Seneta Wa Mtwiz
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 3,622
- 4,138
Hapa napoishi tumeingia mkataba na kampuni moja ya kibongo kuhusu suala la ulinzi usiku. Hawa walinzi wanatakiwa kuingia saa kumi na mbili ila wao wanaingia saa yoyote hata saa mbili. Mfano leo hata hajaja na kama hawaji hata hawatoi taarifa hadi upige kwa mwenye kampuni nae anaanza kushangaa afanye mbinu alete mwingine blah blah kibao yaani.
Inaelekea mwenye kampuni hawalipi vizuri kwaiyo wanaacha kazi inabidi abadilishe mara kwa mara.
Hofu yetu ni kwamba kwa wiki eti wanaweza kuja hata watu wanne tofauti tofauti. Sasa sisi hatupendi watu tofauti tofauti waje hapa kwetu maana tunaona kama ni hatari kwetu. Mwenye nyumba ambae ni boss wangu kazini yeye hata hajui hii issue yeye kanikabidhi hapa kila kitu yeye hakai bongo hata kuwalipa nalipa mimi na mkataba nimesaini mimi.
Nimevumilia kumsemea huyu bwana apigwe chini tutafute wengine ila sasa nimechoka naona tu niwe mkweli.
Eti wadau ni sawa walinzi kubadilishwa kila siku jamani?
Walinzi wazuri wanatakiwa waweje ili nikiingia mkataba mpya nitoe hayo masharti maana nimewachoka hawa wananiletea lawama.
MKUU,
LINDO KAMA HIZO TUPE SISI WAMASAI,
TUNAHAKIKISHA TUNALINDA KWA MBINU ZA KIMORANI NA KILAIBONI!
TUNALINDA TUKIWA NA #Mama_Yeyoo PEMBENI,
AMBAPO HATUTOKI MTU SAA 24,
SISI TUKIONDOKA,
YEYE ANAKUWEPO AKILINDA SIME, MKUKI, NGAO, UPINDE NA MISHALE.
NIPE HIYO KAZI MKUU.