Uyu mama kama angekua na akili and I hope she was, angekatia insurance hio nyumba baada ya kumaliza tuu maana najua alikua anafahamu kabisa alivunja sheria kujenda pale
Huyo mama yenu ni jipu la kisiginoniYote yanawezekana inawezekana mama mchungaji alitoa kidogodogo kwa maofisa wa NEMC sasa wamemgeuka ila sheria ni msumeno,inakula mebele na nyuma ngoja tusubiri tuone
hao nemc ndio wanaotoa vibali vya ujenzi? kama ni kweli, inatakiwa kuangaliwa kwenye ramani, je, hapo alipojenga ni ramani sahihi ya jiji inayoruhusu jengo kujengwa, jibu likiwa ndiyo basi wasimsumbue mama wa watu, ila jibu likiwa hapana, basi hilo ni jipu, wahusika waliomruhusu(si atakuwa na nyaraka) wakamatwe na kuhojiwa waliruhusu vipi wakati haparuhusiwi kujengwa, na jengo libomolewe mara moja. imefika kipindi hata majaji na mahakimu wanaotoa maamuzi ambayo hayana maslahi na nchi wafukuzwe kazi wapewe majaji wengine wenye faida kwa taifa. maslahi ya wengi ni ya muhimu zaidi kuliko mtu mmoja.
mbona hata yangu ilikua na thamani kubwa saana kwa haka kauwezo kangu? ibomolewe tu.Nimesoma habari hii kwenye Mwananchi la Leo. Kuna para moja Wakili Msomi Msemwa anasema ya kwamba " nyumba ya mteja wangu ina thamani kubwa na hana sehemu ya kwenda ikibomolewa". Nikajiuliza, kwani wale wa jangwani si walienda mabwepande! Na yeye aende huko!
Lengo sio kuisoma namba wala herufi, lengo turejee kwenye mstari sahihi. Tusiishi kama taifa holela ambalo mtu anakurupuka huko aliko, anatuongoza kwa miaka 10 halafu jamii anaiacha inaishi kama swala na punda mwituni. Lazima sheria na taratibu zote zisimamiwe...ndio!!...zisimamiwe. Ushabiki maandazi wa kiitikadi tuuweke pembeni, lets discuss issues. Tumsaidie Rais hata kama chama chake hatukipendi tupende usimamizi wake wa sheria na kanuniBado natafakari, nani anaisoma namba haswaa!!!
Kuna kitu kinaniambia hii nyumba hii haitabomolewa!. Mimi ni Tomaso, siamini kuwa nyumba hii itabomolewa mpaka pale itakapobomolewa!, it is not done until it is done!, and it is not over until it is over!,
Pasco
Kumbe serikalini kuna mkubwa zaidi ya Magufuli!!Pasco I can understand your concern,
Halima Mdee kule Twitter anasema yuko "mkuwa Wizara ya Ardhi" ambae abambeba isibomolewe
Nikaanza kuwaza tu mengi bila majibu