Wasomi wanena: Kuchaguliwa kwa Magufuli ni pigo kubwa kwa UKAWA!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,847
43,336
Wasalaam wana jamvi!
Baada ya chama cha mapinduzi kumteua Dr Magufuli kupeperusha bendera yao kwenye uchaguzi mkuu hapo octoba kwakweli watu wengi wakiwemo wananchi wamefurahishwa na uteuzi huo na kusema hakika CCM wamecheza kama Pere!

Wasomi nao hasa wahadhiri wa chuo cha Dares-salaam bila kuwasahau wachambuzi wa siasa hawakusita kusema wazi kuwa CCM wamepatia kweli kweli na hakika UKAWA watapata wakati mgumu au ndoto yao ya kwenda ikulu imeyayuka kabisa maana magufuli ni chaguo zuri na ana uzika ndani na nje ya CCM!

Wasomi wengine nao hawakuwa nyuma kuweka wazi kuwa wakati UKAWA bado wako kwenye malumbano ya kupata mgombea wa Urais..wenzao CCM wameweka mtu wa kuotea mbali ambaye hawezi kuangushwa na Mgombea yeyote wa UKAWA!

Wasomi hao waliendelea kusema kuwa UKAWA hawakutegemea kama CCM itaweka mgombea kama Magufuli ..wao akili zao zilikuwa kwa Lowasa na Membe sasa ujio wa Magufuli ni pigo kubwa kwao na wana kazi kubwa sana kuwashawishi wananchi wamnyime kura Dr Magufuli!

Karibuni Wana jamvi!
Source : ITV
 
Haihitaji kua genius kujua kua Magufuli is the best candidate this country have ever had

Huyu mtu kafika alipo kwa CV yake na wala sio umaarufu.

Alijenga jina lake kiutendaji ambapo ilitegemewa achukiwe na wengi kwa kubomoa nyumba za waliojenga katikai ya bara bara lakini ndio walimpenda zaidi.

Angalia hata kutangaza kwake nia

Hakurusha live

hakua na makundi

Hakusema kitu kabla hajasoma yaliyoandikwa kwenye fomu

Hakua na mbwembwe

Aliongozana na mlinzi na dereva tu

Hakuhitaji wadhamini maelfu wala mabasi yenye picha zake

Huyu jamaa yeye alipiga kimya kimya kama anaua nyoka na kashinda kwa kishindo kikubwa mpaka yeye mwenyewe kashangaa

CCM ni zaidi ya uijuavyo. Uachaguzi wake ni kama ule wa papa tu. SIRI MNO!

Rais Kikwete kaweka historia ya kutuachia Rais tumtakae bila gharama wala makundi
 
Hao wasomi walizungumzia lolote kuhusu tume huru ya uchaguzi? Tatizo sio mgombea mzuri au mbaya wa ccm bali ni tume huru ya uchaguzi. Kwa tume hii hata mgombea wa ccm akiwa prof maji marefu ana uwezo wa kushinda. Kama kweli ccm na wasomi wanaamini wamepatia kwa mgombea tuweke tume huru kama ccm haijapoteana.
 
UKAWA wao ndio walitakiwa kudai hayo kabla ya bunge kuisha wao wakaona hilo halina umuhimu! Wasomi walikuwa wanafanya uchambuzi juu ya wagombea...
 
UKAWA wao ndio walitakiwa kudai hayo kabla ya bunge kuisha wao wakaona hilo halina umuhimu! Wasomi walikuwa wanafanya uchambuzi juu ya wagombea...

Acheni utapeli nyie watu wa CCM. Tunauliza maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005 wakati anaingia madarakani yako wapi?
 
UKAWA wao ndio walitakiwa kudai hayo kabla ya bunge kuisha wao wakaona hilo halina umuhimu! Wasomi walikuwa wanafanya uchambuzi juu ya wagombea...

wadai mara 2? Walipokutana na rais siku ya mkutano wa vyama siasa na rais akaahidi kutekeleza. Halafu kama kweli kila wanachodai ukawa ccm wanatekeleza mbona walitaka mswaada wa ges na petrol usuburi na bado mkagoma.
 
