KERO Wakazi wa Malela, Tuangoma (Kigamboni) tunaishi kwa mashaka sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwanini kipindi chote raia wanajenga Nssf isiwastopishe?

Mmeacha mpaka watu wamemaliza ujenzi na kuamia katika makazi yao alafu leo hii nyumba zote zimewekwa X-Bomoa!

Muda wote mlikuwa wapi kuzuia watu wasijenge kwenye hayo maeneo?

Naomba serikali iangalie kwa jicho la pekee wananchi wake wanaoteseka na kuishi kwa mashaka ya kukosa makazi yao huko malela

20240610_062325.jpg

20240610_062345.jpg
 
Wananchi wa Malela Toangoma mkabala na nyumba za NSSF wameamuliwa kuhamisha vitu vyao na kutafuta makazi sehemu nyingine ili kupisha zoezi za ubomoaji wa nyumba za wananchi waliokuwa wakiishi hayo maeneo, zoezi hilo limewajumuisha pamoja na wale waliojenga kwa chini katika bonde linalopitisha maji kwenda mto Mzinga ambao wanayatazama maghorofa ya NSSF (wamezungukwa na magorofani ya NSSF ) zoezi hilo limeanza kwa kuwekwa X nyumba za wananchi miambili (200) mpaka kufikia tarehe 10 June 2024, wote waliojenga kwenye hilo bonde.

SWALI LA MSINGI
Uongozi au mamlaka husika za NSSF zilikuwa wapi kipindi chote hicho raia wanaanza zoezi la ujenzi? Kwanini wasiwazuie na wakawaacha mpaka wamemaliza ujenzi na kuhamia kwenye makazi yao?

Kiukweli hili jambo halijakaa sawa kwa sababu viongozi wa NSSF walikuwa wanaona na hawakuchukua hatua mapema, kuwabomolea wananchi nyumba zao ni ukatili mkubwa na sio jambo zuri kitakaa.

TUNAOMBA SERIKALI IWAANGALIE KWA HURUMA NA UKARIMU WANANCHI WAKE WA MALELA TWANGOMA

BAADHI YA NYUMBA ZILIZOWEKWA X

20240611_083104.jpg
20240610_062327.jpg
20240610_062345.jpg
 
Kwanini wanavamia maeneo na kujenga nyumba wakati sio yao?

Na kama waliuziwa basi taratibu za kununua ardhi zinafahamika. Ndio shida ya kupenda vya bei rahisi.

Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Mtihani mgumu sana huo ila ni vema sana kujiridhisha kabla ya kununua eneo na kuanza ujenzi hapa jirani yangu Kuna eneo linatambulika kama eneo la shule na shule zipo msingi na sekondari na wengi walishahama wakazi ila kuna watu wamekuja wamejenga fasta nyumba ziko juu najiuliza Hawa watu ubomoaji ukianza watasemaje!?
 
Kwanini wanavamia maeneo na kujenga nyumba wakati sio yao?

Na kama waliuziwa basi taratibu za kununua ardhi zinafahamika. Ndio shida ya kupenda vya bei rahisi.

Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.
Hawakuvamia waliuziwa katika utaratibu unaotambulika kisheria chini ya ofisi za serikari ya mtaa chini ya mwenye kiti kama inavyofahamika kisheria, wapo kwa muda mrefu sana takribani miaka 10
 
Back
Top Bottom