Wapo wapi? Ama kweli jana sio leo na leo sio kesho

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,027
62,578
WAPO WAPI? KWELI JANA SIO LEO; NA LEO SIO KESHO

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Maisha yanahitaji upendo. Ukijifanya mjanja subiri wakati wako maisha yatakapokufanya Mpumbavu

Yajana yanachekesha lakini pia yanaumiza. Lumaanisha ya leo wapo wanaoumia na kucheka lakini kesho itakuwa kinyume chake. Hata hivyo wapo salio hela jana na bado hata leo wanacheka. Pia wapo walioonja joto la jiwe Jana na bado wanakula Msoto mkali.

Maisha ni mabadiliko. Lolote huweza Kubadilika kwa yeyote kwa muda wowote. Hii tukilijua basi tutaishi kwa tahadhari tukipendana.

Unakumbuka Jana? Pengine hukumbuki vyema, ngoja tukumbushane; mtaniwia radhi pale hisia zangu zikinizidi mpaka kufikia kucheka au kulia. Haya nikukumbushe;

Siasa siasani, visa na mikasa kwenye sahani, kuchinjana na kukatana shingoni. Wabezaji wamegeuka Wabeza, washika jambia leo wanatimuka mbio Kwa hofu. Ole wale makonda waliojifanya wamiliki WA gari ilihali wao ni washika pesa Tu za Maboss wao. Dooh!

Wapo wapi wale waliokuwa na TV pekee yao kijiji kizima? Hawa walikuwa wengi wao wanasheria ngumu kweli, watoto wao walikunyanyasa? Wapo wapi leo ikiwa jana ilikuwa hivyo?

Wapo wapi wale waliokuwa wakitoka likizo Dar es salaam wakituringishia na kutuona washamba kisa hatujaenda Dsm. Shuleni wakitusumbua na Stori zao za viunga vya Dsm. Unajua walipo kwa sasa au unataka nikujuze?

Unawakumbuka wale masister Duu tukiwa under twenty twasoma walivyosumbua? Walikuwa hawali Kande🤣🤣 wala chakula cha shule. Madada wa biskut, chocolate na juisi. Unajua wanachokula sasa hivi??😀😀

Vipi wale vidosho tukiwa under 20 waliojaliwa maumbo na uzuri usiosemeka, walivyoleta tafrani pindi wakipita mitaani wakitingisha Makalio yao. Unajua walipoishia? 🤣🤣

Wapi ma-bitozi nyangema AKA mabishoo milegezo waliokunyang’Anya Demu wako enzi hizo unajua walipoishia?

Wapi walipo wale waliokuita mshamba na sio hadhi yao wakakutukana kisa ulikuwa unavaa marapu rapu na masamtula🤣🤣 wameolewa na mawaziri au mapedeshee au wameishia kuolewa na walewale waliowadharau wakiwa mabinti vigoli😄😄

Wapo wapi wale viranja wa shule waliokutesa kwa kimbelembele chao kama tai ya Afisa mikopo. Vipi wameishia wapi?😅😅

Unawakumbuka vipanga butu wa shule? Wazee wa connection za paper za necta waliokuwa wakipata paper zilizovuja. Walijisikiaje kukunyima Gaka alafu bado ukafaulu mtihani, au ukafeli lakini kwa sasa hawana mbele wala nyuma?

Wapo wapi walioacha wachumba zao baada ya kufika chuo; ati walitaka wasomi wenzao na watu wamjini hawakukutaka mwenzangu na miye wa Makanya kule Naivoli. Vipi ndoa zao zinaendeleaje huko?

Wapo wapi wababe wa mtaa na kijiji enzi hizo? Je, bado ni wababe au wameishia kuwa na majeraha miilini mwao kama paka shume😢😢

Wapo wapi waliomdharau Mama na Baba yako kwa umasikini wake, Leo Mungu amekuona wazazi wako wanaheshimika kwa ajili yako. Wapo wapi?