Wewe mhuni wa UK ndio umerudi tena baada ya kupotea muda mrefu humu JF? CCM ni ile ile, mfumo ni ule ule, sera ni zile zile, na viongozi ni wale wale. Hakuna jipya ndani ya CCM. Acheni kutapeli watu. Mtueleze Watanzania maisha bora tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005, yapo leo hii?
Mkuu hata ukitukana ukweli utabaki pale pale

Mmepigwa ngumi ya pua....

Kama unabisha jenga katikati ya barabara....
 
wadai mara 2? Walipokutana na rais siku ya mkutano wa vyama siasa na rais akaahidi kutekeleza. Halafu kama kweli kila wanachodai ukawa ccm wanatekeleza mbona walitaka mswaada wa ges na petrol usuburi na bado mkagoma.
Umesahau kuwa walipo ahidiwa lakini wao waliendelea kususa na hata kwenye bunge hili wameshindwa kuendelea kudai na kukumbusha! hatuna wapinzani serious..
 
anaweza kumfikisha jk mahakamani kwa kesi km za escrow hela zetu na vitalu vya gesi km kweli mnamkubali ama maslahi ya chama kwanza km ilani ilivyo
 
Mimi nimekuuliza swali wewe hujajibu bado. Swali langu ni hili, yale maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005 wakati anaingia madarakani yako wapi?

Mkuu hilo swali lako lihifadhi kwanza utawauliza watanzania baada ya Oktoba 25 sasa hivi hutapata majibu!
 
Endelea kusubiri na uvivu wako!Najua unaweweseka jiandae kwa mchakamchaka!

Wewe jibu swali mkuu. Tatizo Watanzania mnapenda sana kwenda kwa mihemuko na hisia zaidi. Manapenda kutajiwa tu matukio na sio kujadili matukio; mnapenda kuambiwa namba na sio hesabu. Swali langu ni hili, yale maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005, Kikwete anapoondoka mwaka huu, je hayo maisha bora yamepatikana? CCM ni chama kile kile, sera ni zile zile, mfumo ni ule ule, na viongozi ni wale wale. Hakuna jipya ndani ya CCM. Watanzania safari hii hatudanganyiki! Hata aje Malaika ndani ya CCM, hawezi kuleta mabadiliko yoyote
 
Mkuu hilo swali lako lihifadhi kwanza utawauliza watanzania baada ya Oktoba 25 sasa hivi hutapata majibu!

Kwa nini nisipate majibu wakati ilani ya 2010-2015 ndio inaisha hivi? Wakati ni sasa. Tatizo nyinyi ni matapeli, mnadhani watu tumesahau mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani
 
anaweza kumfikisha jk mahakamani kwa kesi km za escrow hela zetu na vitalu vya gesi km kweli mnamkubali ama maslahi ya chama kwanza km ilani ilivyo
Hakuna kosa la jk katika yote uliyo yataja..!
 
Mimi nimekuuliza swali wewe hujajibu bado. Swali langu ni hili, yale maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005 wakati anaingia madarakani yako wapi?
Wanao fanya kazi kwa bidii maisha bora wanayapata na watapa..!

Asiye fanya gani na asile "
 
Wasomi nao hasa wahadhiri wa chuo cha Dares-salaam bila kuwasahau wachambuzi wa siasa hawakusita kusema wazi kuwa CCM wamepatia kweli kweli na hakika UKAWA watapata wakati mgumu au ndoto yao ya kwenda ikulu imeyayuka kabisa maana magufuli ni chaguo zuri na ana uzika ndani na nje ya CCM!

Wasomi wengine nao hawakuwa nyuma kuweka wazi kuwa wakati UKAWA bado wako kwenye malumbano ya kupata mgombea wa Urais..wenzao CCM wameweka mtu wa kuotea mbali ambaye hawezi kuangushwa na Mgombea yeyote wa UKAWA!

Wasomi hao waliendelea kusema kuwa UKAWA hawakutegemea kama CCM itaweka mgombea kama Magufuli ..wao akili zao zilikuwa kwa Lowasa na Membe sasa ujio wa Magufuli ni pigo kubwa kwao na wana kazi kubwa sana kuwashawishi wananchi wamnyime kura Dr Magufuli!

Hamna jipya hapa .. typical wasomi uchwara wa TZ ... kuropoka tu kama kawaida yao. Kwani wanamlinganisha na mgombeaji gani wa ukawa?
 
Back
Top Bottom