Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,309
- 9,623
Ni ukweli usiopingika kwamba sekta ya mafuta na gesi imefungua fursa kwa wawekezaji wakubwa na wadogo katika taifa letu, na kutoa mwanya kwa wale wanaotaka kuwa wajasiriamali katika sekta hii.
Sekta hii imendelea kutengeneza utajiri kwa wawekezaji mbalimbali waliojizatiti kuwekeza hasa wawekezaji wakigeni.
Lakini inavunja moyo sana asilimia kubwa ya Watanzania bado wako kwenye benchi wanasubiri kwa sababu ya ukosefu wa taarifa ambazo ndio leo nakuja kuzitoa kwenye jukwaa hili waziwazi.
Watanzania wajasiriamali tunaakili sana lakini tunacheza kidogo sana katika tasnia ya mafuta na gesi.
Ukweli mchungu ni kwamba uchumi wetu wa ndani utaweza kubadilishwa na kuwa bora zaidi kwa ushiriki wetu mkubwa kwenye uwekezaji katika hii Sekta wala sio wageni.
Kwa nini tunasubiri hadi sasa wakati wengine wamechukua maeneo yote mazuri kwenye tasnia ya mafuta na gesi? Ila bado hatujachelewa.
Ingawa fursa katika tasnia ya mafuta na gesi zinaweza kuonekana kama zinahitaji mtaji mkubwa, lakini kuna fursa nzuri tu za uwekezaji mdogo katika tasnia hii.
Haijalishi ukubwa wa mfuko wako, ukitazama kwa umakini, bado utagundua fursa za biashara ndogo ndogo unazoweza kuwekeza na kuleta ushiriki wako katika sekta hii.
1. Muuzaji wa jumla wa gesi ya kupikia ya LPG
Msambazaji mjasiriamali anaweza kutuma maombi ya kuwa mfanyabiashara mkuu wa kampuni ya uuzaji wa mafuta ambaye atafanya kazi nao kwa sehemu ili kuuza gesi (LPG), majiko, na vifaa vingine muhimu vinavyohitajika kwenye mfumo wa jiko la gesi la kupikia
Mtoa huduma wako (kampuni kubwa ya uuzaji wa mafuta) atakupa mitungi iliyojaa gesi kwa bei ya jumla ya chini kabisa, na wewe, utauza na kupata kiasi cha faida cha kawaida, na unaweza kuamua kuuza kwa bei ya rejareja ili kupata faida mara mbili na zaidi.
Kama muuzaji bora, itabidi uhakikishe kwamba una mzigo wa kutosha wa mitungi ya gesi ya LPG wakati wote ili uweze kuwahudumia wateja wako kwa wakati. Pia unatakiwa angalau uwe na mtoa huduma mmoja wa uhakika ili kuhakikisha unakua na mzigo wa kutosha wakati wote. Ili kufanya biashara hii bila kusuasua utahitaji uwekezaji wa kati ya Tsh 35,000,000 hadi Tsh 60,000,000 wakati unaanza.
2. Kuanzisha kituo kidogo cha kujaza mafuta chenye pampu mbili katika maeneo ya vijijini.
Mahitaji ya mafuta ya petroll na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka, ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama "boda boda".
Wizara ya nishati imetengeneza mazingira wezeshi ya kutoa mkopo na EWURA wametengeneza mwongozo wa jinsi ya kuanzisha vituo vya kujaza mafuta vijijini tena kwa mtaji mdogo kabisa.
Hivyo kama unatafuta fursa za biashara kuanzisha kituo kidogo cha mafuta maeneo ya kijijini kunaweza kuwa chaguo bora zaidi. Kiukweli yapo maeneo ya vijijini mimi nayafahamu ni potential sana kuanzisha biashara ya vituo vya mafuta.
Unapochagua eneo la kujenga kituo cha mafuta kijijini hakikisha eneo hilo lina shughuli nyingi za kiuchumi zilizo changamka kama vile uchimbaji wa madini, biashara, usafirishaji, kilimo na uvuvi. Bila kusahau hakikisha lina idadi kubwa ya magari, pikipiki, mashine mbalimbali na bajaji.
