yaani kwa kuwa jambo limenenwa na mtu ambaye ni mpinzani wake kisiasa hata kama ni la kitaifa litapingwa kwa nguvu zote au kubezwa.........
Akili zetu kwa kulewa siasa uchwara tunashindwa kutofautisha jambo la kitaifa na jambo la kisiasa.....
Wewe unaongea kama nani ambaye unasema upunzani uingie upange mji vizuri ulizaliwa lini. Si ndio nyie mmeteta watu wa mabondeni unajolaumu serikali ni kipi hasa. Kama ni mpinzani kweli basi kumbukumbu zako ziko tenge tafakari kwanza msimamo na mawazo yako kabla hujapeleka hewani
Huyu kotapini ni Kubenea.Wewe unaongea kama nani ambaye unasema upunzani uingie upange mji vizuri ulizaliwa lini. Si ndio nyie mmeteta watu wa mabondeni unajolaumu serikali ni kipi hasa. Kama ni mpinzani kweli basi kumbukumbu zako ziko tenge tafakari kwanza msimamo na mawazo yako kabla hujapeleka hewani
Hawajijui kuwa wao ni wakurupukaji kama nyumbu. Waandikie kichwa cha habari cha kuponda kitu uone watakavyokurupuka bila kuthibitisha.Yani kama vile hamyajui magazeti yenu vile,nunua hilo gazeti usome heading na content ni tofauti kabisa.Acheni kutokwa na povu pasipo sababu.
Wewe egesha gari lako sehemu urudi ukute liko juu ya mawe.Nijuzeni jamani. Mipaka ya kstikati ya jiji ni ipi? Na nikitoka na gari langu huko pembezoni ya mji nilipaki wapi nitembee kwa miguu au nipande hayo magari ya haraka?
Ukiwa muelewa utaelewa
Unapomzuia mtu kutumia gari lake binafsi katikati ya jiji ni ubabe na ubaguzi wa hali ya juu sana. Watu wana ratiba na shughuli zao ninazowalazimu kutumia Magari yao wenyewe kwa sababu mbalimbali. Leo hii unatoa tamko la kuwakataza. Huo unakuwa ubabe wa hali ya juu sana.
Boresheni miundo mbinu ya reli na barabara tu. Waacheni wananchi wasafiri watakavyo.
Hata usipokatazwa kwenda na gari lako katikati ya jiji, ukweli unabaki pale pale kwamba hautaweza kupita wala kufika katikati ya jiji kwani njia zimejaa, hazipo. The city centre is simply unaccessible.
Unapomzuia mtu kutumia gari lake binafsi katikati ya jiji ni ubabe na ubaguzi wa hali ya juu sana. Watu wana ratiba na shughuli zao ninazowalazimu kutumia Magari yao wenyewe kwa sababu mbalimbali. Leo hii unatoa tamko la kuwakataza. Huo unakuwa ubabe wa hali ya juu sana.
Boresheni miundo mbinu ya reli na barabara tu. Waacheni wananchi wasafiri watakavyo.
Chifu, hili ndilo nilikuwa nikifikiria pia. Yaani hawa viongozi wetu sijui uwa wanafikiri vipi? Hawa wanasafiri Ulaya lakini hawajifunzi!!
Kama ulivyosema, dawa ni kuongeza kodi za kutumia barabara za City Centre, na kuweka parking fees hapo City Centre kuwa bei za juu sana. Parking kwenye maeneo ya katikati ya Jiji iwe ni biashara ya Jiji. Haya mambo mawili yatapunguza gari automatically bila hata serikali kutumia nguvu nyingi. Wanaweza kufunga CCTV kwenye maeneo yote ya kuingia na kutoka City Centre kwa ajili ya kurekodi idadi ya magari ili wafanye monitoring ya wanaolipa na wasiolipa hizo kodi.
Hilo la uandishi wa kubabaisha ni tatizo kubwa sana barani Afrika. Watu wanabakia kuwa mazuzu kwa sababu ya aina ya ukanjanja wa uandishi wa habari.Waandishi kanjanja!!
Majaliwa hajakataza, ila kashauri!!
Nia ya brt ni hiyo, watu waache magari wapande mabasi! Ila hakuna katazo!!
Word.Mkuu wala huhitaji kuhangaika na hizo process zote za kufunga CCTV! Unaweza kuamua kwamba kila gari inayoingia city center iwe na sticker ambayo iko verified na system... sticker ilipiwe certain amount (one month to one year!). Ukikutwa huna hiyo sticker ni fine.
Mkuu, vitu vingine ni ubunifu tuu..sasa tatizo viongozi wetu sijui hawana washauri! (Ofcourse washauri wapo lakini 80% ni political advisors!) Yaani hili ni jambo ambalo halihitaji hata kupiga kelele na kudraw attention ya wananchi. After all wanaoendesha magari ni middle class! And I can assure you..tutakuwa tumepunguza msongamano na serikali inapata hela ya kuboresha huduma ndani ya JIJI letu.
Masanja.