Wanajadili Historia ya Bibi Titi Mohamed lakini hakuna hata mmoja anaeijua historia yake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
22,062
32,207
Nimefikishiwa taarifa kuwa kuna Group la vijana leo kutwa nzima wanajadili historia ya Bibi Titi.

Mpashaji habari wangu kaniuliza maswali mengi kuhusu historia ya Bibi Titi na kama nilimfahamu wakati wa uhai wake.

Ukweli ni kuwa hakuna aliyemwandika Bibi Titi kama anavyostahili kuandikwa.

Historia ya Bibi Titi imekuwa kitendawili kama ilivyokuwa kitendawili kwa wazalendo wengi katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia zao ni kitendawili kinachosubiriwa kuteguliwa.

Nilimjua Bibi Titi toka udogo wangu kwa kumuona.

Ukubwani nilibahatika kuzungumzanae nyumbani kwake Upanga na kabla ya hapo nilifika nyumbani kwake Temeke alipokuwa akiishi baada ya kutoka kifungoni.

Bibi Titi aliwajua wazee wangu cha kiasi ya kuwatania aliponieleza kuwa akiwafahamu vyema wakiishi mitaa ya Gerezani, Dar-es-Salaam.

Naweka hapa video chache vipande vifupi, vifupi kuwezesha watu lau kwa kiasi kuifahamu historia ya Bibi Titi Mohamed na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

View: https://youtu.be/ja_cL5te4Lw?si=WEuF3XiyW-AaMNjF

View: https://youtu.be/tZtKiNdaiz0?si=6x4oy2p1jov5hFyY

View: https://youtu.be/MTO6IDmiSfU?si=GTkpa1jKO_levFyH

View: https://youtu.be/tZtKiNdaiz0?si=KskGajWl7rm5iJk-

View: https://youtu.be/j2_JpqAXeBs?feature=shared

View: https://youtu.be/H-lKHxRvBXM?feature=shared

View: https://youtu.be/EGlJS8PwzoA?si=-R20dx-_PyhHmp9x
 
Asante kwa historia, lakini nashangaa hapa leo haujamuandika Sykes...🙄
Ama labda umesahau...🤔
 
Asante kwa historia, lakini nashangaa hapa leo haujamuandika Sykes...🙄
Ama labda umesahau...🤔
Ushi...
Ushimen said:
Asante kwa historia, lakini nashangaa hapa leo haujamuandika Sykes...🙄
Ama labda umesahau...🤔

Ushi...
Ikiwa ni historia ya kuundwa kwa African Association, TANU na uhuru wa Tanganyika huwezi kuacha kuwataja akina Sykes.

1924 Kwegyir Aggrey anakutana na Kleist Sykes na anamweleza umuhimu wa Waafrika kuunda jumuiya yao.

1929 Kleist, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Cecil Matola Rawson Watts na Raikes Kusi wanaunda African Association.

1933 Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Jumbe Kiro kwa kuwataja wachache wanaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na chama hiki kinaunganishwa katika kupambana na ukoloni.

1950 Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi ukiwa uongozi wa vijana unaingia TAA na kuleta mapinduzi makubwa ya siasa.

1950 inaundwa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa Abdul Sykes, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, John Rupia na Steven Mhando.

Abdul Sykes anamwingiza Earle Seaton katika kamati hii kama mshauri kuhusu Tanganyika kama Mandate Territory.

1950 Abdul Sykes anakutana na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Kun'gu Karumba, Bildad Kaggia na Paul Ngei katika mkutano wa siri Nairobi.

1951 Abdul Sykes anajaribu kumshawi Chief David Kidaha Makwaia ajiunge na TAA wamchague Rais na 1952 waunde TANU.

1952 Julius Nyerere anapelekwa nyumbani kwa Abdul Sykes na Kasella Bantu.

1953 Ally Sykes anaandikiana na Kenneth David Kaunda wa Northern Rhodesia.

1953 Ally Sykes na Denis Phombeah wanakamatwa Southern Rhodesia wakiwa njiani kwenda Lusaka kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Kaunda na Henry Nkumbula.

