Wakuu hivi huwa mnadili vipi na watu wa aina hii? Please naomba mawazo yenu

Ukicheka na Nyani utavuna mabua,wateja watapakimbia hapo mgahawani kwako siku sio nyingi.
Huo usumbufu na uchafu wao utakuwa kero kwa wateja na wahudumu.Hawajaanza kudhuru watu na kupiga mayowe hovyo?watakuletea nuksi mgahawa utakuwa kama kibanda tu.
Fukuza fukuza!Acha kuwachekea wamekuja kukufanyia chuma ulete hao...
Mkuu umeongea points, Yani wananikera sometimes hata ukiwapa chakula hawaridhiki wanakuja tena, alafu wanaanza kuomba omba hela wateja, yani wananikosesha raha,
 
Ningekuwa na-click report kila wakitokea, au nawachonganisha na moderator(s) aliye zamu awape ban.
Haha, mkuu ujue hii ni serious issue,
Unakuta nikishaona simu ya muhudumu tu baasi najua wageni wameshavamia
 
mkuu wewe teua mmoja ya wafanyakazi wako awe mlinzi wa muda kushughulika na hao unaowaita vichaa. akitokea ampe ngumi kadhaa za uso, kesho haji tena, hakuna kichaa anayekula hotelini kila siku.
** Ila Ndugu una huruma za mshumaa, unamulikia watu wengine wewe unateketea.
 
Hongera kwa kuwasaidia!!! Usiache kuwasaidia ata kama wanafanya makusudi ila wakiongezeka itabidi uwe serious kidogo itakua utani sasa. Cha kufanya waanzishe tabia ya kuwapeleka nyuma ya restaurant wakale. Ili mda mwingine wajue pa kwenda na sio kuja kukaa kwa wateja.
 
Tafta mlinzi akae hapo mlangoni akiwaona tuu awatimue wasiingie ila wasikuone wewe uwe umekaa kwa mbali.......
Lkn kama unaona unajiweza Fanya kama sadaka kila Sikh wakija wape tuu mungu atakulipa..... Lakini usiwakalishe sehemu wanapokaa wateja kuna baadhi ya wateja wana kinyaa so unaweza ukapoteza wateja
 
Zoezi hilo litanifanya niwe nakaa pale muda wote ili kuangalia usalama manake muda mwingi wanakuwa wafanyakazi, Sasa nahofia wanaeza wakagombana na huyo mvuta bangi then wakavunja vitu vya vioo,
Ila nitajitahidi niufanyie kazi huu ushauri
wakamate uwapeleke hospital .
 
Jenga kitu kama uzio mfupi wenye geti katikati yaani wateja wote wawe wanaingilia na kutokea hapo kusiwe na njia yeyote nyingine ya kuingilia hapo au kutokea afu muweke mlinzi awe anachuja watu wasioeleweka hasahasa hao vichaa.kazi imekwisha.
Mkuu hili wazo lako nahisi linaweza likaniokoa, shukran
 
Una moyo wa kibinadamu sana mkuu.
Kama unaona wanakutia hasara, basi wafanyie mpango wa kutunziwa
ukoko ambao haujaungua ili wawe wanapatiwa wakija.
Zungumza na mpishi wako kwani kuwafukuza itasababisha thawabu yako kupungua.
Yawezekana baraka unayoipata ya wateja kula hapo, inatokana na hao vichaa.
Mkuu kuwapa chakula sio tatizo, hasahasa hawa wawili waliopo. Wasiwasi wangu ni pale endapo wataongezeka au kama wakifanya fujo, hasahasa huyu wakike ndio mkorofi sana, muda mwingine nawaza nikawaite madokta wa mentaly waje wawakamate
 
Decide kama wataka kuwasaidia na uweke budget yao kabisa, na ulimit ni wangapi. Huwezi wamaliza hao, watakuja buku. When you decide uwezo wako ni wa kusaidia wawili, weka budget yao na wakija, unawapa wanasepa kwenda kulia popote, sio hapo hapo. You have paying customers, they need that service, ukiwachanganya nao unawakosea wateja, you will fail your business, na wewe utakosa kipato, na wao watakosa chakula, priority is business!
Shukrani sana mkuu, Umetumia busara sana, na kuanzia hapa angalau nimepata pa kuanzia,
ubarikiwe mkuu
 
Ushauri mzuri, lakini nahisi angewafukuza tu yeye mwenyewe ili mazoea yaondoke
Kwa jinsi ninavyoonekana na nilivyojiweka pale, watu watanishangaa sana wakiniona nafanya kitendo hiko, na nadhani heshima itashuka,
Labda nimuajiri mtu kwa kazi hiyo
 
Hahaaaaa kwa hiyo mkuu huyo kichaa alimstua mwenzake na kumwambia oya vip mimi huwa naenda kununua msosi pale twende na wewe ukanunue ili tumchangie mshikaji.!?
Hahaha, Wnaleta usanii ndani ya jumba la sanaa
 
Pengine labda ni wapelelezi (spy) wametumwa na watu waje kukuchunguza..

Huenda labda ni vichaa kweli hawana sehemu maalumu ya kula

Au labda ni wazima lakini wanajifanyisha.... mjini kuna mbinu nyingi aisee

Cha msingi fanya upembuzi yakinifu halafu utoke na maamuzi sahihi ila usiwafukuze kwanza..FIKIRI KABLA YA KUTENDA
 
Ndo tatizo la vichaa.. akishakariri hapa pana menu anakuwa kama sisimizi... anawaita wenzie wote waweke kambi..!!!
 
Back
Top Bottom