Wakuu hivi huwa mnadili vipi na watu wa aina hii? Please naomba mawazo yenu

Ukicheka na Nyani utavuna mabua,wateja watapakimbia hapo mgahawani kwako siku sio nyingi.
Huo usumbufu na uchafu wao utakuwa kero kwa wateja na wahudumu.Hawajaanza kudhuru watu na kupiga mayowe hovyo?watakuletea nuksi mgahawa utakuwa kama kibanda tu.
Fukuza fukuza!Acha kuwachekea wamekuja kukufanyia chuma ulete hao...
 
Sasa mkuu kwamfano ungekuwa ndio wewe ungewachukulia hatua gani? Manake sometimes nafikiria hata nimuajiri mlinzi kwaajili ya kazi hiyo tu

Ningekuwa na-click report kila wakitokea, au nawachonganisha na moderator(s) aliye zamu awape ban.
 
Jenga kitu kama uzio mfupi wenye geti katikati yaani wateja wote wawe wanaingilia na kutokea hapo kusiwe na njia yeyote nyingine ya kuingilia hapo au kutokea afu muweke mlinzi awe anachuja watu wasioeleweka hasahasa hao vichaa.kazi imekwisha.
 
Una moyo wa kibinadamu sana mkuu.
Kama unaona wanakutia hasara, basi wafanyie mpango wa kutunziwa
ukoko ambao haujaungua ili wawe wanapatiwa wakija.
Zungumza na mpishi wako kwani kuwafukuza itasababisha thawabu yako kupungua.
Yawezekana baraka unayoipata ya wateja kula hapo, inatokana na hao vichaa.
 
Wadau bila kupoteza muda naomba tujadiliane kuhusu hili,
Kuna mtu mmoja mwenye matatizo ya akili(kichaa) alikuwa anakuja kwenye restaurant yangu sasa kutokana huruma za kibinadam nikawa namwambia muhudumu ampe tu chakula,
basi kidri siku zinavyozidi kwenda akawa anakuja kilasiku, na ikitokea labda mimi sipo au labda nikimkaushia(asipopewa msosi) huwa anaanza kuwasumbua wateja kwa kuwaomba hela au anakaa kwenye viti muda mrefu sana, kiasi mpaka anaziba siti za wateja wengine,
Hilo sio tatizo, sasa tatizo linakuja skuizi kuna mwingine nae anakuja so wanakuwa wawili, na anafanya action kama anazofanya kichaa mwenzake,
Wakuu sio kwamba sipendi kuwasaidia ila naona sasa watanivurugia mauzo pamoja na kunifukuzia wateja,
hasahasa ukizingatia appearance zao.
Naombeni mnishauri nifanye nini?
Nahisi nikiwafukuza wateja watanichukulia sina utu.

Sometimes unakuta nimekaa na marafiki zangu tunakula alafu ghafla unaona yule kichaa huyoo anaingia anakaa kwenye kiti, basi unakuta roho inaniuma kumfukuza nataka lakini nahisi itajenga bad image kwa marafiki hivyo nabaki kumtazama tu.
Hebu nishaurini wadau manake nisipokuwa makini Resta yangu itafilisika.

Decide kama wataka kuwasaidia na uweke budget yao kabisa, na ulimit ni wangapi. Huwezi wamaliza hao, watakuja buku. When you decide uwezo wako ni wa kusaidia wawili, weka budget yao na wakija, unawapa wanasepa kwenda kulia popote, sio hapo hapo. You have paying customers, they need that service, ukiwachanganya nao unawakosea wateja, you will fail your business, na wewe utakosa kipato, na wao watakosa chakula, priority is business!
 
Tafta mtu Mvuta bangi mpe mchongo mzma akiona wanakuja awatimue we kaa mbali sehem ambayo watu hawakuoni wenzio ndo wanavyofanyaga hivyo
Ushauri mzuri, lakini nahisi angewafukuza tu yeye mwenyewe ili mazoea yaondoke
 
Ukicheka na nyani utavuna mabua niite nije nipige maombi uone kama awajakata mguu hahahaha
 
Hahaaaaa kwa hiyo mkuu huyo kichaa alimstua mwenzake na kumwambia oya vip mimi huwa naenda kununua msosi pale twende na wewe ukanunue ili tumchangie mshikaji.!?
 
Endelea tu kuwaita vichaa wakati wenzio washakusoma na wanaendelea kupiga msosi wa bure. Muda si mrefu utakuwa unalisha familia nzima ya 'vichaa'.
ndo zao hizo siku hizi imentoka juzi hiyo Niko sehemu kaomba ela akapewa akaja mara kaja mwingine nkamuambia mwenzio katoka sasa hivi hapa
 
Mkuu wachunguze ujue kama ni vichaa kwel au la! Usije ukakuta ni wazima lakin wanapretend ili kupata chakula kirahis
 
Ndo baraka zenyewe hizo mbabaa then tushakujua una mgahawa
Baraka wakati napata hasara? Muda mwingine wanakuja marambili, sometimes hata uwape chakula hawaondoki, wee unadhani nitafanya nini?
 
Back
Top Bottom