1953 Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika wanakwenda Nansio, Ukerewe kwa Hamza Mwapachu kutaka kauli yake ya mwisho kuhusu kumwingiza Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 TANU iundwe.

1953 Abdul Sykes na Nyerere wanagombea nafasi ya Rais wa TAA Ukumbi wa Arnautoglo Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) akiwa Denis Phombeah.

Nyerere "anachaguliwa," President Makamu wake Abdul Sykes.

1954 TANU inaundwa Nyerere akiwa President.

Kadi ya TANU No. 3 Abdul Sykes, No. 2 Ally Sykes na No. 1 Julius Nyerere.

Kadi 1000 za mwanzo alinunua Ally Sykes kutoka mfukoni kwake na ndiye msanifu wa kadi ya TANU.

Vipi mimi niwe hapa nafundisha historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU nisitaje majina muhimu katika historia hii kuanzia mwanzo mwaka wa 1924?

Bahati mbaya nafsi yako inakereka na majina haya ya Sykes kuwa sehemu ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wewe si wa kwanza wala hauko peke yako.

Wapo waliokutangulia katika hili na wakayafuta majina haya.

Hii ndiyo sababu wewe leo unahisi hayastahili kuwapo katika historia.

Hivi sasa majina haya yamo kwenye Cambridge Journal of African History na Dictionary of African Biography.

Mimi sijaghafilika kumtaja Kleist Sykes na wanae katika historia ya Bibi Titi.

Nitakueleza.

Ilikuwa kama kesho TANU inafanya mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja, Bibi Titi Mohamed, Tatu bint Mzee na wanawake wengine na ile kamati ya ndani ya TANU wanakusanyika nyumbani kwa Abdul Sykes kupanga mikakati ya nini kifanyike kuujaza uwanja.

Labda haya yangekuwepo toka mwanzo usingeshangaa.

Waliosahau ni wale walioandika historia ya TANU na majina haya yakawa hayamo katika vitabu vyao.

Hilo ndilo la kukushughulisha wewe.

Si hili la kunikejeli mie ati nimesahau kuwataja akina Sykes.
 
Nimefikishiwa taarifa kuwa kuna Group la vijana leo kutwa nzima wanajadili historia ya Bibi Titi.

Mpashaji habari wangu kaniuliza maswali mengi kuhusu historia ya Bibi Titi na kama nilimfahamu wakati wa uhai wake.

Ukweli ni kuwa hakuna aliyemwandika Bibi Titi kama anavyostahili kuandikwa.

Historia ya Bibi Titi imekuwa kitendawili kama ilivyokuwa kitendawili kwa wazalendo wengi katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia zao ni kitendawili kinachosubiriwa kuteguliwa.

Nilimjua Bibi Titi toka udogo wangu kwa kumuona.

Ukubwani nilibahatika kuzungumzanae nyumbani kwake Upanga na kabla ya hapo nilifika nyumbani kwake Temeke alipokuwa akiishi baada ya kutoka kifungoni.

Bibi Titi aliwajua wazee wangu cha kiasi ya kuwatania aliponieleza kuwa akiwafahamu vyema wakiishi mitaa ya Gerezani, Dar-es-Salaam.

Naweka hapa video chache vipande vifupi, vifupi kuwezesha watu lau kwa kiasi kuifahamu historia ya Bibi Titi Mohamed na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

View: https://youtu.be/ja_cL5te4Lw?si=WEuF3XiyW-AaMNjF

View: https://youtu.be/tZtKiNdaiz0?si=6x4oy2p1jov5hFyY

View: https://youtu.be/MTO6IDmiSfU?si=GTkpa1jKO_levFyH

View: https://youtu.be/tZtKiNdaiz0?si=KskGajWl7rm5iJk-

View: https://youtu.be/j2_JpqAXeBs?feature=shared

View: https://youtu.be/H-lKHxRvBXM?feature=shared

View: https://youtu.be/EGlJS8PwzoA?si=-R20dx-_PyhHmp9x

Asante.
P
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom