Watumishi wa umma kutopanda vyeo/madaraja hadi wapitie mafunzo maalumu

Wekea nyams kidogo hii habari. Ni watumishi wote ama baadhi ya kada?
 
Serikali ya kibashite, sijui hawa mawaziri wanatumia nini kulewea. Mmoja juzi kaja na vyeti (yule hakujipanga). Huyu atakuwa kaagizwa atafute sababu ya serikali kutopandisha madaraja, hivi hizo taasisi za kutoa mafunzo kwa watumishi wote wa umma zitatosha na hizo pesa zitatoka wapi ikiwa pesa tu za kuajiri watumishi wapya hazipo (maana kasema mafunzo yatagharamiwa na serikali).
Safi sana Waziri hivi ndiyo viwanda vya CCM.
 
Wewe inaonyesha huzijui kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Shortly:Mtumishi wa umma huajiriwa katika daraja fulani kulingana na elimu yake, na atatakiwe apande daraja moja kila baada ya miaka 3 au 4 kulingana na bajeti. Na endapo atakuwa na cheti cha elimu ya juu zaidi ya kile alichoajiriwa basi atatakiwa akiwasilishe baada ya miaka 3 ili apandishwe daraja stahiki na elimu yake.
Kuna utofauti kati ya neno CHEO na DARAJA katika utumishi wa umma.
Government is not a company in terms of circle.
Sijui kati yangu mimi na wewe anani ambaye hajui,uzi unasema hutaruhusiwa kupanda cheo au daraja Mimi nimezungumzia upande wa kupanda Daraja Sijazungumzia Cheo na sijasema kuwa cheo na daraja ni sawa!
Alafu kwenye utumishi wa Umma kupanda daraja ni kila baada ya miaka 3 hii ni kada yoyote ile hiyo 4 sijui wewe umetoa wapi?? .Kuna baadhi ya kada ili upate daraja fulani ni lazima ukapate mafunzo au uongoze Elimu kada hizo ni upande wa Mchumi,Mhasibu na utumishi kwa kada zingine sijajua inakuwa vipi.
Hata hivyo utofauti kati ya cheo na daraja Ni mdogo sana,kwani vina uhusiano kulingana na Muundo wa vyeo vya utumishi wa Umma.Mfano Kicheo mtu wa kada nyingine atakuita ''Mchumi'' lakini ukija kimuundo Unaitwa Mchumi daraja fulani!
 
Katika utumishi wa umma Cheo ni wadhifa anaopewa mtu .Mfano :Uliajiriwa kama mhandisi mitambo daraja la pili kisha baadaye ukapewa nafasi ya kukaimu umeneja ,UMENEJA NDIYO CHEO.
Daraja ni nafasi inayodetermine kiwango kipi ulipwe kulingana na elimu yako katika taasisi husika.Daraja mtu hupanda kila baada ya muda wa miaka mitatu au minne kama tu hr officer wako atakuwa active bila kujalisha umekwenda tena kujiendeleza au la!
Kama hujaelewa subiri takujibu nikiamka
Kaka kachukue standing order usome upya ,Hapo Mhandisi daraja la pili ndio cheo cha huyo Mhandisi-kwenye utumishi wa umma Cheo ni kazi yako inayokutofautisha na kada zingine ndio cheo.
Na kwa mfano wake maana yake Kwa uoande wa Halmashauri za Wilaya na Miji,manisipaa na MIkoa wenye vyeo ni MKurugenzi wa Halmasauri ya Wilaya ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,RAS,RC ndio wenye vyeo tu!
 
Unaweza ukatueleza kwa ufasaha tofauti ya kupandishwa cheo na kupandishwa daraja?

Mana kwa maelezo uliyotoa naweza sema hujaongelea kabisa upandishwaji wa vyeo na una tofauti gani na ule wa upandishwaji madarajaupoje.

Kwa uelewa wangu mtu hupanda daraja ndani ya cheo fulani. Na mtu hupanda cheo kwa kutoka cheo kimoja cha chini kwenda cheo kingine cha juu.
Mkuu kulingana na Standing Order inayotumika Mpaka sasa ulilolisema ndio upo sawa Mtu hupandishwa daraja ndani ya cheo fulani mfano Mhasibu daraja la kwanza-husomeka kama cheo kwenye standing order
 
Back
Top Bottom