Watumishi wa umma kutopanda vyeo/madaraja hadi wapitie mafunzo maalumu

Mpaka mafunzo? Huyo anayetoa mafunzo anakua amegewa mafunzo na nani? Na anayempa mafunzo mtoa mafunzo na yeye anakua amegewa mafunzo na nani? Na huyu aliyempa huyu mafunzo....

Kuna namna ya kupiga pesa au kutafuta sababu za kutoajiriwa zinaandaliwa.
Hizi ni dalili tosha za kutokutaka kupandisha madaraja wafanyakazi wa umma!
 
Nimeiona, hiyo ni kauli ya Bi Angela Kairuki na amesema ianze maramoja.
Walishaandaa budget ya hayo mafunzo mwaka Jana? Au ametoa tu kauli ili kudhurumu watu kwa kutowapandisha madaraja na vyeo? Ni sheria gani inayosema usimpandishe cheo au daraja mtumishi anayestahili kwa vile hujampa mafunzo maalum? Ma mbona haya mafunzo yamekuwa yakitolewa Mara kwa Mara makazin bila kuathiri upandaji wa vyeo na madaraja miaka yote?

Inamana kama serikali itakosa fedha kuwezesha hayo mafunzo kwa miaka 5 hakuna atayepandishwa daraja wala cheo?
 
Walishaandaa budget ya hayo mafunzo mwaka Jana? Au ametoa tu kauli ili kudhurumu watu kwa kutowapandisha madaraja na vyeo? Ni sheria gani inayosema usimpandishe cheo au daraja mtumishi anayestahili?

Inamana kama serikali itakosa fedha kuwezesha hayo mafunzo kwa miaka 5 hakuna atayepandishwa daraja wala cheo?
Kuna jambo halieleweki, hivi kwa hii serikali isiyoheshimu bajeti mbona kuna uwezekano mdogo sana wa kupandisha wafanyakazi madaraja? Mbona kwenye masharti ya ajira hili jambo halipo? Au wanatafuta migogoro na wafanyakazi? Huyu Angela anataka kulikoroga, ni wakati wa kumwelewesha utaratibu na ustaarabu wa kushughulikia stahili za wafanyakazi.
 
kwani kipya Hapo ni nini?? mbona mafunzo huwa watu wanaenda au ndio kutafuta kiki Mfano Afisa utumishi,Wahasibu kuna daraja hawezi kupata hadi akapate mafunzo vilevile Mchumi kuna daraja huwezi kupewa Mpaka Uwe na Masters
Kila kada huwa kunautaratibu fulani lazima mtumishi apite ndio apewe daraja labda kwa Walimu ndio sifahamu
Wewe inaonyesha huzijui kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Shortly:Mtumishi wa umma huajiriwa katika daraja fulani kulingana na elimu yake, na atatakiwe apande daraja moja kila baada ya miaka 3 au 4 kulingana na bajeti. Na endapo atakuwa na cheti cha elimu ya juu zaidi ya kile alichoajiriwa basi atatakiwa akiwasilishe baada ya miaka 3 ili apandishwe daraja stahiki na elimu yake.
Kuna utofauti kati ya neno CHEO na DARAJA katika utumishi wa umma.
Government is not a company in terms of circle.
 
Haya ndio matamko ambayo hatuyahitaji. Kwenye mikataba waliyojaza watumishi hakuna kipengere kinachosema mtumishi kupanda daraja anatakiwa ahudhurie mafunzo. Hivi hawa watu wakoje
 
Wewe inaonyesha huzijui kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Shortly:Mtumishi wa umma huajiriwa katika daraja fulani kulingana na elimu yake, na atatakiwe apande daraja moja kila baada ya miaka 3 au 4 kulingana na bajeti. Na endapo atakuwa na cheti cha elimu ya juu zaidi ya kile alichoajiriwa basi atatakiwa akiwasilishe baada ya miaka 3 ili apandishwe daraja stahiki na elimu yake.
Kuna utofauti kati ya neno CHEO na DARAJA katika utumishi wa umma.
Government is not a company in terms of circle.
Unaweza ukatueleza kwa ufasaha tofauti ya kupandishwa cheo na kupandishwa daraja?

Mana kwa maelezo uliyotoa naweza sema hujaongelea kabisa upandishwaji wa vyeo na una tofauti gani na ule wa upandishwaji madarajaupoje.

Kwa uelewa wangu mtu hupanda daraja ndani ya cheo fulani. Na mtu hupanda cheo kwa kutoka cheo kimoja cha chini kwenda cheo kingine cha juu.
 
Mafunzo maalum ni mafunzo gani? Kama kuna anae yafahamu atujuze ili tuone kama yana tija au la!!!
 
Unaweza ukatueleza tofauti ya kupandishwa cheo na kupandishwa daraja?
Katika utumishi wa umma Cheo ni wadhifa anaopewa mtu .Mfano :Uliajiriwa kama mhandisi mitambo daraja la pili kisha baadaye ukapewa nafasi ya kukaimu umeneja ,UMENEJA NDIYO CHEO.
Daraja ni nafasi inayodetermine kiwango kipi ulipwe kulingana na elimu yako katika taasisi husika.Daraja mtu hupanda kila baada ya muda wa miaka mitatu au minne kama tu hr officer wako atakuwa active bila kujalisha umekwenda tena kujiendeleza au la!
Kama hujaelewa subiri takujibu nikiamka
 
Hahaha, kairuki nae sio mda atajikuta anapigwa mawe nae amekua mtu wa blaah blaah nyingi sana kwenye utumishi wa umma, anatoa matamko wakt anajua anaetekeleza ni sizonje.

Ajira kesho oooh kesho kutwa. Hakuna awamu mawaziri wanapoteana kama hii
 
Hahaha, kairuki nae sio mda atajikuta anapigwa mawe nae amekua mtu wa blaah blaah nyingi sana kwenye utumishi wa umma, anatoa matamko wakt anajua anaetekeleza ni sizonje.

Ajira kesho oooh kesho kutwa. Hakuna awamu mawaziri wanapoteana kama hii
Kwa haya tunayoyaona kwa kweli neno fasaha kweny "wanapoteana".

Nchi imekuwa kama mji usio na Mjumbe nyakati zile za utawala wa awamu ya kwanza.
 
Hivi kwenye bajeti ya 2017/18 waliweka kipengere cha nyongeza ya mshahara,wanajua watujuze.Standing order na muundo huwa vinahitaji watu kupanda vyeo na vigezo vikubwa ni utendaji mzuri,muda wa kukaa kazi ni,labda wagavi,wahasibu hutakiwa kuwa na Sifa za umahiri hasa kwa nafasi za uandamizi.labda wabadili sheria na taratibu ili kigezo cha mafunzo kiingie.Pia watapelekaje watu mafunzo wa kama hâta pesa za Matumizi ya ofisi ni shida
 
Ishu ya uhakiki wa vyeti imeishia kwa bashitee, wanaibuka na mafunzo maalumu ili waendelee kuchelewesha kutupandisha madaraja na mishahara yetu. Kama kuna mtumishi wa umma alimpigia Magu kura na amchague tena 2020.
Vyeti hawana courage ya kuviongelea tena! Maana itakuwa kama wanamsema mwanamfalme "le Prince"
 
Jana nikiwa natazama taarifa ya habari kupitia ITV niiona taarifa hii ambayo waziri Kairuki alikuwa akielezea kutopanda kwa madaraja na vyeo kwa watumishi mpaka wawe wamepitia MAFUNZO katika chuo cha utumishi.
 
Back
Top Bottom