Baraka Sabi
Member
- Mar 16, 2017
- 19
- 14
WAKUU, AMANI NA IWE NANYI. Ni lengo la sera ya elimu ya mwaka 1995 na 2014 kuwa na Mtanzania aliyeelimika, mwenye maarifa, stadi na mtazamo chanya katika kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa la Tanzania.
Nikiri tu kwamba, Serikali imefanikiwa kuwaelimisha kwa kuwapa maarifa na stadi walimu wasio na ajira, elimu isiyo na mchango chanya katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
Walimu hawa hawana tofauti na bidhaa (commodities) nyingine sokoni ambazo hazina budi kuzalisha faida/ return kwa mfanyabiashara. Wakiwa vyuoni (Daraja la IIIA, Diploma na Vyuo Vikuu) Serikali iliingia gharama kubwa kuhakikisha walipo kuna miundombinu ya kutosha, kama vile:- majengo na mifumo yake yote, vifaa toshelevu vya kujifunza na kujifunzia, lishe bora na ya kutosha halikadhalika wakufunzi na wahadhiri. Uwekezaji huu si mdogo hata kidogo. Kitendo cha bidhaa hii kukosa soko ili Serikali iweze kuvuna jasho na faida ya uwekezaji wake si tu ni hasara kwa Taifa bali mzigo.
Kitendo hiki kimeleta maumivu makubwa kwa Serikali, wahusika wenyewe, familia zao, ndugu zao na jamii wanamoishi. Hapa chini ni ushauri wangu kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ikiwa itawapendeza.
(i) Kupunguza kasi na idadi ya udahili wa wanafunzi wa kusomea ualimu katika vyuo vyote vya ualimu nchini.
(ii). Wizara itambue kwa dhati ya moyo wake mchango na umuhimu wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu nchini kupitia ushirika wa PPP (Public- Private Partnership. Ziko taasisi zisizo za kiserikali nchini mfano taasisi za dini nk. zimeanzisha vituo vya kutolea elimu kwenye maeneo yao. Wawekezaji kama hawa ni wa kushika mkono. Serikali itengeneze mazingira ya kuwapa walimu kwa makubaliano yatakayoridhiwa na pande zote mbili ili kupunguza "stock" ya walimu iliyojaa gharani.
(iii). Serikali iongeze kasi ya kuajiri walimu kwenye shule zake za umma. Kwa idadi ya wanafunzi 20-40 Kwa mwalimu mmoja(Shule ya msingi) na wanafunzi 40-50 Kwa mwalimu mmoja (Sekondari) ni dhahiri uhitaji wa walimu ni mkubwa.
HII INAWEZEKENA. AMANI NA IWE NANYI TENA.