Wapo wapi waliokuacha kwa kejeli na dharau kisa hauna gari wala nyumba nzuri kazi yako ilikuwa kuzurura MJINI? Leo wanaendeleaje huko kwenye mandinga na majumba ya kifahari.

Wapo wapi waliokukataa kisa hauna chura😃😃😃 wala huna sura hata ya makeup wakaenda kuoa wanawake wenye matako na sura kama malaika. Unajua kinachowapata huko Kwenye ndoa?

Wapo wapi waliodharau kazi yako ya kuvuja jasho pesa Madafu wao wakataka kazi za tamaa. Leo wanaendeleaje kwenye ubilionea?

Jambo moja walipo kuwa hawajui ni kuwa jana sio leo.
Na kama bado wapo wanaokudharau waambie tuu leo sio kesho muda utaongea

Hakuna raha kama kuishi kwa upendo
Hakuna raha kama kuishi kwa kuheshimiana

Vijana mliopata msije mkajisahau mkadhani kesho itakuwa kama leo. Maisha yanabadilika
Yule unayemcheka leo usishangae kesho akawa jiwe kuu lako la pembeni

Wote tunaikumbuka jana ilivyokuwa. Tunawapost waliokuwa na maisha yakutamanika ambao leo wapo choka mbaya. Upo msemo usemao; mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Usitukane mamba kabla hujavuka mtu.

Vijana ambao bado Mnaonja joto la jiwe na mnadharaulika, msikate tamaa. Leo sio kesho. Pambaneni kwa uwezo wenu wote.

Hayo mnayopitia wengine tulishapitia tunajua uchungu wake ingawaje mimi nilikuwa nacheka(huwa nina Tabia ya kujicheka pale nikutwapo na madhila)

Wengi waliotucheka jana kwa dharau leo hii hawataki kuonana na sisi kwani mambo yamegeuka🤣🤣🤣🤣

Mwisho tuishi kwa upendo

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Yuko wapi yule jamaa aliyesema hajaribiwi, hatishwi na wala hapangiwi... yule aliyejifananisha na jiwe na kujibaraguza kutaka kuongoza malaika mbinguni?

Yako wapi yale mabunduki yaliyokuwa yanamlinda na kumpa jeuri? Ni kweli yamezidiwa nguvu na ziraili?

Nauliza yuko wapi?
 
Wako
WAPO WAPI? KWELI JANA SIO LEO; NA LEO SIO KESHO

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Maisha yanahitaji upendo. Ukijifanya mjanja subiri wakati wako maisha yatakapokufanya Mpumbavu

Yajana yanachekesha lakini pia yanaumiza. Lumaanisha ya leo wapo wanaoumia na kucheka lakini kesho itakuwa kinyume chake. Hata hivyo wapo salio hela jana na bado hata leo wanacheka. Pia wapo walioonja joto la jiwe Jana na bado wanakula Msoto mkali.

Maisha ni mabadiliko. Lolote huweza Kubadilika kwa yeyote kwa muda wowote. Hii tukilijua basi tutaishi kwa tahadhari tukipendana.

Unakumbuka Jana? Pengine hukumbuki vyema, ngoja tukumbushane; mtaniwia radhi pale hisia zangu zikinizidi mpaka kufikia kucheka au kulia. Haya nikukumbushe;

Wapo wapi wale waliokuwa na TV pekee yao kijiji kizima? Hawa walikuwa wengi wao wanasheria ngumu kweli, watoto wao walikunyanyasa? Wapo wapi leo ikiwa jana ilikuwa hivyo?

Wapo wapi wale waliokuwa wakitoka likizo Dar es salaam wakituringishia na kutuona washamba kisa hatujaenda Dsm. Shuleni wakitusumbua na Stori zao za viunga vya Dsm. Unajua walipo kwa sasa au unataka nikujuze?

