Watanzania acheni unafiki

Sawa yote uliyoyasema ni kweli kabisa na mimi nakubaliana na wewe kwa 100% huyu rais atufai. Ila swali langu ni hili jambo alilolifanya la kuchunguza mchanga ni baya?
 
Mkuu ulikuwa unataka nini?.. Kwa hio kama zamani walilifumbia macho hili swala then,na utawala huu wafumbie macho????
Magufuli naye ni mpya kwenye CCM?

kipindi kile mikataba ya madini inapitishwa BUNGENI hakuwepo?

Si ndio huyu huyu aliyekuwa akipinga kwa nguvu zote hoja za wapinzani kuhusu mapungufu ya mikataba hii?
 
Hivi unajua sera za Magufuli na mikakati yake ni tofauti na JK?!Kwahiyo kilichomshinda JK basi JPM akiache na yeye kisa tu Kikwete kilimshinda?!

Munakera sana na umbumbumbu wenu,hebu nendeni mukasome huko ata google jamani!!aibu aibu !!Elimu,Elimu
mkuu naona inawezekana hili jambo kwako ni geni ila naomba nikukumbushe kuwa wabunge wa upinzani walilipigia kelele sana jambo hilo na rais akiwa ndani ya baraza LA mawaziri wa awamu zilizopita akishiriki kutunga na kupitisha sheria zilizoruhusu Mchanga huo kutoka.Kama sio unafiki ninini?
Kwa nini hakupinga kipindi kile sheria na kanuni hizo zikipitishwa? Acheni ujinga wala hapaswi kusifiwa ila anapaswa kulaumiwa coz ni yeye pia aliyehusika tukafika hapa tulipofika,wala sio suala la kumbebesha mzigo Mhongo hapana.
Kama yeye amedhamiria kweli awaondolee kinga ya kushitakiwa marais waliohusika katika kadhia hiyo.
Zaidi ya hapo uhuni mtupu,wamekula wamemaliza sasa wanatutafutia mchawi.
 
Wewe ndiyo umekurupuka kunijibu paka huo mchanga kusafirishwa kuna mikataba iliyopitishwa bungeni na huyu magufuli alikuwa unadhani walikurupuka tu kusafirisha siku nyingine usiwe na mihemko
Acha kuchanganya mambo, mikataba inapitishwa bungeni???
 
Umetoka instagram huko kwa chizi wenu mange ndio unatulea povu lako humu!we unajua nini kuhusu madini na usafirishaji wake?! Kuna mkataba wowote unaujua kuhusu usafirishaji?!

Wewe na Magufuli nani anajua zaidi?!hivi unaujua uzembe wa Muhongo katika hili kweli au unapovuka tu!?kama hujui ni heri tu ukakaa kimya!!

Kwahiyo magufuli asikemee chochote kile kibaya kinachotokea kwasababu tu itaonekana makosa yalifanyika nyuma kwa hiyo viongozi wasasa hawahusiki basi wasiwajibishwe?!bogus kabisa,mnyonge mnyongeeni haki yake mpeni,Muhongo alifanya uzembe uliotukuka...

Ahsante Magufuli
Karogwa huyu, hizi akili za kushikiwa hivi unaanzaje kukejeli kwa inshu kama hii, of kozi hatukatai kukosoa pale palipo na mapungufu sasa mtu anakuja kuzungumzia unafiki as if ni big issue. Hivi kuna mwanasiasa ambaye si mnafiki???
 
Kama ulikuwa hujui taratibu za kiutumishi ni kwamba hakuna kitu kinachoitwa sikuwa mimi au sikuwepo. Unapopewa majukumu ni pamoja na kuyafanyia kazi yanakuhusu na ndio maana unaweza kukuta waziri anatemeshwa leo na kesho anachaguliwa mwingine na anakwenda kujibu maswali bungeni na huwezi kusikia waziri anasema sikuwa mimi.
Muhongo anawajibishwa katika makosa ya kiutendaji haya yote alitakiwa kuyajua na kuyachukulia hatua na si hadi kusubiri tume.
 
Back
Top Bottom