Zaidi ya hayo, kituo chako cha mafuta si lazima kiwe mjini kama Dar es salaam au Mwanza. Unaweza kuanzisha kituo kidogo cha mafuta katika maeneo ya vijijini. Makampuni makubwa ya mafuta yanapendelea kujenga vituo maeneo ya mijini. Hivyo huwa wanapuuza maeneo haya ya vijijini. Kuwa na kituo chako kidogo cha petroli au dizeli katika maeneo ya vijijini sio ghali sana kukianzisha na kukiendeleza na bado kinakuhakikishia faida endelevu. Kinachofanya iwe ngumu kuanzisha kituo cha kujaza mafuta maeneo ya mjini ni viwanja kuwa ghali sana wakati vijijini utapata kiwanja kwa bei ndogo sana. Ujenzi pia hautakua ghali maeneo ya vijijini ukilinganisha na mijini.
3. Kuwa wakala
Kama wakala utafanya kazi ya kuwaunganisha wasambazaji wa bidhaa au huduma na kampuni ya mafuta na gesi pamoja. Kama wakala jukumu lako ni kutafuta wateja wa hiyo bidhaa au huduma na kwa kawaida utapata kamisheni kutokana na huduma zako.
Kwa sehemu kubwa, mawakala hufanya kazi kwa wasambazaji. Kwa mfano, unaweza kuzitafuta kampuni za mafuta na gesi nchini zinazohitaji kununua aina fulani za bidhaa au huduma. Ukishafahamu unawatafuta wasambazaji wa bidhaa na huduma hizo ndani au nje ya nchi. Ukishawapata unaomba kuwawakilisha kwa wateja ambao ni hizo kampuni za mafuta na gesi zilizopo nchini.
Lakini wakati mwingine unaweza kuwa wakala wa kampuni inayosambaza mafuta au gesi nchini. Wewe ukafanya kazi ya kuitafutia wateja wa bidhaa au huduma zao ukalipwa kwa kamisheni.
4. Duka la kuuza Gesi ya Kupikia kwa rejareja
Soko la gesi ya kupikia (LPG) linazidi kukua kwa kasi katika taifa letu kutokana kuongezeka kwa matumizi makubwa ya LPG kama chanzo cha nishati ya kupikia katika maeneo ya makazi ya watu, na kuchukua nafasi ya mkaa na kuni.
Chaguo la kwanza la kuingia katika biashara ya gesi ya kupikia (LPG) ni kuanzisha duka la rejareja la gesi. Ili kuanzisha biashara hii ya gesi ya kupikia unahitaji angalau mitingi 22 hadi 35 ya gesi (ikiwezekana mitingi ya 15Kg na 6Kg ya gesi). Pia unahitaji regulators, hose na weighing scale (mizani ya kupimia). Utanunua gesi ya kupikia kutoka kwa wauzaji wa jumla na kuiuza kwa watu rejareja.
Huwa najiuliza swali wanapataje faida wakiona kuna ushindani mkubwa kwenye biashara hii. Lakini jibu ni jepesi sana, ukweli ni kwamba, kadiri idadi ya kaya zinazotumia gesi ya kupikia zinavyoongezeka, na mahitaji nayo yanaongezeka, na wateja zaidi huongezeka.
5. Usafirishaji wa mafuta na gesi au bidhaa za petroli
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa za petroli yaani mafuta na gesi katika nchi za Afrika Mashariki, usafirishaji wa bidhaa hizo (kwa mfano, petroli, dizeli, mafuta ya taa na bidhaa nyingine za petroli kama vile mafuta ya vilainishi) imefungua fursa nzuri sana ya uwekezaji kwa wajasiriamali.
Biashara hii inahusu kutumia malori kusambaza bidhaa za petroli na gharama za usafirishaji zitategemeana na umbali wa kupeleka bidhaa hizo na ujazo wa bidha husika.
Utalazimika kupata leseni kutoka EWURA ili kuruhusiwa kusafirisha mafuta na gesi nchini au nchi jirani. Pia utalazimika kununua lori na kuajiri dereva aliyehitimu na mwenye uzoefu ambaye atasafirisha bidhaa za petroli hadi mahali zinapotakiwa kutoka kwa wauzaji wa jumla kwenye bohari.
Ningependekeza uanze na usafirishaji wa bidhaa za petroli kutoka bohari hadi vituo vya kujaza mafuta ndani ya nchi. Biashara yako itakapopanuka, unaweza kupata leseni mpya ya kusafirisha mafuta hadi nchi jirani za Uganda, Kenya, Rwanda na Kongo DRC.