Unawakumbuka wale masister Duu tukiwa under twenty twasoma walivyosumbua? Walikuwa hawali Kande🤣🤣 wala chakula cha shule. Madada wa biskut, chocolate na juisi. Unajua wanachokula sasa hivi??😀😀

Vipi wale vidosho tukiwa under 20 waliojaliwa maumbo na uzuri usiosemeka, walivyoleta tafrani pindi wakipita mitaani wakitingisha Makalio yao. Unajua walipoishia? 🤣🤣

Wapi ma-bitozi nyangema AKA mabishoo milegezo waliokunyang’Anya Demu wako enzi hizo unajua walipoishia?

Wapi walipo wale waliokuita mshamba na sio hadhi yao wakakutukana kisa ulikuwa unavaa marapu rapu na masamtula🤣🤣 wameolewa na mawaziri au mapedeshee au wameishia kuolewa na walewale waliowadharau wakiwa mabinti vigoli😄😄

Wapo wapi wale viranja wa shule waliokutesa kwa kimbelembele chao kama tai ya Afisa mikopo. Vipi wameishia wapi?😅😅

Unawakumbuka vipanga butu wa shule? Wazee wa connection za paper za necta waliokuwa wakipata paper zilizovuja. Walijisikiaje kukunyima Gaka alafu bado ukafaulu mtihani, au ukafeli lakini kwa sasa hawana mbele wala nyuma?

Wapo wapi walioacha wachumba zao baada ya kufika chuo; ati walitaka wasomi wenzao na watu wamjini hawakukutaka mwenzangu na miye wa Makanya kule Naivoli. Vipi ndoa zao zinaendeleaje huko?

Wapo wapi wababe wa mtaa na kijiji enzi hizo? Je bado ni wababe au wameishia kuwa na majeraha miilini mwao kama paka shume😢😢

Wapo wapi waliomdharau Mama na Baba yako kwa umasikini wake, Leo Mungu amekuona wazazi wako wanaheshimika kwa ajili yako. Wapo wapi??

Jambo moja walipo kuwa hawajui ni kuwa jana sio leo.
Na kama bado wapo wanaokudharau waambie tuu leo sio kesho muda utaongea

Hakuna raha kama kuishi kwa upendo
Hakuna raha kama kuishi kwa kuheshimiana

Vijana mliopata msije mkajisahau mkadhani kesho itakuwa kama leo. Maisha yanabadilika
Yule unayemcheka leo usishangae kesho akawa jiwe kuu lako la pembeni

Wote tunaikumbuka jana ilivyokuwa. Tunawapost waliokuwa na maisha yakutamanika ambao leo wapo choka mbaya. Upo msemo usemao; mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Usitukane mamba kabla hujavuka mtu.

Vijana ambao bado Mnaonja joto la jiwe na mnadharaulika, msikate tamaa. Leo sio kesho. Pambaneni kwa uwezo wenu wote.

Hayo mnayopitia wengine tulishapitia tunajua uchungu wake ingawaje mimi nilikuwa nacheka(huwa nina Tabia ya kujicheka pale nikutwapo na madhila)

Wengi waliotucheka jana kwa dharau leo hii hawataki kuonana na sisi kwani mambo yamegeuka🤣🤣🤣🤣

Mwisho tuishi kwa upendo

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
wapi waliotaka aongezewe miaka saba mingine atu? Wako wapi na waliojiita miyungu mutu?
 
Yuko wapi yule jamaa aliyesema hajaribiwi, hatishwi na wala hapangiwi... yule aliyejifananisha na jiwe na kujibaraguza kutaka kuongoza malaika mbinguni?

Yako wapi yale mabunduki yaliyokuwa yanamlinda na kumpa jeuri? Ni kweli yamezidiwa nguvu na ziraili?

Nauliza yuko wapi?
😃😃😂😂😂

Mungu anatujulia hakika

Kuna mambo ukiyatafakari yanautisho wenye mafunzo
 
Hivi yuko wapi yule mshamba toka Kolomije aliyelivamia jiji na kutamba kuwa ni mali yake na kuwataka wote wasiokuwa na kazi waondoke kwenye mkoa wake??

Fala yule alidhani jiji hili analijua kuliko wazaramo ....
Jana yake imepita na sasa anaiishi leo yake huku akiisubiria kesho yake
 
Back
Top Bottom