Wazazi tusomeshe watoto waje kujiajiri kwa taaluma walizosomea au kuajiriwa, biashara kwa hapa Tanzania zataka moyo

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,094
Tangu nimezaliwa 1980s mwishoni nimeshaona wafanya biashara wengi sana wakifirisika, kufunga biashara, mtu anaenda dukani kila siku asubuhi hadi jioni hana muda wa familia, kurudishwa nyuma kwa maduka kuungua au kuibiwa, umafia katika biashara, n.k.

Lakini kwa wakati huo huo niliona waajiriwa wengi maisha yao yakiwa at least na nafuu, ni wachache sana waliofukuzwa makazini, walikuwa na muda wa kupumzika na familia zao, mshahara wa uhakika hata wakiumwa, kupanda vyeo, n.k.

Ni kweli wafanyabiashara waapo waliotoboa sana lakini ni wachache, tena ni wachache zaidi ambao hudumu na hali hio kwa zaidi ya miaka 20, lakini kwa upande mwengine ukicheki wale waajiriwa wenye afadhali hawawezi kufikia wafanyabiashara wachache waliotoboa lakini kwa idadi wapo wengi na wanaishi maisha standard kwa muda mrefu tu.

Ukienda hata maeneo wanayoishi watu wenye maisha kama osterbay, mbezi bech, n.k. ni kweli wafanyabiashara wapo na wamejenga majumba ya mabilioni lakini ni wachache idadi yao ni ndogo lakini waajiriwa unawakuta ndio wamejaa zaidi, hapa ndipo unapoona ni kweli waafanya biashara wametoboa ila ni wachache kwa idadi.
 
Biashara inanyima uhuru ,unatembea na roho mkononi.

Ajira kama za serikali zina consistency nzuri in terms of earning cash.
 
Field yoyote ukiwa na focus lazima upate matokeo chanya.

Hapa tz unakuta MTU anafikisha miaka 30 bado ameshindwa kuweka focus katika jambo moja
Ndio biashara unajitoa kweli ,namuona father mdogo ameajiri watu ila analala saa 7 ila alfajiri yupo macho acha yaani.

Kuna gari zake zinapiga route mpaka zifunge na maduka yake yote ndio analala.
 
Mbn wenzio wanafanikiwa?
hao mnaowaona wamefanikiwa ni wachache sana, na ni kweli wamefanikiwa kuzidi waajiriwa lakini ni wachache, mfano ukienda mitaa wanaayoishi watu wanaojiweza utawakuta wafanyabiashara wachache lakini waaajiriwa wengi.

Wafanyabishara maeneo hayo ndio wanajenga nyumba za kifahari zaidi ya wengine lakini ni wachache
 
Ndio biashara unajitoa kweli ,namuona father mdogo ameajiri watu ila analala saa 7 ila alfajiri yupo macho acha yaani.

Kuna gari zake zinapiga route mpaka zifunge na maduka yake yote ndio analala.
Inaonekana kinachokusumbua wewe ni uzembe. Hata hao walioajiriwa wakapata nafasi kubwa zenye maslahi usidhani wanapata muda wa kulala tuu na kula bata. Wanasota sana kutimiza wajibu kwenye nafasi zao
 
hao mnaowaona wamefanikiwa ni wachache sana, na ni kweli wamefanikiwa kuzidi waajiriwa lakini ni wachache, mfano ukienda maeneo ya watu wanaojiweza utawakuta wafanyabiashara wachache

Inategemea umeajiriwa wapi na unaingiza sh ngapi.
 
Kwa hiyo kujiajiri atakuwa anafanya nini, hiyo sio biashara? Umejiajiri kwenye kilimo..unakodi shamba,unalima, unavuna, unatafuta soko, unauza. Hiyo sio biashara?
Cpa - Muhasibu kama Mengi (Rip)
Advocate - wanasheria kama kina Mukono
Madaktari
Consultants
ConstructionEngineers
 
Inategemea umeajiriwa wapi na unaingiza sh ngapi.
Point ni kwamba hata maeneo kama Osterbay, Upanga, Mbezi ni kweli wafanyabiashara wapo na wamejenga majumba ya mabilioni lakini ni wachache idadi yao ni ndogo, wengi wanaoishi hizo sehemu ni waaajiriwa

Unagundua kwamba waajiriwa wana share kubwa katika demographics husika
 
Point ni kwamba hata maeneo kama Osterbay, Upanga, Mbezi ni kweli wafanyabiashara wapo na wamejenga majumba ya mabilioni lakini ni wachache idadi yao ni ndogo, wengi wanaoishi hizo sehemu ni waaajiriwa

Unagundua kwamba waajiriwa wana share kubwa katika demographics husika



Kwanza wekeza katika wewe Fanya self-investment.

Kufika on top iwe biashara au ajira inahitajika Akili inayowaza vyema.
 
Back
Top Bottom