6. Huduma ya Matengenezo
Huu ni mradi mwingine wenye faida kwa sababu makampuni ya mafuta na gesi yana vifaa vingi, ikiwa ni pamoja na mabohari, mitambo ya gesi, matenki, mitambo ya kuzalisha umeme, visima vya gesi. Kwa hiyo, lazima watahitaji kurekebisha na kufanyia matengenezo. Na hapo ndipo unapoingia.
Hata hivyo, swala muhimu zaidi, utahitaji ujuzi wa kutosha wa kiufundi na ukusanye timu imara ya wahandisi na mafundi wa kutoa huduma hii ili kuwaridhisha wateja wako kikamilifu.
7. Uanzishaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Mitungi ya Gesi.
Najua lazima itakuvutia kufahamu kwamba Tanzania inaagiza asilimia kubwa ya mitungi ya gesi kutoka India.
Hivyo hii inatoa fursa kubwa kwa wajasiriamali wanaotaka kuanzisha viwanda vya kutengeneza mitungi ya gesi hapa nchini.
8. Kuanzisha kampuni ya Ushauri
Ingawa makampuni mengi ya ushauri katika taifa letu yamejielekeza kwenye uhandisi na ushauri wa miradi, lakini kuna pengo katika soko ambalo linahitaji mwongozo, msaada, na rasilimali kwa wawekezaji wanaomiliki au wanaotaka kuanzisha biashara katika sekta ya mafuta na gesi.
Hivyo, unaweza kujaza pengo hili kwa kuanzisha kampuni yako ya ushauri na kutoa msaada wa kibiashara kwa watu wanaotaka kuanzisha biashara endelevu katika sekta ya mafuta na gesi.
Biashara hii ya ushauri inafaa zaidi kwa watu ambao hawana mtaji mkubwa wa kujitosa katika biashara ghali ya mafuta na gesi lakini wanao ujuzi wa kina uliojikita katika sekta ya mafuta na gesi.
9. Kiwanda cha Kuhifadhi Gesi ya kupikia (LPG)
Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji katika taifa letu. Aina hii ya uwekezaji ina vyanzo vingi vya mapato. Kama muuzaji mkubwa wa gesi ya kupikia, unaagiza, kuhifadhi na kuuza gesi ya kupikia kwa wafanyabiashara wakubwa, wamiliki wa vituo vya kujaza gesi, na unaweza pia kuuza kwa wingi kwa wateja wa kibiashara kama vile hoteli, nyumba za kulala wageni, shule na vyuo.
Zaidi ya hayo, unaweza kupata mapato ya ziada kwa kutoa huduma za ufungaji wa matanki, mitandao na bomba kwenye shule na hoteli zinazohitaji kutumia gesi ya kupikia.
Mahitaji ya awali ya mtaji ya kuanzisha biashara hii ni makubwa kidogo: utahitaji si chini ya TZS 1.5 bilioni. Lakini, biashara ina faida zaidi kwani utauza gesi ya kupikia kwa wingi.
10. Au nenda kwenye uuzaji na usambazaji wa pampu za mafuta na gesi.
Kama umewahi tembelea kituo cha mafuta / kituo cha kujaza mafuta, utaona wanaouza petroli, dizeli, mafuta ya taa au gesi kwa rejareja wanatumia pampu kuuzia mafuta.
Hii inaonyesha kuwa kuna soko la pampu za mafuta na gesi katika taifa letu.
Itaendelea......
Mengineyo:
Agiza gesi ya kupikia mahali ulipo kupitia hapa: Campus City Shopping Mall - Online Shopping for Popular Electronics, Fashion, Home & Garden, Toys & Sports, Automobiles and More.
Kama unahitaji msaada wa kuandika na kuhariri documents zako mbalimbali, tunayo habari njema kwako!
Bright and Genius Editors wapo hapa kukusaidia.
Tunatoa huduma za uandishi na uhariri wa documents za aina zote.
Wasiliana nasi kwa njia yoyote upendayo:
Piga/WhatsApp : +255687746471/+255612607426
WeChat ID: bandg_editors
Barua pepe: bandg.editors@gmail.com/submit@bgeditors.com/contact@bgeditors.com
Pia, unaweza kutembelea tovuti yetu www.bgeditors.com, Bright & Genius Editors kujifunza zaidi kuhusu huduma zetu na kufanya maombi yako moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu.

Fursa za Biashara Zenye Faida Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Katika Taifa letu