Watumishi wa umma kutopanda vyeo/madaraja hadi wapitie mafunzo maalumu

Wekea nyams kidogo hii habari. Ni watumishi wote ama baadhi ya kada?
 
Safi sana Waziri hivi ndiyo viwanda vya CCM.
 
Sijui kati yangu mimi na wewe anani ambaye hajui,uzi unasema hutaruhusiwa kupanda cheo au daraja Mimi nimezungumzia upande wa kupanda Daraja Sijazungumzia Cheo na sijasema kuwa cheo na daraja ni sawa!
Alafu kwenye utumishi wa Umma kupanda daraja ni kila baada ya miaka 3 hii ni kada yoyote ile hiyo 4 sijui wewe umetoa wapi?? .Kuna baadhi ya kada ili upate daraja fulani ni lazima ukapate mafunzo au uongoze Elimu kada hizo ni upande wa Mchumi,Mhasibu na utumishi kwa kada zingine sijajua inakuwa vipi.
Hata hivyo utofauti kati ya cheo na daraja Ni mdogo sana,kwani vina uhusiano kulingana na Muundo wa vyeo vya utumishi wa Umma.Mfano Kicheo mtu wa kada nyingine atakuita ''Mchumi'' lakini ukija kimuundo Unaitwa Mchumi daraja fulani!
 
Kaka kachukue standing order usome upya ,Hapo Mhandisi daraja la pili ndio cheo cha huyo Mhandisi-kwenye utumishi wa umma Cheo ni kazi yako inayokutofautisha na kada zingine ndio cheo.
Na kwa mfano wake maana yake Kwa uoande wa Halmashauri za Wilaya na Miji,manisipaa na MIkoa wenye vyeo ni MKurugenzi wa Halmasauri ya Wilaya ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,RAS,RC ndio wenye vyeo tu!
 
Mkuu kulingana na Standing Order inayotumika Mpaka sasa ulilolisema ndio upo sawa Mtu hupandishwa daraja ndani ya cheo fulani mfano Mhasibu daraja la kwanza-husomeka kama cheo kwenye standing order
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…