Wasomi wanena: Kuchaguliwa kwa Magufuli ni pigo kubwa kwa UKAWA!

Kwanza PhD yake ina mashaka. Muulizeni kwanza zile nyumba alizowapa supervisors wake kwa sababu zipi kabla hata ya kumaliza PhD?
Onesha hayo mashaka acha maneno mengi Bavicha!
 
Hamna jipya hapa .. typical wasomi uchwara wa TZ ... kuropoka tu kama kawaida yao. Kwani wanamlinganisha na mgombeaji gani wa ukawa?
Wanaonekana wameropoka kwakuwa wanaye muongelea ni wa CCM lakini angekuwa ni wa UKAWA unge wapongeza.....
 
Wasomi ni akinanani? Hawa wanaojipendekeza ili wapate ulaji au wapi?! Bola ungesema labuda wakulima au wavuvi!
 
Uzuri wakati mie nasoma masters yeye alikuwa anasoma PhD. Ni wewe peke yako ndiyo hujui, pole sana.
Naona unaendelea kuongea maneno matupu! Nasema tena eleza hayo mashaka yako!
 
Wasomi ni akinanani? Hawa wanaojipendekeza ili wapate ulaji au wapi?! Bola ungesema labuda wakulima au wavuvi!
Hivi hizo sifa wangempa mgombea wa UKAWA unge uliza hayo maswali?
 

Ruttashobolwa sasa wasomi wakisema ndiyo inakuwaje? Tanzania ina wasomi wangapi? Wasomi hao ni wangapi mpaka waweze kusemea nafsi za watanzania milioni 45?

Ungekuwa unajua kwanza maana ya neno msomi basi usingethubutu kukurupuka hayo unayoyasema.

Chris Lukosi wewe kwanza si raia wa Tanzania sasa hizi siasa za nchi hii wewe zinakuhusu nini? Pia kwanza nani kakwambia uongozi ni CV? Pili kuchukua kwake fomu kimya kimya ndiyo imekuhalalishia wewe kuwa Magufuli ni kiongozi bora?

Kuna mzee mmoja alishawahi kuniambia ukifika au ukipata kuishi hizo nchi za ulaya hata usipo kwenda shule mazingira tu yatakufanya kuwa tofauti sana na vijana wengi wa hapa nchini lakini nikitazama maandiko yako mengi humu JF napingana kabisa na kauli ya yule mzee.

Acheni mambo ya kishabiki hii nchi ilipofika ni pabaya na inahiaji mabadiliko na mabadiliko hayawezi kuletwa na CCM pekee.
 
UKAWA wao ndio walitakiwa kudai hayo kabla ya bunge kuisha wao wakaona hilo halina umuhimu! Wasomi walikuwa wanafanya uchambuzi juu ya wagombea...

Wakiitwa wasomi nao wataenda eti wasomi wamevumbua nini wakati hata leso ya mkononi made in china .
 
Ngoja tupate huduma yake,ila kwa ccm tuisha jalibia sana,naona kama imefika mwisho.hakuna namna lazma tubadilike.
 
Hivi hizo sifa wangempa mgombea wa UKAWA unge uliza hayo maswali?

Shida kubwa ya watanzania ni mfumo/chama na sio mtu anaekubalika tu,maana tuliwaona watu na uwezo wao lkn mfumo wa kifisadi ukawameza!
Sasa ndomaana najuwa wengi mnaojiita wasomi ni wachumia tumbo na swala la ukawa ni mfumo ambao unaonekana kwa uborawake.
 
wasomi hao hao kupitia REDET walisema Lowasa anaongoza kinyang'anyiro cha urais akifatiwa na Slaa....
 

UkAWA hawakutegemea kuwa magufuli ndo atakuwa mgombea Urais? Ninadhani UKAWA walijiandaa kwa mgombea yeyote kati ya wale watia nia 38.Mgombea yeyote alikuwa na chance ya kushinda.Anyway UKAWA wapo kimya hatujui nini kinaendelea
 
Labda atasikiliza pia yale malalamiko ya wanaoishi mbali na kampuni yenu ilipo ili wasitozwe pesa nyingi kama mtu anatokea North Engalnd, Scotland au NI etc kutuma gari TZ. MOT itatosheleza au? Na MOT kwa magari yote au? Niliwasoma wadau wengi wa huko waliongelea humu.

Naona umerudi sasa uchaguzi huo ndio unaanza kuwaka waka.
 
Back
Top Bottom