Wasiopenda udhibiti wa uandishi wa habari wana malengo ya kisiasa au kibiashara?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,484
7,292
Kila leo utasikia waandishi wa habari wanalalamika kwamba hawana uhuru. Utasikia kila siku wakilalamika kwa sababu wao ndio watoa habari. Usifanye kosa ukadhani hilo ndio tatizo kubwa nchini.

Waandishi wakizungumzia kazi yao utafikiri ndio inaleta maendeleo nchini kumbe wengi ni ajira na wengi ni biashara tu. Ili ufanikiwe kibiashara lazima uuze sana. Na ili uuze sana lazima uandike habari zinazopendwa au kusisimua sana.

Inatokea wakati mwingi waandishi wa habari wanaandika uzushi au uongo ili wauze habari. Wengine wanakua na malengo ya kisiasa kwa kueneza fikra za kigeni au utamaduni usiofaa. Kwa vyovyote chama na serikali iliyoko madarakani itakua na mwelekeo wake kisiasa kimaadili na kitamaduni kulinda.

Ndio maana utaona kila kukiwa na mabadiliko ya kiongozi nchini waandishi wa habari wanaibuka kudai uhuru wa uandishi. Shida kubwa malengo yao ya kibiashara yanapingana na malengo ya serikali au maslahi ya kijamii.

Kwa hivyo wanakuwa na matumaini kiongozi aliyeingia ataweza kuruhusu maslahi ya kibiashara kutawala yale ya kisiasa kimaadili kiitikadi na kadhalika ya taifa.
 
Kila leo utasikia waandishi wa habari wanalalamika kwamba hawana uhuru. Utasikia kila siku wakilalamika kwa sababu wao ndio watoa habari. Usifanye kosa ukadhani hilo ndio tatizo kubwa nchini.

Waandishi wakizungumzia kazi yao utafikiri ndio inaleta maendeleo nchini kumbe wengi ni ajira na wengi ni biashara tu. Ili ufanikiwe kibiashara lazima uuze sana. Na ili uuze sana lazima uandike habari zinazopendwa au kusisimua sana.

Inatokea wakati mwingi waandishi wa habari wanaandika uzushi au uongo ili wauze habari. Wengine wanakua na malengo ya kisiasa kwa kueneza fikra za kigeni au utamaduni usiofaa. Kwa vyovyote chama na serikali iliyoko madarakani itakua na mwelekeo wake kisiasa kimaadili na kitamaduni kulinda.

Ndio maana utaona kila kukiwa na mabadiliko ya kiongozi nchini waandishi wa habari wanaibuka kudai uhuru wa uandishi. Shida kubwa malengo yao ya kibiashara yanapingana na malengo ya serikali au maslahi ya kijamii.

Kwa hivyo wanakuwa na matumaini kiongozi aliyeingia ataweza kuruhusu maslahi ya kibiashara kutawala yale ya kimaadili kiitikadi na kadhalika ya taifa.
aliyeelewa naomba anifafanulie!.
P
 
Back
Top Bottom